Elections 2010 Ya Gazeti la Raiamwema na makala za Mbwambo; Tujadili hoja

Elections 2010 Ya Gazeti la Raiamwema na makala za Mbwambo; Tujadili hoja

Tafakari kwanza ningekushauri ubadiri jina kwani alilingani na hayo uliyo yaandika.Huna sifa ya kutafakari.Kama sikosei nafikiri wewe nia MAKAMBA katibu mkuu wa ccm kwani tumemzoea kwa kua na kauli zinazofanana na hizo.Uadirifu wa Pinda,Slaa,Mwakyembe,Sitta na Watanzania wengine wengi unauhusiano gani na kazi za JK.Je unajua ujenzi wa chuo kikuu DOM ilikua ilani ya chama gani?.Mbwambo anapomshauri kujifunza kwa Kagama anamaanisha nchi iliyoku katika vita vya muda mrefu baada ya kupata kiongozi imara katika kipindi kifupi imeweza kuipita Tanzani.Nchi yenye amani ,madini na rasilima n.k.JK anamapungufu mengi ambayo tukiyanyamazia kama wewe ataipeka nchi kubaya.Hivyo ndio maana watu wenyekutafakar wanauvalia njuga udhaifu wake na wasiotafakari kama wewe mnamsifia na kusifia vitu ambavyo havina uhusiano na JKMUNGU IBARIKI TANZANIA
Gazeti hili na hasa makala ya Johson Mbwambo ni za chuki za wazi kwa JK imekuwa ada kwa makala za Mbwambo kila wiki kumsema,kukejeli na kumkosoa vibaya JK.kwa muda mrefu sana hali hii inatia kinyaa na kumuona Mbwambo ni mtu asiyeaminika.Tukumbuke kuwa kabla ya kampeni za uchaguzi mtu huyu aliandika makala huku akisema kuwa Waandishi wazingatie maadili katika kipindi hiki.
Lakini mlolongo wa makala zake toka mwanzo wa kampeni umeanza kwenda kinyume na kile alichokiandika kabla ya kampeni.Umeanza kuonyesha kuwa Mbwambo amekuwa na agenda yake iliyojificha dhidi ya JK.Mara aseme kimfaacho Jk ni asasi na si urais huku akisahau kuwa ni Kikwete huyu huyu ambaye amekuwa madrakani kwa miaka mitano iliyopita huku Mbwambo akiwa kama mwananchi wake. Hili ameliandika katika makala yake ya jana 06/10/2010.Amefikia mahali akathubutu hata kuandika kuwa inafaa JK akajifunze kwa Rais Kagame wa Rwanda.Sina hakika kama alitaka JK akajifunza kutumia nchi za wengine kufadhili ghasia na kutumia nafasi hiyo kusaidia nchi yake au alimaanisha JK akajifunze jinsi ya kuwanyima wapinzani uhuru na kutishia vyombo vya habari,sijui hasa alimaanisha nini.Labda Watanzania wenzangu mtanisaidia.
Hivi Ukubwa wa Tanzania utaufananisha na Rwanda? kama kujifunza kwanini Kagame wa Rwanda asije kujifunza kwa JK KWENYE ujenzi wa Chuo kikuu cha kuigwa cha Dodoma?Mbwambo hivi Rwanda wana chuo kama UDOM? umeshindwa kumpa heko JK hata kwa jambo kama hilo?Au wewe ndo ulipanga shughuli hiyo?Maandishi ya MBWAMBO hayana tofauti na mwandishi anayetumia jina la bandia anayejiita MSOMAJI RAIA hawa ni kama mapacha na Mbwambo kuanzia mtiririko wa uandishi wao,mawazo hasi dhidi ya JK, chuki zao za wazi zisizo na sababu kwa JK .HUYU MSOMAJI RAIA kaanza kuandika toka mwaka jana kuwa Rais Jk hashauriki. Hiyo ilikuwa mwezi wa tisa 2009. mwaka huu kajisahau kaandika kuwa Rais Kikwete anasikiliza marafiki zake sana. sasa mtu ambaye hashauriki atasikiliza marafiki na watu wake wa karibu?Cha ajabu minal rahman Mbambo kawahi kuandika makala kumsifu waziri Mkuu Mizengo Pinda kama waziri makini na mtendaji ni swali je aliyemteua Pinda si ndio JK? kazi hizo zinazo mfurahisha Mbwambo ndizo za JK.anafanya kwa maelekezo ya JK. HII NI DOUBLE STANDARDS.MFANO gazeti la jumatano ya jana Mbwambo karudia habari ya World Economic Forums uliofanyika Dsm 5-7 Mei 2010.
huko nyuma aliwahi kuandika makala ya kukebehi mkutano ule kwa vile tu mgeni Rasmi alikuwa JK.imekuwa kama Mbwambo ana allergy na jina la JK.ameamua kuwa anarudia rudia maneno ya kumchafua JK.NAJIULIZA kama Mbwambo angepewa fursa ya kuambiwa ukimuombea jambo jema moja jirani basi wewe utapata mara mbili, yaani kama ukiomba jirani awe na nyumba basi Mwenyezi Mungu atakupa nyumba mbili. kwa Mbwambo angeomba yeye atolewe jicho moja ili Jk akose macho mawili.masikini maombi huombwa kwenye mambo mema tu.
Napata ugumu kujua kama Raia mwema ni gazeti la Kina Ulimwengu au ni la Padri Slaa? maana Tanzania Daima inajulikana ni la Mbowe na hili ni la Slaa?
Naishia hapa kwa sasa.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Kwani kumwandika kwa namna ya kumkosoa ubovu wa JK ndio kukiuka maadili ya uandishi? Au bado uko katika zama zile za 'zidumu fikra za mwenyekiti wa ccm?' Tafakari

