Ya Feisal, Yanga na maamuzi ya TFF

Mtu atoke nyumbani arudishe Sare za mwajiri eti nimeacha kazi Tangu Jana? Kama taratibu na kuacha au kuqchishwa kazi ni rahisi kiasi hicho Nani angebaki kazini? Kuna watu Kila kitu kwao ni ushabiki Tu hata masuala ya Kisheria..
Inawezekana kabisa si ni maslahi tu. Mtu analipwa m4 ana nn cha kupoteza kama maslahi yamewekwa mezani? Unadhani akipewa pesa nzuri atabaki kuwa loyal kwa klabu huku ana njaa?
 
Umeandika kitu gani?au bado kuna vitu kichwani?
Kwa mkataba wa thamani ya M4 ukilinganisha na anachofanya yule mtoto uwanjani hata shabiki mwenzangu wa simba mzee vesoP anamlipa fei mishahara ya miaka 5 aachane na utopolo asitufunge yale magoli ya mbali. Mpira ni burudani na biashara. Wachezaji wanatafuta maslahi tupate burudani na wadhamini wapate biashara halafu nyinyi mnataka wajitolee kwa posho ya m4.
 
Pamoja na yote uliyo andika Feisal bado ni mali ya Yanga utake usitake
 
Fei Toto ni mchezaji wa Yanga, timu inayomtaka itoe hela hakuna dezo!
 
unajua we ni mjinga sana Feisal ni mchezaj halali wa yanga we endelea kujifariji maisha sio marahisi hivyo na usipende short cut kwenye maisha
 
Hakuna cha bure unataka mchezaji toa Hela sio janja janja.
 
Kweli. Mzeee feisal anapiga. Football vyema kabisa cha msingi pesa aongezewe
 
Hili suala la fei naona limejaa majungu tu
 
Mapenzi kwa vilabu vyao,umbumbumbu na chuki dhidi ya vilabu pinzani ni tatizo Sana.
 
Ni bora uache dharau. Jamiiforum tunatumia ID fake, wee unauhakika gani kua mleta mada hausian na TFF
 
Siku hizi ushakuwa mtaalamu wa sheria?
 
Wengi wanaogopa mashuti ya Feisal siku wakikutana na Yanga.Wameshasahau Kuna K Azz. Kipa wao ilifikia hatua ikikaribia mechi ya Yanga na Simba anajiumiza vidole Kwa maksudi Ili asicheze mechi hiyo. By redio


Bonge la comment
HPo umenena,ni bora kuwaambia ukweli wajue kuwa azizi k bado yupo,wasijifanye wanaruka mkojo kumbe wanakanyaga bonge la timba
 
Imekaa poa Sana..!! Wengi hawana weledi na mambo ya kisheria..!!
 
Yaani hata mi nilishangaa kuona watu wanashupaza shingo kwa kesi nyepesi namna hii.
Ilikua wazi kabisa kua Feisal kaingia mkenge na hata mwenyekiti wa serikali ya mtaa alikua anaweza amua kesi hii😄
Aliingizwa cha kike na waliomshauri. Hata huko CAS akienda, lazima aangukie pua tu. Mkataba hauwezi kuvunjwa kizembe hivyo. Talaka yenyewe lazima wanandoa waende mahakamani
 
Taarifa ya TFF Ina Mapungufu Mengi sana.

Utadhani meandikwa na watu waliokosa Elimu.
 
Mnaongea kishabiki sana.Fikiria ingekuwa upande wa pili yaani yanga wenyewe wanaamua kumuacha mchezaji,je ni lazima akubaliane nao kwa maana mnayoisema pande mbili kukubaliana?

Tumieni akili zenu za kawaida.Ukiwa na mfanyakazi na ukaamua kumuachisha kazi unamlipa stahili zake kulingana na mkataba na sheria zilizopo.
Vivyo hivyo mchezaji akitaka kuvunja mkataba,kama kipengele cha kulipa fidia ama kuununua kipo,mchezaji anafanya hivyo

Utopolo wa yanga ni pale walipoweka kiasi kidogo cha kuununua mkataba sasa baada ya Fei kuonekana wa moto,wanaona milioni 100 haitoshi.

Ni kwa nini waliandika hiyo 100M na mishahara ya miezi mitatu?
Je inalipwa wakati gani hiyo kama siyo katika mazingira kama haya ya sasa?

Acheni kumfanya mchezaji mtumwa.Waarabu walikuja na ofa ya 600M huku Fei akiahidiwa mshahara mkubwa,utopolo kwa jinsi mlivyo na roho mbaya mkakataa.Na bado hamkumuongeza mshahara.Kwa nini mnawafanya wachezaji watumwa?
Kuna vijana hapo mmeajiri upande wa habari vimeshakuwa vigagula tu.Kila siku kujaribu kuuonesha umma Fei si kitu kwamba yupo Aziz!!!
Vijana mnakuwa wajinga kiasi hiki?Hivi Fei ni wa kulipwa milioni 4 halafu Manara analipwa milioni 11??! Kwa kipi?
Aziz ni wa kulipwa milioni 25 na Fei 4 kweli?Mbona mnakuwa na roho za kichawi sana.
Halafu msivyo na shukrani,kijana alicheza kwa moyo hadi mwisho ila mnamkejeli!!
Vigagula wa utopolo !!

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…