Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Wafuatiliaji wa vita watakumbuka kule Ukraine siku jeshi la Zelensky lilipotangaza kifo cha kamanda wa jeshi la wanamaji wa Urusi,general SOKOLOV halafu siku ya tatu yake akaonekana yuko hai kwenye kikao akifuatilia mada ya mkutanoni.Kwa butwaa Ukraine ikasema ilikuwa ni picha yake kutoka chumba cha maiti kwa vile alikuwa haongei.
Kuna kamanda mwengine wa ngazi za juu wa Hamas ambaye kwa mbwembwe kubwa jeshi la Israel lilitangaza limemuua katika vita vya mwaka 2014 .Kamanda huyo ni Mohammed Sinwar ambaye ni ndugu wa kiongozi wa Hamas wa sasa huko Gaza,Yahya Sinwar.
Katika tangazo lake mwaka huo jeshi la Israel lilimuonesha Mohammed Sinwar akiwa maiti katikati ya dimbwi la damu na kutangaza ubora wa silaha zao usiokosea shabaha.
Kilichofuatia ni kuondoka kwenye fikra za watu kuhusu kamanda huyo ambaye katika vita vya mwaka 2011 alifanikisha pakubwa kuachiliwa kwa wafungwa 1000 nzima wa kipalestina kubadilishana na askari wa Israel,Gilad Shalit aliyekuwa akishikiliwa mateka.
Miongoni mwa wafungwa waliokuwa juu katika orodha ya mateka hao 1000 wa kipalestina ni Yahya Sinwar ambaye ndiye kiongozi wa sasa wa Hamas.
Baada ya tangazo hilo Mohammed alipotea machoni mwa wapalestina na hata miongoni mwa wanafamilia wake akiwa amejichimbia kwenye kazi zake za kiofisi
Miaka 10 mbele na kwa mshangao mkubwa baada ya shambulio la oktoba 7 jeshi la Israel limegundua kuwa Mohammed Sinwar bado yupo hai na kitengo chake cha kazi ni kile kile cha kuteka na kushikilia mateka katika vita pamoja na kutunza orodha za wafungwa wa kipalestina wanaotakiwa kubadilishana na mateka hao kutoka Israel
Hii kwa mara nyengine inadhihirisha kuwa jeshi la Israel na kitengo chake cha intelijensia cha Shinbet hawana uwezo wa Mungu wa kujua kila kitu kinachotokea miongoni mwao na jirani zake kama ambavyo wamekuwa wakisifiwa.Na kwamba wapalestina wamepata mbinu za kupambana nao.
Ushahidi mwengine ni kudukuliwa kwa mfumo wote wa ulinzi wa Israel mnamo tarehe 7 Oktoba na kufanikiwa kwa shambulio wenyewe waliloliita la kushtukiza kutoka kwa Hamas.