Kwani hakuna mazuri ya JK ni mabaya na ukosoaji tu au yeye amesomea ukosoaji peke yake? If that the case topic closed
 
Mjadala huu ulioanzishwa na TAFAKARI ni mzuri ingawa nina uhakika kuwa wengi kama inavyojionyesha hapa watapinga. Uzuri wa mjadala huu ni pale tunapoanza kujadili utendaji wa vyombo vya habari na waandishi wa habari wenyewe. Ukweli ni kuwa waandishi wa habari wana nafasi kubwa katika jamii yetu ambapo wanaweza kubomoa au kujenga nchi. Hii ni kutokana na nafasi yao katika jamii. Ndio maana waandishi wadogo tu kwa vyeo au hata umri utakuta wanaogopwa hivi sasa na mawaziri, wakuu wa mikoa wakuu wa mashirika na watu wengine mashuhuri kutokana na nguvu kubwa waliyonayo waandishi wa habari.

Kutokana na nguvu kubwa hii kw awaandishi wa habari baadhi hyao wameanza kuvimba vichwa wakidhani wao wako juu ya jamii. Waandishi wengi wana mbwembwe nyingi na kubwa za ajabu. Many of them are very arrogant leave alone the fact that they are also very (many of them) unethical in their profession.

Waandishi wa habari wengi ni wala rushwa wakubwa. Ukitaka kulijua hili andaa semina au warsha uone namna mwisho wa semina wanavyohangaikia kupata bahasha za khaki zikiwa na shilingi elfu kumi au 20 au 50 na kadhalika. Ukiwapa fedha kidogo utaipata. Watadai kwanini umewapa 'nauli' kidogo.

Juzi juzi kulikuwa na confrence moja inayomhusu mtu mmoja anayedaiwa ni mmoja wa mafisadi ambaye alikuwa ameitisha pamoja na mambo mengine ili ajisafishe. Tunaelezwa kila aliyekwenda kwenye press confrence hiyo alipewa sh. 100,000/- kama posho. lakini pamoja na hayo asubuhi yake magazeti yaliandika alichosema lakini hayakuandika kuhusu sh. 100,000/- zilizotolewa kwa kila mwandishi aliyehudhuria press confrence hiyo.

