Hivi karibuni tumeshuhudia mafuriko ya Nepal yanayofahamika kama flash floods yalivyosomba makazi ya watu na kusababisha uharibifu wa mali, majumba, miundo mbinu na zaidi hasa maisha ya watu wengi kupotea. Katikati ya majanga haya, kuna jengo moja lilibaki likisimama peke yake, likistahimili mikiki mikiki ya mafuriko hayo, na waliopo kwenye lile jengo kupona. Jengo lile liliacha msisimko mkubwa kwa kila aliyeweza kuona kilichotokea. Binafsi nilichukua video clip ya lile jengo na kuiweka status yangu ya whatsaap, na pia kwenye magroup kadhaa ya whatsaap.
Watu wengi wakacomment, "Mungu mkuu", "huu ni muujiza", "Ni mkono wa Mungu wa maajabu", na maneno mengine mengi ya aina hiyo. Nikajiuliza, mbona hakuna anayeuliza jengo hilo lilijengwaje? Sikatai mambo ya Mungu, mimi ni mkristo, namwamini Mungu, na sikatai, miujiza ipo. Ila kwa tukio lile nilikataa kuamini katika miujiza pekee. Nikajaribu kuingia mtandaoni kutafuta details kadhaa, bahati nzuri nikafanikiwa kupata nilichokuwa nakitafuta. Lile jengo lilijengwa kwa umahiri mkubwa, ukuta wake kwenye kona zote za nyumba, na kwenye lenta, na chini kwenye kiti palichimbwa sana chini wakasuka nondo na zege la uhakika.
Nikarudi kwenye biblia Mathayo 7: 24-27. Kisa alichotoa Yesu kuhusu watu wawili. Mmoja alijenga nyumba yake juu ya mwamba, na mwingine akajenga juu ya mchanga. Huyu wa pili upepo ulipovuma ukaipiga nyumba ikadondoka. Nikisoma kisa hiki nasimama kuwapinga wakristo wenzangu mnaoamini kwamba nyumba ile imesimama vile kwa sababu ya mkono wa Mungu. Sawa, sikatai Mungu ana sehemu, lakini ni upumbavu pia kushindwa kukubaliana kwamba mjenzi wa nyumba ile alitumia ustadi wa hali ya juu na gharama kubwa kustahimili madhara ambayo yangetokea. Unaweza kufuatilia haya maelezo hapa chini
View: https://www.youtube.com/shorts/MYC_DsITVP4

Ifike mahali tukubali makosa yetu sisi binadamu. Waafrika wengi tunamsingizia Mungu vitu ambavyo hata hahusiki. Hata tunaugua magonjwa yanayosababishwa na mfumo mbovu wa maisha au umaskini alafu tunasema mapenzi ya Mungu. Si sahihi. Mungu ninayemfahamu hana mpango na hajawahi kuwa na mpango kwamba mabaya yatupate. Mambo mengine ni uzembe wetu. Hatupo tayari kufanya kazi kwa bidii tutafute pesa, tunashinda makanisani tukisubiri kupokea miujiza alafu tunakufa kizembe tunasema ni mapenzi ya Mungu.
View: https://www.youtube.com/shorts/z5pOCVRVmZQ