Ya Mdude Chadema yamenikumbusha kauli ya babu mmoja "Unamhurumia mtu, yeye mwenyewe amekwambia anajihurumia"?

Ya Mdude Chadema yamenikumbusha kauli ya babu mmoja "Unamhurumia mtu, yeye mwenyewe amekwambia anajihurumia"?

Mkaruka

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
19,629
Reaction score
34,199
Honestly, kila binadamu mwenye utu ukiona jambo baya na la uonevu linamtokea mtu hujisikii vizuri.

Huyu kada wa Chadema naweza kusema, yupo tu kwenye siasa ila hazijui vizuri.

Siasa za nchi hii, ukizifanya kwa mihemko huwezi kupiga hatua. Kwanza hao unaodhani uko nao kwenye mapambano wengi wanapambania kitu ambacho huenda hukijui. Yuko wapi Alphonce Mawazo ambaye alikosana na maRCs, DC, RPC, RCO katika siasa zake?

Familia yake imebaki yatima tu, huku Mbowe na familia yake ndio kwanza wananunua majumba na kufurahia maisha Dubai.

Anyway, kuna babu yangu mmoja ambaye yeye akikuona unamtetea sana mtu, unamhurumia kwa vile anavyofanyiwa amekuwa akitoa kauli hiyo.

Kwamba wewe unamhurumia na kumtetea, Je, yeye mwenyewe amekwambia anaumia, na anajihurumia ?

Tumemtetea sana Nusrat Hanje alipowekwa mahabusu, leo katolewa huko na yuko na hao hao waliomweka. Tena haongei chochote kuwa aliteseka huko mahabusu.

Nchi hii unaweza kujikuta unapata stress na kukonda kwa kumtetea mtu, wakati mtu mwenyewe unaedhani anateseka ndio kwanza ananenepa.
 
Huyo Hanje unataka aongee nini wakati sasa hivi yuko kule bungeni anahujumu uchumi wa Watanzania?

Halafu kosa la Mdude ni lipi? kusema atatumia wembe ule ule kumnyoa Samia kama ataendelea kuleta jeuri?

Ok, kama una akili timamu jiulize; Samia ana jeuri au hana? kama anavunja sheria za nchi wazi hiyo siyo jeuri ni nini, au ni kiburi?

Atanyolewa kwa wembe ule alionyolewa marehemu, simply atapingwa kama alivyopingwa mtangulizi wake, kosa liko wapi hapo?

Haya mambo msiwe mnayachukulia kwa mahaba mpaka mnapoteza uwezo wenu wa kuchambua mambo.

Nawashangaa mnakuwa wepesi kumlaumu Mdude anaekemea uovu kwa sababu tu ni mpinzani alietoka jela, ila mnakuwa wepesi kumlinda yule anaevunja sheria za nchi kwa kigezo cha "mama"

Muache hizi double standard zenu za kitoto tujenge nchi yetu kwenye misingi ya haki, utu, na utawala wa sheria.
 
Huyo Hanje unataka aongew nini wakati sasa hivi yuko bungeni anahujumu uchumi wa watanzania?
Hana la kuongea.

Shida ni sisi tuliotumia nguvu, muda na pesa kumhurumia na kumtetea tukidhani anaumia na kuteseka kumbe siyo kweli
 
Mdude ameahidi kumnyoa mama kwa wembe.

1625294619547.png
 
Yaan ndugu yangu umeongea kwa philosophy ya hali ya juu sana,ambayo wengi hawaioni.Binadamu ni wa ajabu sana.Mfano:Kuna ambao Magufuli aliwapa madaraka,aliwapigania na mpaka aliwapa majina ya vitu .Mfano ,soko la ndugai.Lakini alipokufa ,ndio hao walikuwa wa kwanza kumgeuka.

Ninakubaliana na usemi .Tenda wema usingoje shukrani. Lakini tuwe na kiasi na standard quality za kutenda wema.Maana binadamu hachelewi kukugeuka.
 
Halafu kosa la Mdude ni lipi? kusema atatumia wembe ule ule kumnyoa Samia kama ataendelea kuleta jeuri?

Atanyolewa kwa wembe ule alionyolewa marehemu, simply atapingwa kama alivyopingwa mtangulizi wake, kosa liko wapi hapo?
Mkuu, Haya siyo maneno yako,

Haya maneno ya Mdude, ni maneno ya mtu mmoja jasiri asiye tumia akili kuwasilisha,

Naungana na mleta hoja kwamba, Ujasiri wa vitu vya kijinga na kipumbavu kwa hapa bongo, ni kuyadharau maisha yako binafsi

Tunayo mifano mingi na kama ambavyo mleta hoja kagusia, na kwa bahati mbaya kabisa, hata hao ambao huwapa jeuri hiyo, mtu yakimtokea, wao hujificha nyuma ya mitandao kukoroma kusiko saidia chochote

Mf mdogo, Huyu Mdude katoka Jera si kwa sababu kashinda kesi, bali kwa sababu kuna mtu hayupo, na kwa sababu hiyo, embu jiulize, endapo huyo mtu ambaye hayupo angekuwepo, Ni nani angejitokeza kuwa mtetezi wa mdude hadharani kwamba, angeweza hata kuandamana ili tu mdude atoke??

akipata jibu la hiyo, nadhani anaweza kuanza kupuuza baadhi ya mihemko ya kisiasa, Tulikuwa na kina Beni saa8, ni nani ambaye alionyesha nia ya hata kuandamana kutaka ben apatikane?