Jingine kiwango cha elimu kwa waandishi wengi ni cha chini mno. Yaani hata wale mnaodhani wamebobea ukiomba cv zao utaingia uvunguni mwa kitanda kwa aibu ukiziona. Ndiyo maana habari nyingi zinazoandikwa siyo za uchambuzi ila ni za juu juu tu huku zikiwa za majungu zaidi.

Kwa hiyo ndio maana uandishi wengi wa habari wa tanzania ni majungu majungu zaidi. N akwa kivuli cha uhuru wa vyombo vya habari wanaandika mambo ya ajabu kabisa.

Kwa ufupi uandishi wa habari wa tanzania ni wa kishabiki zaidi. Wale wanaomchukia JK jkwa mfano wataandika mabaya zaidi ya JK kuliko mazuri. Na wale wanaompenda JK wataandika mazuri zaidi kuliko mabaya. Kwa hiyo wale wa CHADEMA watapenda habari mbaya kuhusu JK na watamuona mwandishi aliyeandika habari hizo kuwa ni gwiji anayestahili kupata Noble prize.

Hata kwenye Simba na Yanga hivyo hivyo. Wako waandishi wa habari wa YANGA na wako Waandishi wa habar wa SIMBA. Kwa hiyo wale waandishi wa habari wa SIMBA wataandika mazuri ya SIMBA hata kama ni UONGO. Na wale wa YANGA watandika mazuri ya YANGA hata kama ni UONGO. Mbaya zaidi Waandishi wa pande zote mbili wanaweza kutumika kuandika mabaya ya SIMBA au YANGA wenyewe wanaita kubomoa.

Kwa hiyo jamii ya watanzania wanalishwa mambo ya ajabu kabisa. Ukitaka upate ukweli wa tukio lolote lile utapaswa mtu ununue magazeti tofauti zaidi ya15 kwa siku ili angalau uweze kutathimini ukweli wa habari. Habari peke yake ambayo ni ya ukweli kwenye gazeti lolote ni jina la gazeti na bei yake.

Sisi Watanzania tunayo kazi. haya sasa endeleeni na mjadala wenu.
 
habari ni habari hata kama hainifurahishi cha msingi ni kuzingatia maadili ya uandishi.na habarri yenyewe iwe na ukweli.
kuandika mabaya ya mtu si ukosefu wa maadili haswa kama hayo mabaya ni ya ukweli.
kikwete hastahili kusifiwa kwa mazuri hata kama ni mengikuliko mabaya bali anatakiwa kulaumiwa kwa yale mabaya,utaniuliza kwa nini? jibu ni rahisi alipokuja kuomba kazi ina maana alijua ataifamya kwa asilimia mia moja na mshahara sisi mabosi wake tunalipa kwa asilimia mia moja,marupurupu yote haki zake zote na kwa kifupi nikuambie wewe unayejiita tafakari ni kwamba huyu kikwete analipwa hela nyingi kuliko obama.
sasa kama nina mahali anapwaya lazima watu wapige kelele.siwezi kukupa kazi nikakulipa mshahara halafu ukikosea nikikulaumu uniite eti sina fadhila au shukrani. TAFAKARI KAMA MBONGO INA AKILI KAMA HAINA KITU BAKI NA HILO JINA KWANI SIO MBAYA.
 
Kwani hakuna mazuri ya JK ni mabaya na ukosoaji tu au yeye amesomea ukosoaji peke yake? If that the case topic closed

Tatizo la viongozi wa bongo mnapenda sana sifa hata zisizostahili. Kwani JK aliombwa na watanzania kuwa rais au yeye ndiyo aliyeomba kazi hiyo. Sasa unapoomba kazi maana yake unatakiwa kutimiza majukumu yako na chochote utakachofanya katika ofisi ya umma kama ni kizuri basi umetimiza wajibu wako kama ni kibaya lazima ukosolewe.
 
