jitombashisho
JF-Expert Member
- Jun 11, 2020
- 667
- 2,245
Wengi kama si wote bado hawaelewi ni kwa sababu gani hasa vyama vikongwe kama CCM vinaendelea kubaki madarakani. Jibu ni moja, uimara na ubora wao katika nyanja ya mikakati imara na ubobevu wao katika suala la ukachero chanya uhusuo maisha ya CCM yao. Huo ndiyo msingi wa ukongwe wao na ni kweli kwalo CCM ni JABALI!
Francis Nanai kwa mfano, ni mmoja wa wana-mikakati na kachero aliyepelekwa kwa makusudi kabisa kwenda pale Mwananchi kwa maslahi ya nchi na CCM na wengi wetu hatukulitambua hilo. Leo, mwana mkakati huyo amefanikiwa kwa kiwango chake kuyatimiza malengo yaliyo mpeleka pale Mwananchi Communication. Na hivi punde, kwa kazi bora aliyoifanya anaenda kupewa zawadi ya Ubunge na baadae ndiye atakuwa Waziri mdogo wa Habari. 'Muda utaongea.'
Funzo kwa Vyama vingine; ni lazima kwanza mkuze/mkue uwezo wenu wa intelijensia. Pia, mtambue ni ngumu kwenu kukua kwenye nchi zenye magwiji wengi wa fitina pasi na ninyi kuwa sehemu ya.
CCM tupende au tusipende bado ipo ipo sana katika nchi hii. Na hii ni kwa sababu imewekeza pakubwa mno katika kupata taarifa za kiintelijensia kutoka pande zote. Na hata hao tunaowaita wenye vyama vyao vya Upinzani usikute pia wao ni sehemu ya wana mikakati ya CCM.
CCM ni hatari!