Wooote walikuwa kimya cha mtungi, zaidi sana wamekoroma, ni mitandaoni,

Aache ngebe, atulizane atunze familia yake
 
Mkuu, Haya siyo maneno yako,

Haya maneno ya Mdude, ni maneno ya mtu mmoja jasiri asiye tumia akili kuwasilisha,

Naungana na mleta hoja kwamba, Ujasiri wa vitu vya kijinga na kipumbavu kwa hapa bongo, ni kuyadharau maisha yako binafsi

Tunayo mifano mingi na kama ambavyo mleta hoja kagusia, na kwa bahati mbaya kabisa, hata hao ambao hutoa jeuri hiyo, mtu yakimtokea, hujificha,

Mf mdogo, Huyu Mdude katoka Jera si kwa sababu kashinda kesi, bali kwa sababu kuna mtu hayupo, na kwa sababu hiyo, embu jiulize, endapo huyo mtu ambaye hatupo angekuwepo, Ni nani angejitokeza kuwa mtetezi wa mdude hadharani kwamba, angeweza hata kuandamana ili tu mdude atoke??

akipata jibu la hiyo, nadhani anaweza kuanza kupuuza baadhi ya migemko ya kisiasa, Tulikuwa na kina Beni saa8, ni nani ambaye aliontesha nia ya hata kuandamana?
Sasa hivi kina Ben Saanane utafikiri hawajawahi kuwepo nchi hii.

Chadema wenyewe hawana hata muda. Wako busy wanawaza uchaguzi tu.

Unajua wabongo wengi ni kelele tu, yakikukuta unabaki peke yako.

Wengine wanaendelea na maisha yao.
 
Unajua wabongo wengi ni kelele tu, yakikukuta unabaki peke yako.
Siasa si lazima zikutumikishe, Pana tofauti kubwa kati ya siasa zetu na za ulaya, America na Asian!

Kwetu sisi tunaujasiri wa midomoni ila sio vitendo, wenzetu wako na vyote,

Shauri yake mwacheni yamkute
 
Honestly, kila binadamu mwenye utu ukiona jambo baya na la uonevu linamtokea mtu hujisikii vizuri.

Huyu kada wa Chadema naweza kusema, yupo tu kwenye siasa ila hazijui vizuri.

Siasa za nchi hii, ukizifanya kwa mihemko huwezi kupiga hatua. Kwanza hao unaodhani uko nao kwenye mapambano wengi wanapambania kitu ambacho huenda hukijui. Yuko wapi Alphonce Mawazo ambaye alikosana na maRCs, DC, RPC, RCO katika siasa zake?

Familia yake imebaki yatima tu, huku Mbowe na familia yake ndio kwanza wananunua majumba na kufurahia maisha Dubai.

Anyway, kuna babu yangu mmoja ambaye yeye akikuona unamtetea sana mtu, unamhurumia kwa vile anavyofanyiwa amekuwa akitoa kauli hiyo.

Kwamba wewe unamhurumia na kumtetea, Je, yeye mwenyewe amekwambia anaumia, na anajihurumia ?

Tumemtetea sana Nusrat Hanje alipowekwa mahabusu, leo katolewa huko na yuko na hao hao waliomweka. Tena haongei chochote kuwa aliteseka huko mahabusu.

Nchi hii unaweza kujikuta unapata stress na kukonda kwa kumtetea mtu, wakati mtu mwenyewe unaedhani anateseka ndio kwanza ananenepa.
Kuna kisa flani nilipata kusikia huko upareni kwenye mashamba ya katani yaliyomilikiwa namgiriki.

Mgiriki alikuwa akiendesha pikipiki akaangusha begi la hela bila kujua. Mswahili mfanyakazi wake akaliona kulifungua akaona burunguti za noti za kutosha nakumkimbiza na makelele kumrudishia. Jamaa akasimama. Mswahili akampa begi akamuambia begi lalo hili na pesa zote zimo hata shilingi haijapotea.

Mgiriki alishikwa na ghazab akamgeukia akampa kwanza ngumi kali ya tumbo, nigger bado anashangaa kinachoendelea akapewa nyingine ya mgongo, wakati anatafakari mmatumbi akala buti kali la kalio. Akamsukumizia buti la mgongo kwenye korongo lililokuwa pembeni.

Akawasha pikipiki kabla ya kuondoka akamuambia jamaa ambaye alikuwa anagargara kwa maumivu makali utakufa maskini wewee nyambafu

Ncha Kali
 
Back
Top Bottom