Napata ugumu kujua kama Raia mwema ni gazeti la Kina Ulimwengu au ni la Padri Slaa? maana Tanzania Daima inajulikana ni la Mbowe na hili ni la Slaa?
Naishia hapa kwa sasa (QUOTE).

RAIA MWEMA ni gazeti la akina Ulimwengu, Mbwambo na wengineo. Lakini kamwe SLAA hahusiki na gazeti hili ingawa ananufaika na sera ya gazeti hili. Mnajua sera ya gani hili ni nini? Sera yao andika mabaya yote ya serikali. UKiwauliza kwanini hawaandiki mazuri utaambiwa kuwa hawawezi kuandika mazuri kwa kuwa kazi ya serikali ni kufanya mazuri tu na siyo mabaya.

Kwa hiyo SLAA na CHADEMA wananufaika na RAIA MWEMA kutokana na sera ya gazeti hili.
 
Gazeti hili na hasa makala ya Johson Mbwambo ni za chuki za wazi kwa JK imekuwa ada kwa makala za Mbwambo kila wiki kumsema,kukejeli na kumkosoa vibaya JK.kwa muda mrefu sana hali hii inatia kinyaa na kumuona Mbwambo ni mtu asiyeaminika.Tukumbuke kuwa kabla ya kampeni za uchaguzi mtu huyu aliandika makala huku akisema kuwa Waandishi wazingatie maadili katika kipindi hiki.
Lakini mlolongo wa makala zake toka mwanzo wa kampeni umeanza kwenda kinyume na kile alichokiandika kabla ya kampeni.Umeanza kuonyesha kuwa Mbwambo amekuwa na agenda yake iliyojificha dhidi ya JK.Mara aseme kimfaacho Jk ni asasi na si urais huku akisahau kuwa ni Kikwete huyu huyu ambaye amekuwa madrakani kwa miaka mitano iliyopita huku Mbwambo akiwa kama mwananchi wake. Hili ameliandika katika makala yake ya jana 06/10/2010.Amefikia mahali akathubutu hata kuandika kuwa inafaa JK akajifunze kwa Rais Kagame wa Rwanda.Sina hakika kama alitaka JK akajifunza kutumia nchi za wengine kufadhili ghasia na kutumia nafasi hiyo kusaidia nchi yake au alimaanisha JK akajifunze jinsi ya kuwanyima wapinzani uhuru na kutishia vyombo vya habari,sijui hasa alimaanisha nini.Labda Watanzania wenzangu mtanisaidia.
Hivi Ukubwa wa Tanzania utaufananisha na Rwanda? kama kujifunza kwanini Kagame wa Rwanda asije kujifunza kwa JK KWENYE ujenzi wa Chuo kikuu cha kuigwa cha Dodoma?Mbwambo hivi Rwanda wana chuo kama UDOM? umeshindwa kumpa heko JK hata kwa jambo kama hilo?Au wewe ndo ulipanga shughuli hiyo?Maandishi ya MBWAMBO hayana tofauti na mwandishi anayetumia jina la bandia anayejiita MSOMAJI RAIA hawa ni kama mapacha na Mbwambo kuanzia mtiririko wa uandishi wao,mawazo hasi dhidi ya JK, chuki zao za wazi zisizo na sababu kwa JK .HUYU MSOMAJI RAIA kaanza kuandika toka mwaka jana kuwa Rais Jk hashauriki. Hiyo ilikuwa mwezi wa tisa 2009. mwaka huu kajisahau kaandika kuwa Rais Kikwete anasikiliza marafiki zake sana. sasa mtu ambaye hashauriki atasikiliza marafiki na watu wake wa karibu?Cha ajabu minal rahman Mbambo kawahi kuandika makala kumsifu waziri Mkuu Mizengo Pinda kama waziri makini na mtendaji ni swali je aliyemteua Pinda si ndio JK? kazi hizo zinazo mfurahisha Mbwambo ndizo za JK.anafanya kwa maelekezo ya JK. HII NI DOUBLE STANDARDS.MFANO gazeti la jumatano ya jana Mbwambo karudia habari ya World Economic Forums uliofanyika Dsm 5-7 Mei 2010.
huko nyuma aliwahi kuandika makala ya kukebehi mkutano ule kwa vile tu mgeni Rasmi alikuwa JK.imekuwa kama Mbwambo ana allergy na jina la JK.ameamua kuwa anarudia rudia maneno ya kumchafua JK.NAJIULIZA kama Mbwambo angepewa fursa ya kuambiwa ukimuombea jambo jema moja jirani basi wewe utapata mara mbili, yaani kama ukiomba jirani awe na nyumba basi Mwenyezi Mungu atakupa nyumba mbili. kwa Mbwambo angeomba yeye atolewe jicho moja ili Jk akose macho mawili.masikini maombi huombwa kwenye mambo mema tu.
Napata ugumu kujua kama Raia mwema ni gazeti la Kina Ulimwengu au ni la Padri Slaa? maana Tanzania Daima inajulikana ni la Mbowe na hili ni la Slaa?
Naishia hapa kwa sasa.

