Yadhihirika: Nyama choma inasababisha kansa

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
140122_MEDEX_GrilledPork.jpg.CROP.promo-mediumlarge.jpg

Kwa wale tuliozoea na kupenda sana nyama choma, iwe ni ya kuku, mbuzi, ng'ombe au nyama aina nyingine, habari mbaya zinazoenea kwa kasi katika ulimwengu wa vyakula ni kwamba wanasayansi wanasema wamethibitisha kwamba uchomaji nyama unasababisha kansa ya ngozi, ini, tumbo na nyinginezo kutokana na kemikali zijulikanazo kama polycyclic aromatic hydrocarbons, moto uunguzapo nyama.

Wanasayansi wanasema huu ukweli umejulikana toka miaka ya 1960, na kwamba inatia ndani nyama za kukaushwa kwa moshi, kama vile samaki, nk.

Habari yenyewe ndiyo hiyo. Iliyobaki ni kuchagua kusuka au kunyoa.

Source:
http://www.slate.com/articles/healt...t_time_to_give_up_smoked_and_fried_foods.html
 
Wamaasai na wamang'ati wamefanyiwa Research hii? Jamii kubwa ya wafugaji hula nyama choma karne na karne
 
Sasa sijui tule nini, maana kila kitu ni sumu.
 
Kufa ni kufa tu......mxiiiiu zao.....
 
Wamaasai na wamang'ati wamefanyiwa Research hii? Jamii kubwa ya wafugaji hula nyama choma karne na karne

Mkuu, unajua kisababishi kikubwa cha vifo vya Wamasai, ni uzee? Huwezi kujua, labda ni kansa.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Wamaasai na wamang'ati wamefanyiwa Research hii? Jamii kubwa ya wafugaji hula nyama choma karne na karne
Kama huo utafiti ni wa kweli basi kusingekuwa na wazee wa Kimasai na Kimang'ati.
 
Hawa wazungu bwana wakitaka kuporomosha bei ya kahawa wanasema inaleta maradhi ya moyo, wakitaka bei ipande wanasema coffee is good for your health, wakikaa juani masaa machache wao wanapata cancer sisi tunadunda tu. Nyama wenyewe (wazungu) huwa wanaunguza juu juu tu wanaona raha kuona damu ndani
 
......mpaka watapogundua kwanini kifo hakiepukiki ndio nitawaamini hawa wanasayansi, otherwise....

Hata usipokula nyama choma, utakufa kwa #Malaria !
 
Hivi mbona hawa watafiti wamekomalia nyama tu?

Juzi tu wamedai mdudu anavimelea(tegu) visababishavyo kifafa.

Wanataka wote tuwe ma-vegetarians?
 
Kwa wale tuliozoea na kupenda sana nyama choma, iwe ni ya kuku, mbuzi, ng'ombe au nyama aina nyingine, habari mbaya zinazoenea kwa kasi katika ulimwengu wa vyakula ni kwamba wanasayansi wanasema wamethibitisha kwamba uchomaji nyama unasababisha kansa ya ngozi, ini, tumbo na nyinginezo kutokana na kemikali zijulikanazo kama polycyclic aromatic hydrocarbons, moto uunguzapo nyama.

Wanasayansi wanasema huu ukweli umejulikana toka miaka ya 1960, na kwamba inatia ndani nyama za kukaushwa kwa moshi, kama vile samaki, nk.

Habari yenyewe ndiyo hiyo. Iliyobaki ni kuchagua kusuka au kunyoa.

Source:
Cancer risk from grilled meat: Is it time to give up smoked and fried foods?

Duh, nyama imeanza kuchomwa toka enzi za "mashimo/machimbo ya mfalme Suleiman"...na mijamaa ilikuwa na nguvu kama Simba! Acha tufe tu...
 
Ukichunguza zaid utagundua haohao ndo wanaongoza mahudhurio ya BBQ party
 
Hivi huwa najiuliza kama hivi vyakula vina madhara kwa nini mungu alitupa? Nyama majanga , mchele matunda mengine nayo majanga sasa tule nini.
 
140122_MEDEX_GrilledPork.jpg.CROP.promo-mediumlarge.jpg

Kwa wale tuliozoea na kupenda sana nyama choma, iwe ni ya kuku, mbuzi, ng'ombe au nyama aina nyingine, habari mbaya zinazoenea kwa kasi katika ulimwengu wa vyakula ni kwamba wanasayansi wanasema wamethibitisha kwamba uchomaji nyama unasababisha kansa ya ngozi, ini, tumbo na nyinginezo kutokana na kemikali zijulikanazo kama polycyclic aromatic hydrocarbons, moto uunguzapo nyama.

Wanasayansi wanasema huu ukweli umejulikana toka miaka ya 1960, na kwamba inatia ndani nyama za kukaushwa kwa moshi, kama vile samaki, nk.

Habari yenyewe ndiyo hiyo. Iliyobaki ni kuchagua kusuka au kunyoa.

Source:
Cancer risk from grilled meat: Is it time to give up smoked and fried foods?
Hata usipokula kitu utakufa kwa njaaa
 
Back
Top Bottom