Ya kale Dhahabu

Ya kale Dhahabu

Kati ya wachezaji waliocheza mpira kuanzia miaka ya 1985 kuendelea, wachezaji wafuatao ni ngumu sana kuwafananisha na mastaa wa sasa wa hapa kwetu;
Hamisi Gaga
Athumani China
Zamoyoni Mogella
Hussein Marsha
Saidi Mwamba
Edibily Lunyamila
Method Mogella
George Masatu

Hawa jamaa walijuwa wanaujua kweli.
 
View attachment 318684

NAOMBA KUWEKEWA PREFIX YA STICK KWA HUU UZI
Nahisi hii ilikuwa ni mechi ya timu ya Taifa
Wa kwanza kushoto sioni sura yake ila ni kama Hamisi Gaga Gagarino then Zamoyoni Mogella then Athuman China kama sikosei na wa mwisho Hussein Amaan Marsha...naamini ni timu ya Taifa kwani pamoja na Marsha kusajiliwa Yanga 1994 hakuwahi ichezea kabisa kwani yeye na Mohammed Mwameja walisajili Yanga na Simba huku Keneth Mkapa na Lunyamila wakisainibpia Simba, ikabidi Rais Mwinyi aingilie kati wabaki timu zao za zamani
 
Kati ya wachezaji waliocheza mpira kuanzia miaka ya 1985 kuendelea, wachezaji wafuatao ni ngumu sana kuwafananisha na mastaa wa sasa wa hapa kwetu;
Hamisi Gaga
Athumani China
Zamoyoni Mogella
Hussein Marsha
Saidi Mwamba
Edibily Lunyamila
Method Mogella
George Masatu

Hawa jamaa walijuwa wanaujua kweli.
John Makelele
mavumbi Omary
itutu kigi
hassan afif
 
The dream team ya 2001 chini ya Udhamini wa MO , NBC na Simba Cement, na kocha akiwa mtaalamu James Siang'a...acha kabisa nafikiri hapa ni kabla ya kuizaba 44KJ ya Mbeya 7-0 kapteni Mwameja, Pawassa, Shekhan Rashid Madaraka Suleiman mzee wa kiminyio , Matola na Magere Masatu wanaonekana hapo
 
Moja ya vikosi bora kabisa vya Simba sports Club, kama sikosei hii ni 1993 kabla ya moja ya mechi za Kombe la CAF
Mstari wa juu waliosimama kushoto ni Azim Dewji, Madaraka Suleiman??/( sina hakika) then Fikiri Magoso au Deo Mkuki, kisha Mwameja, Hussein Marsha, Mustapha Hozza na George Magere Masatu ambaye jezi yake anaonekana amebadilishana na Edward Chumila (RIP)
Mstari wa chini nimewasahau karibia wote labda wa mwisho kulia ambaye atakuwa ni marehemu Edward Chumila
 
Moja ya vikosi bora vya Young Africans Sports Club, kama sikosei hii ni 1993 maana baadhi ya wachezaji waliopo hapo walicheza mwaka huo.

mstari wa juu toka kushoto Stephen Nemes, David Mwakalebela, Zamoyoni Mogella ( mwaka ambao Mogella alichezea Yanga), kisha wawili mwishoni kulia ni Kenneth Mkapa na Charles Mgombelo Meneja wa timu
Mstari wa chini kushoto ni Edibily Lunyamila, na wawili wa mwisho kulia ni Marehemu Said Mamba Kizota na Marehemu Riffat Said
 
Back
Top Bottom