MUNGU IBARIKI TANZANIA

Wewe ni zuzu usiyejielewa, kama kweli unamuonea huruma JK kwa kukosolewa na Mbwambo kwa nini humuonei huruma kwa nafasi aliyoshika kuwa kubwa zaidi ya uwezo wake?
1. Ana maradhi yasiyoisha ndio maana kila anapokwenda ni lazima ambulance iwepo.
2. Anasahau kuwa yeye ni mkuu wa nchi na anafanya dhihaka hata kwa mambo makini yanayohusu hatma ya taifa.
3.Hajui chanzo cha umaskini wa tanzania japokuwa ina utajiri wa madini na maliasili nyingine.
4. Anaongelea udini kitu ambacho hakipo tanzania isipokuwa yeye na rafiki zake ndio wanalazimisha kiwepo.
 
Did you find this post helpful? |
icon1.png
Re: Ya Gazeti la Raiamwema na makala za Mbwambo;Tujadili hoja.

quote_icon.png
Originally Posted by nguvumali
ccm woote mmejaa mawazo mdebwedo
32255_121703247858782_112258888803218_222024_70321_s.jpg

He! ubunifu huu ni kiboko

Wengine hatuwezi kusoma maadishi yasiyo na paragraphs!
 
Siku zote ukweli unauma. Pole sana kaka. Shida ya Mbwambo ni msema ukweli sasa amesahau kuwa kuna watu wana allegy na ukweli.
 
Sihitajii kusema sana hapa. katika waandishi ambao nilikuwa nikiwaheshimu ni Mbwambo lakini nilishamtoa kwenye hesabu! Mwandishi akishakuwa hakimu, kuna haja gani tena ya kumsoma, anaandika yeye na kuhukumu yeye!! Hili ni pamoja na yule mwingine. AKA aliyekimbizwa Zanzibar lakini ndio mfumo wa waandishi habari wengi Tanzania :teeth:

ILA KILICHOJIFICHA NYUMA YAO HAKINA MUDA KITAJULIKANA............
 
Raia mwema,mwanahalisi,mwananchi na Tanzania Daima
haya ni magazeti ya ukweli kwa watanzania na daima yatapendwa!
sasa ww baki ukisoma uhuru,mtanzania nk. Hayo magazeti yako watu
hatuyapendi maana yanamtazamo mgando
 
....jamani time ya "kuchimba dawa" badoooo!! basi leteni valuu bariiiiidiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii nasikia kiu.................na mbuzi pia wa kuchoma...
 
