Yahusu serikali tatu

Yahusu serikali tatu

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Posts
608
Reaction score
1,655
Naomba leo tujadili kitu muhimu sana kwa Taifa letu; muungano wetu watanganyika na zanzibar. Muungano huu umekuwa chachu ya mijadala katika kipindi hiki ambacho taifa letu limeingia katika mchakato wa kuandika katiba mpya nami naamua kutafakuri kuhusu jambo hili. Mwanzo kabla ya yote kabla hatujaingia ndani kabisa ya mjadala huu ni lazima tujiulize je ni nini lilikuwa lengo la kuunganisha nchi hizi mbili?

Kila muungano una malengo yake ambayo nchi ambazo zimeungana zinataka kuyafikia. Kwahiyo kiini cha muungano wowote ni zile fikra za kwanza zilizouunda.

Nitameng'enyua kanini nchi zinaungana kwa sababu zifuatazo ;

1. Watu huungana kuongeza nguvu au mamlaka

2. Watu huungana kwasababu tu watu wa mataifa yao wana mila na nasaba zinazofanana hivyo huungana kutokana na sababu za undugu wao.

Katika sababu hizi mbili naamini taifa letu liliungana na zanzibar kwa sababu hii ya pili na sio ya kwanza na hiko ndio kiini cha muungano wetu na sio kuongeza nguvu na mamlaka. Sababu ya kwanza inauliwa pia na udogo wa zanzibar.

Kwenye sababu ya kwanza nchi zozote zenye ukubwa na wingi wa unakaribiana kulingana wanaweza kuungana ili kuongeza nguvu na influence katika dunia, kila nchi hutoa baadhi ya mamlaka yake kwa serikali ya shirikisho na serikali ya shirikisho ndiyo itakayoshika damira na dira ya pamoja ya mataifa hayo kujiendeleza na kuinukia katika uso wa dunia.

Kwahiyo katika muungao wetu ni dhahiri ya kwamba ni muungano wenye dhamira ya kuunganisha watu tu na sio kuunganisha nguvu za mataifa haya mawili ni muungano wenye malengo ya kiundugu. Sio muungano wa kulifanya taifa hili liwe lenye nguvu. Kwa udogo wa Zanzibar sababu ya kwanza isingewezekana.

Baada ya kujua hili embu turudi katika mifumo ambayo inajadiliwa sana katika mchakato huu wa katiba tuanze na mfumo wa serikali tatu. Kuna sheria asilia katika nature ambayo ina balance nature. Hii inaitwa law of equilibrium. Naelezea sheria hii kuelezea mfumo wa serikali tatu jinsi gani ulivyo mgumu katika nature kila kitu kiko balanced that is how nature works. Hatuwezi kupefusha uzani huu pasipo muungano kuvunjika na kuna hatari kubwa kama muungano ukivunjika majaliwa ya tanganyika yatakuwa hatarini pia.

Tuna nchi mbili hapa Tuna tanganyika na zanzibar. Zenye ukubwa na uwiano wa watu unao tofautiana. Tanganyika ina watu millioni Arobaini na kitu wakati Zanzibar ina watu millioni moja tu na tunataka kutengeneza muungano wa serikali tatu. Hii ina maana ya kuwa taifa hili ligawanywe katika Mamlaka tatu; Yaani mamlaka ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mamlaka ya Tanganyika na Mamlaka ya Zanzibar kwa kawaida katika miungano ya namna hii kila taifa hutoa baadhi ya mamlaka yake kwa serikali ya shirikisho. Swali la kujiuliza Tanganyika itatoa mamlaka yake kiasi gani bila kukinzana na mamlaka ya serikali ya shirikisho ukizingatia udogo wa zanzibar? Equalization of power itakuwa wapi hapa? Ili kuwe na balance ni lazima serikali ya shirikisho iwe na mamlaka sawa kutoka kila upande ili kuwe na balance of power. Ni muhimu kutambua kwamba serikali hizi mbili ya Shirikisho na ya Tanganyika lazima zita collide tu. Na ziki collide sidhani kama tanganyika itabaki salama hakuna msalia mtume hapa. Msijaribu mifumo ambayo hamna uhakika nayo. Nasema tena udogo wa zanzibar unazuia uwezekano wa taifa hili kuwa shirikisho.

