Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Kwa wale tuliozoea na kupenda sana nyama choma, iwe ni ya kuku, mbuzi, ng'ombe au nyama aina nyingine, habari mbaya zinazoenea kwa kasi katika ulimwengu wa vyakula ni kwamba wanasayansi wanasema wamethibitisha kwamba uchomaji nyama unasababisha kansa ya ngozi, ini, tumbo na nyinginezo kutokana na kemikali zijulikanazo kama polycyclic aromatic hydrocarbons, moto uunguzapo nyama.
Wanasayansi wanasema huu ukweli umejulikana toka miaka ya 1960, na kwamba inatia ndani nyama za kukaushwa kwa moshi, kama vile samaki, nk.
Habari yenyewe ndiyo hiyo. Iliyobaki ni kuchagua kusuka au kunyoa.
Source:
http://www.slate.com/articles/healt...t_time_to_give_up_smoked_and_fried_foods.html