Yote Yaliongewa Katika Gazeti ni Analysis ya Ukweli na Changamoto Kubwa Inchini. Hawa Wanainchi Wanaolalamika Kuhusu Journalism Roles za Tanzania Hawajui Kazi ya Vyombo vya Habari. Wanataka Kila Mtanzania Kumbeba JK na CCM Kila Leo. Hawajiulizi nini Kazi ya TBC, Daily News na Magazeti ya Serikali. Wanainchi Kama Hawa Wamezoea Kumpigia JK Makofi Kila Siku na Kufikiri Maendeleo Yataletwa na Upole na Ndugu Mweshimiwa. Aliepost Hii Article Anafanya Kazi Daily News? Pole Mtumishi Hatukaliani Swala Lako la Uandishi Tanzania...
 
Raia Mwema Toleo Na 1
Masikini Mzee Ali Hassan Mwinyi!

Masikini Mzee Ali Hassan Mwinyi!

Ncheme Nchicheme? Oktoba 31, 2007

TUNGEKUWA tumejaaliwa uungwana na Mwenyezi Mungu, nasi tukawa ni watu wa kukiri makosa yetu na kisha tukawa na moyo wa kutaka radhi wale tuliowakosea, basi Watanzania wengi tungekuwa tumekwisha kuunga ujumbe wa watu wasiopungua 500 kwenda kuanguka chini ya miguu ya Mzee Ali Hassan Mwinyi huku tukimwomba atusamehe kwa makosa makubwa tuliyomtendea.

Ujumbe huo ungepaswa uongozwe na wahariri na wasanifu wakuu wa tahariri katika magazeti ya miaka ya mwanzo ya 1990, kwa sababu sisi ndio hasa tulikuwa msitari wa mbele katika kutenda makosa hayo dhidi ya mzee huyo ambaye tulimbatiza jina la "Mzee Ruksa".

Kosa kubwa tulilotenda dhidi ya Rais huyo wa Awamu ya Pili ilikuwa ni kumhusisha na vitendo vya rushwa na ufisadi, hata kuwafanya wasomaji wa magazeti yaliyochapishwa wakati huo, waamini kwamba kilichokuwa kikifanyika Ikulu ulikuwa ni uharamia wa hali ya juu.

Sasa tunajua kwamba yote haya hayakuwa kweli. Haiwezekani kusema kwamba Mzee Mwinyi hakuwa na dosari, kwani kusema hivyo ni kumwondoa kwenye kundi la binadamu.

Alikuwa na dosari zake na udhaifu wake, na hayo bado anayo hadi leo, kwa ilivyokuwa wakati akiwa Ikulu. Lakini pia ni kweli kwamba sehemu ya udhaifu wake ilitokana na wema na upole wake katika mazingira ya "manyang'au" aliowaamini na ambao hawakusita kuutumia upole wake na jina lake kufanya walivyotaka kwa kumsingizia yeye.

Leo hii sote tunajua kwamba tulimwonea sana Mzee Mwinyi kwa kumbebesha mambo yasiyokuwa yake. Na wala si yeye peke yake aliyekumbwa na uonevu huo bali pia mkewe, Bi Sitti Mwinyi, ambaye naye alihusishwa na kila aina ya maovu kutokana na uvumi ulioenezwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Baadhi tutakumbuka pia kwamba Mzee Mwinyi aliwahi kulalamika hadharani kwamba uvumi ulikuwa umeenezwa kuhusu yeye kumwoa kigori mdogo kwa kumfanya aache shule… kila aina ya uvumu na uzushi. Mzee huyu muungwana alivumilia, akavuta subira, akasamehe. Haishangazi kwamba amebaki kuwa kipenzi cha Watanzania kutokana na upole, unyenyekevu na uadilifu wake.

Tunajua sasa kwamba, ingawaje vitendo vya ufisadi vilitendeka chini ya uongozi wake, yeye mwenyewe binafsi hakuhusika moja kwa moja.