Mimi binafsi siruhusu zanzibar itoke mikononi mwa tanganyika ni bora itumike nguvu kuwazima wote ambao wana hatarisha amani ya nchi ni afadhali nguvu itumike kuwazima watu wachache kuliko madhara makubwa yatakayoikumba taifa hili sababu ya ujinga wa wehu wachache. Demokrasia ina mipaka yake inapofikia hatua ya kutaka kuua kiini cha nchi hiyo siyo demokrasia ni upuuzi. Hili Taifa lazima lisimame na zanzibar ni sehemu ya Tanzania mpaka kufa. Ile michanga iliyochanganywa haiwezi kugawanyika milele.
 
Shayu:

Kwa Tanzania serikali tatu, nne, tano, sita au zaidi ya hizo inawezekana. Hivyo tatizo si idadi ya serikali, ukubwa wa Tanganyika au udogo wa Zanzibar. Tatizo lililopo ni wenye mamlaka ya utawala kupenda kujilundikia madaraka huku wakiwa hawana uwezo wa kutumia madaraka hayo kutatua matatizo ya wananchi, hawaheshimu miongozo ya nchi, au kujua mipaka ya utawala wao.

Kwa mfano inakuaje Katibu mkuu wa CCM anakagua miradi ya ujenzi ambayo ipo chini ya serikali?
 
Naomba leo tujadili kitu muhimu sana kwa Taifa letu; muungano wetu watanganyika na zanzibar. Muungano huu umekuwa chachu ya mijadala katika kipindi hiki ambacho taifa letu limeingia katika mchakato wa kuandika katiba mpya nami naamua kutafakuri kuhusu jambo hili. Mwanzo kabla ya yote kabla hatujaingia ndani kabisa ya mjadala huu ni lazima tujiulize je ni nini lilikuwa lengo la kuunganisha nchi hizi mbili?

Kila muungano una malengo yake ambayo nchi ambazo zimeungana zinataka kuyafikia. Kwahiyo kiini cha muungano wowote ni zile fikra za kwanza zilizouunda.

Nitameng'enyua kanini nchi zinaungana kwa sababu zifuatazo ;

1. Watu huungana kuongeza nguvu au mamlaka

2. Watu huungana kwasababu tu watu wa mataifa yao wana mila na nasaba zinazofanana hivyo huungana kutokana na sababu za undugu wao.

Katika sababu hizi mbili naamini taifa letu liliungana na zanzibar kwa sababu hii ya pili na sio ya kwanza na hiko ndio kiini cha muungano wetu na sio kuongeza nguvu na mamlaka. Sababu ya kwanza inauliwa pia na udogo wa zanzibar.

Kwenye sababu ya kwanza nchi zozote zenye ukubwa na wingi wa unakaribiana kulingana wanaweza kuungana ili kuongeza nguvu na influence katika dunia, kila nchi hutoa baadhi ya mamlaka yake kwa serikali ya shirikisho na serikali ya shirikisho ndiyo itakayoshika damira na dira ya pamoja ya mataifa hayo kujiendeleza na kuinukia katika uso wa dunia.

Kwahiyo katika muungao wetu ni dhahiri ya kwamba ni muungano wenye dhamira ya kuunganisha watu tu na sio kuunganisha nguvu za mataifa haya mawili ni muungano wenye malengo ya kiundugu. Sio muungano wa kulifanya taifa hili liwe lenye nguvu. Kwa udogo wa Zanzibar sababu ya kwanza isingewezekana.

Baada ya kujua hili embu turudi katika mifumo ambayo inajadiliwa sana katika mchakato huu wa katiba tuanze na mfumo wa serikali tatu. Kuna sheria asilia katika nature ambayo ina balance nature. Hii inaitwa law of equilibrium. Naelezea sheria hii kuelezea mfumo wa serikali tatu jinsi gani ulivyo mgumu katika nature kila kitu kiko balanced that is how nature works. Hatuwezi kupefusha uzani huu pasipo muungano kuvunjika na kuna hatari kubwa kama muungano ukivunjika majaliwa ya tanganyika yatakuwa hatarini pia.

