Smt016
JF-Expert Member
- Jan 11, 2016
- 3,012
- 4,300
Hapo awali nilileta uzi humu kuwa Yanga wanashindwa kufanya vizuri kwasababu wanakosa vinasaba vya michuano ya kimataifa. Nilipondwa sana na wana Yanga wenzangu lakini mpaka sasa akili zinawakaa sawa baada ya kuona Simba kwake kufuzu klabu bingwa imekuwa kama jambo la kawaida hata akiwa na kikosi cha kuunga unga.
Michuano ya kimataifa unapaswa uwe na mikakati pamoja na mipango ya kutosha kuanzia ndani mpaka nje ya uwanja. Lakini viongozi wa Yanga hakuna mwenye huo uzoefu wa kujua ni nini kinapaswa kifanyike na kwa wakati gani.
Kilichopo kwasasa ni kuiga tu kwa Simba kwa vile vitendo vilivyokuwa wazi lakini wanashindwa kukaa nao chini kuomba siri za vita ili na wao watoboe kama wenzao. Hili linawashinda kwasababu walishaleta ujuaji katika jambo wasilolijua.
Goli alilofunga Mayele ambalo lilikatiwa kuwa ni offside, lilipaswa kuwa ni goli. Kama likitokea goli kama lile limefungwa na Al Hilal huko Sudan basi hilo litahesabika kuwa goli halali kama japokuwa ni kweli ni offside.
Mambo haya kwenye mpira wa Africa yapo. Kule Africa kusini kulikuwa na VAR lakini Simba walilia na kusaga meno kwa maamuzi yaliyotokea. Hapa nawakumbusha viongozi wa Yanga muamke, mjifunze ni nini mnapaswa kufanya mnapocheza mchezo wa kimataifa.
Tuje kwenye mada yangu juu ya mechi ya kesho. Hii mechi imegawanyika katika makundi mawili ya utimamu
1) utimamu katika upande wa saikolojia ya wachezaji, benchi la ufundi na viongozi.
Wakienda kwa mawazo ya hujuma hujuma itawafanya watoke katika morali ya mchezo. Viongozi, wachezaji na benchi la ufundi wanatakiwa waonane na mtalamu wa saikolojia ili wajengwe kifikra na kiakili ili waiendee mechi kwa utulivu mkubwa sana bila kupaniki. Hiki kipengele ni kipengele muhimu mno kwa wachezaji na benchi la ufundi na ndiyo itakayotengeneza hali za wachezaji.
2) Mbinu na ufundi
Nabi akubali tu kuwa timu yake ya msimu huu imekuwa timu inayoruhusu magoli kirahisi mno na hii inatokana na sababu ya safu mbovu ya ulinzi. Jambo la kwanza upande wa kipa mpange Mshery badala ya Diarra. Pamoja na uokozi wake za mmoja dhidi ya mmoja lakini mara nyingi namuona kama hayupo mchezoni, una cross za kucheza hazichezi na ushapu hana. Tena ni kama vile mechi ya fainali ya Azam Confederation imefungua kufuli zake zote za uimara. Na pengine hana tena bahati kwasasa, Mshery achukue nafasi yake kwa mechi ya kesho.
Mpira wa sasa kucheza bila ya kiungo mkabaji halisia ni kuwachosha mabeki. Bangala arudishwe kwenye nafasi ya kiungo kwasababu Aucho sio mkabaji.
Mechi ya awali kocha alifanya kosa kubwa sana kiufundi kwa kutompanga Bangala kwenye kiungo mkabaji, na pia kumaliza silaha zako kwa pamoja na hakuna wa kubadilisha mchezo. Hivyo mechi ya kesho unapaswa kuwa vyema kwanza kwenye kiungo cha ukabaji, ili timu iweze kutulia hasa mabeki.
Mechi ya kesho Yanga wanahitaji utulivu wa akili, upangaji bora wa timu, na kutumia kila nafasi. Michuano ya kimataifa haitaji upate tano ili upate goli moja, bali kila nafasi unaipata kwako inatakiwa uitendee haki.
Mwisho namalizia kwa kusema kuwa Mayele anapaswa kuacha uroho na uchoyo wa kutaka kuzungumziwa yeye tu kwa kufunga bali anapokuwa eneo la goli ampe mchezaji mwenzio aliyepo katika eneo zuri zaidi la kukwasha mpira nyavuni.