Baada ya Mzee Mwinyi kuondoka madarakani ndipo nchi hii imepata bahati mbaya si tu ya kuendelea kuelemewa na vitendo vya ufisadi katika safu za uongozi, bali pia mkosi wa kuwa na ‘kiongozi' mkuu anayesimamia ufisadi huo kwa kushiriki yeye mwenyewe binafsi kuunda kampuni ya biashara na kuisajili rasmi kwa anwani ya ofisi ya umma, na hata kujihaulishia umiliki wa kampuni ya serikali na kuiandikisha kwa jina lake na familia yake na maswahiba zake.

Tumshukuru Mungu tunayo Katiba inayoweka mipaka ya mihula ya uongozi, la sivyo baada ya mihula mitano tungeikuta nchi imehamia bara jingine kwa jinsi tamaa za wakuu zilivyozidi na jinsi matumbo yao yalivyo na nafasi za kujaza.

Kisha tumshukuru Mzee Mwinyi kwa uungwana wake, na mwisho tumwombe radhi kwa jinsi tulivyomdhalilisha.

Sijui Ulimwengu anataka haya tena au historia imhukumu mara ya pili. Hiki kilikuwa kipindi cha yeye kufanya toba baada ya genge aliloliongoza kufanya walichokifanya dhidi ya Mzee Mwinyi kipindi kile wakiwa bado wapo Rai.
 
:drum:

Hauna jipya, na mwenyezi mungu akulaani kwa mitizamo yako hiyo ya kifisadi!!!!!!!!!, I mean ULAAAANIWE NA AIDHA UFUNGWE KABISA WEWE FISADIIIIIIIIIIIIIIIII!!!, watu sasa maslahi ya nchi yapo mbele si CHAMA wala GAZETI, Ni kiongozi aliye na mwelekeo wa kutuondoa hapa tulipo!
 
Dear GOD, may you listen to our prayers and help us win this election (Chadema). Dear GOD, We ask now to ignore our enemies prayers.. Amen.

And why should I listen to your prayers and ignore you enemies prayers?
 
Raia Mwema Toleo Na 1
Masikini Mzee Ali Hassan Mwinyi!

Masikini Mzee Ali Hassan Mwinyi!

Ncheme Nchicheme? Oktoba 31, 2007

TUNGEKUWA tumejaaliwa uungwana na Mwenyezi Mungu, nasi tukawa ni watu wa kukiri makosa yetu na kisha tukawa na moyo wa kutaka radhi wale tuliowakosea, basi Watanzania wengi tungekuwa tumekwisha kuunga ujumbe wa watu wasiopungua 500 kwenda kuanguka chini ya miguu ya Mzee Ali Hassan Mwinyi huku tukimwomba atusamehe kwa makosa makubwa tuliyomtendea.

Ujumbe huo ungepaswa uongozwe na wahariri na wasanifu wakuu wa tahariri katika magazeti ya miaka ya mwanzo ya 1990, kwa sababu sisi ndio hasa tulikuwa msitari wa mbele katika kutenda makosa hayo dhidi ya mzee huyo ambaye tulimbatiza jina la "Mzee Ruksa".

Kosa kubwa tulilotenda dhidi ya Rais huyo wa Awamu ya Pili ilikuwa ni kumhusisha na vitendo vya rushwa na ufisadi, hata kuwafanya wasomaji wa magazeti yaliyochapishwa wakati huo, waamini kwamba kilichokuwa kikifanyika Ikulu ulikuwa ni uharamia wa hali ya juu.

Sasa tunajua kwamba yote haya hayakuwa kweli. Haiwezekani kusema kwamba Mzee Mwinyi hakuwa na dosari, kwani kusema hivyo ni kumwondoa kwenye kundi la binadamu.

