Mkuu watu wakuangalia na kelele zako, mfumo unaanza tangu "O" Level, ukifanikiwa kupata Div. "I", kuanzia hapo unapigwa jicho la mbali, na ukapata Div "I" au "II" unapofika 'A' level, si ajabu ukifika chuo wewe tayari umekuwa wao tuu, hapa CCM na Dola ni wamoja au itokee unakipaji cha uongozi hawakuachi. Katika hili wapo wachache walio fanikiwa kucholopoka, lakini ni wachache sana.
Hata ikatokea wamefahamu wewe ni Big brain na upo kwenye chama cha upinzani utachukuliwa tuu, hata kwa fitna. Na wasipo fanikiwa basi lazima upambane na mizengwe udhoofishwe.
Uongozi wa vyama vya Upinzani ni vigumu sana kupata akili kubwa na wakadumu nayo. Hio ndio hali halisi, wataweza kupata watu wazuri lakini uzuri wao ukianza kuchipuka basi wataondoka na upinzani ukibaki nao hao wasomi, basi ujue wasomi hao hawana madhara.
Tafuta mtu yeyote aliyepata First Class University ambaye hajasumbuliwa na lazima watamchukua tuu. Hii sera ya Serikali karibu zote duniani ama Africa au Ulaya au Marekani.
Wenzetu watu hao wanakua katika mfumo mkuu wa utumishi sisi wanatumika kote. Ndio maana Chadema wanaposema ni Chama cha wasomi, wabobezi hucheka sanaa, sababu wanakuwa na wasomi makapi lakini prime talents zote wanachukua.
Na hivyo ndio nchi inavyoendeshwa.
Jee wajua Makatibu wakuu au Wajumbe, viongozi wote wasomi wa vyama vya upinzani kuna siku wanarudi CCM.
ELIMIKA HIYO NDIO DUNIA INAVYO ENDESHWA; NATAWALA HALAFU SILAHA ZA MAAGAMIZI NIKUACHIE WEWE MPINZANI ILI IWE NINI?