Alikuwa na dosari zake na udhaifu wake, na hayo bado anayo hadi leo, kwa ilivyokuwa wakati akiwa Ikulu. Lakini pia ni kweli kwamba sehemu ya udhaifu wake ilitokana na wema na upole wake katika mazingira ya "manyang'au" aliowaamini na ambao hawakusita kuutumia upole wake na jina lake kufanya walivyotaka kwa kumsingizia yeye.

Leo hii sote tunajua kwamba tulimwonea sana Mzee Mwinyi kwa kumbebesha mambo yasiyokuwa yake. Na wala si yeye peke yake aliyekumbwa na uonevu huo bali pia mkewe, Bi Sitti Mwinyi, ambaye naye alihusishwa na kila aina ya maovu kutokana na uvumi ulioenezwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Baadhi tutakumbuka pia kwamba Mzee Mwinyi aliwahi kulalamika hadharani kwamba uvumi ulikuwa umeenezwa kuhusu yeye kumwoa kigori mdogo kwa kumfanya aache shule… kila aina ya uvumu na uzushi. Mzee huyu muungwana alivumilia, akavuta subira, akasamehe. Haishangazi kwamba amebaki kuwa kipenzi cha Watanzania kutokana na upole, unyenyekevu na uadilifu wake.

Tunajua sasa kwamba, ingawaje vitendo vya ufisadi vilitendeka chini ya uongozi wake, yeye mwenyewe binafsi hakuhusika moja kwa moja.

Baada ya Mzee Mwinyi kuondoka madarakani ndipo nchi hii imepata bahati mbaya si tu ya kuendelea kuelemewa na vitendo vya ufisadi katika safu za uongozi, bali pia mkosi wa kuwa na ‘kiongozi' mkuu anayesimamia ufisadi huo kwa kushiriki yeye mwenyewe binafsi kuunda kampuni ya biashara na kuisajili rasmi kwa anwani ya ofisi ya umma, na hata kujihaulishia umiliki wa kampuni ya serikali na kuiandikisha kwa jina lake na familia yake na maswahiba zake.

Tumshukuru Mungu tunayo Katiba inayoweka mipaka ya mihula ya uongozi, la sivyo baada ya mihula mitano tungeikuta nchi imehamia bara jingine kwa jinsi tamaa za wakuu zilivyozidi na jinsi matumbo yao yalivyo na nafasi za kujaza.

Kisha tumshukuru Mzee Mwinyi kwa uungwana wake, na mwisho tumwombe radhi kwa jinsi tulivyomdhalilisha.

Sijui Ulimwengu anataka haya tena au historia imhukumu mara ya pili. Hiki kilikuwa kipindi cha yeye kufanya toba baada ya genge aliloliongoza kufanya walichokifanya dhidi ya Mzee Mwinyi kipindi kile wakiwa bado wapo Rai.

Na bado, atakuja some Pinda or suchlike nincompoop kuwa rais mtawaomba msamaha mpaka Mkapa na Kikwete.

Mark my words, this is a downhill trend.
 
Ndugu Tafakari nimesoma kwa makini makala yako nimesoma kila neno naona umejieleza vizuri bila shaka labda nikwambie watu wa aina ya Jonson Mbwambo ni wa aina gani, hawa ni watu wasio na shukrani kabisa.............kama unabisha nenda pale Mzumbe sekondari halafu uliza habari zake au tafuta file lake utaona alivyozoea kutukanatukana, kwanza huwa hawezi kujadili kwa hoja wala mantiki badala yake hujikita kwenye upande mmoja tu na kujadili kwa chuki labda niunge mkono wazo lako kwamba kama vile mtu anavyoweza kuwa na allergy na samaki basi na huyu Johnson Mbwambo ana allergy na Kikwete dawa ni kumpuuza kwa maana asiyejua maana haambiwi maana.

yaleyaleee ya kuwataka watanzania kupuuza.....kweli nyie ndo wapuuzi watupu..kama mmejiunga JF kuleta pumba zenu hapa mmechemsha:embarrassed::embarrassed::embarrassed:
 
Back
Top Bottom