Tuna nchi mbili hapa Tuna tanganyika na zanzibar. Zenye ukubwa na uwiano wa watu unao tofautiana. Tanganyika ina watu millioni Arobaini na kitu wakati Zanzibar ina watu millioni moja tu na tunataka kutengeneza muungano wa serikali tatu. Hii ina maana ya kuwa taifa hili ligawanywe katika Mamlaka tatu; Yaani mamlaka ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mamlaka ya Tanganyika na Mamlaka ya Zanzibar kwa kawaida katika miungano ya namna hii kila taifa hutoa baadhi ya mamlaka yake kwa serikali ya shirikisho. Swali la kujiuliza Tanganyika itatoa mamlaka yake kiasi gani bila kukinzana na mamlaka ya serikali ya shirikisho ukizingatia udogo wa zanzibar? Equalization of power itakuwa wapi hapa? Ili kuwe na balance ni lazima serikali ya shirikisho iwe na mamlaka sawa kutoka kila upande ili kuwe na balance of power. Ni muhimu kutambua kwamba serikali hizi mbili ya Shirikisho na ya Tanganyika lazima zita collide tu. Na ziki collide sidhani kama tanganyika itabaki salama hakuna msalia mtume hapa. Msijaribu mifumo ambayo hamna uhakika nayo. Nasema tena udogo wa zanzibar unazuia uwezekano wa taifa hili kuwa shirikisho.

Mimi binafsi siruhusu zanzibar itoke mikononi mwa tanganyika ni bora itumike nguvu kuwazima wote ambao wana hatarisha amani ya nchi ni afadhali nguvu itumike kuwazima watu wachache kuliko madhara makubwa yatakayoikumba taifa hili sababu ya ujinga wa wehu wachache. Demokrasia ina mipaka yake inapofikia hatua ya kutaka kuua kiini cha nchi hiyo siyo demokrasia ni upuuzi. Hili Taifa lazima lisimame na zanzibar ni sehemu ya Tanzania mpaka kufa. Ile michanga iliyochanganywa haiwezi kugawanyika milele.
Umeongea maneno mazito lakini pia yenye walakini kwa mtazamo wangu.

1. Hujapendekeza mfumo gani unafaa na kwasababu zipi
2. Kutofautiana kimawazo na kimtazamo ni wehu au wendawazimu?
3. Watu wasijaribu mfumo wasiouzoea, huu muungano wa sasa ulianza ukiwa na mazoea gani?
4. Kwanini unadhani ni vema nguvu itumike kuwazima wznz wanaotaka nchi yao?
5. Umesema udhaifu wa uongozi ndio uliosababisha kukiuka kwa katiba, halafu unadai hili ni taifa moja
a) Taifa moja lenye taifa jingine linawezekanaje
b) wznz hawataki muungano, utawezaje kuwa na taifa lenye manun'uniko ukastawi?
c) nini madhara kwa Tanganyika muungano ukivunjika?
 
Nikianza kujadili na wewe sidhani kama kutakuwa na muafaka ..tutaishia kwenye mjadala usiokuwa na mwisho. Na hii haitakuwa ni kitu chenye manufaa kwa pande zote mbili napenda mijadala ambayo itakuwa na mwisho, ambayo ukweli utapatikana baada ya logical analysis na kila mtu akakubali.
 
Hukuwa na sababu ya kuanzisha thread kama huwezi kujibu maswali ya Nguruvi3.
 
Last edited by a moderator:
Nikianza kujadili na wewe sidhani kama kutakuwa na muafaka ..
Shayu, ungependa uanze kujadili na mtu wa namna gani? Nafikiri ungetusaidia sana kama ungetoa tahadhari kutoka mwanzo ni wachangiaji wa aina gani unadhani uwezekano wa kupata muafaka upo.
tutaishia kwenye mjadala usiokuwa na mwisho.
Kwa nini mjadala usiwe na mwisho? Kwamba haupo tayari kukiri kushindwa? Labda utusaidie tuweze kujua lengo lako hasa la kuanzisha mada!
Na hii haitakuwa ni kitu chenye manufaa kwa pande zote mbili napenda mijadala ambayo itakuwa na mwisho,
Pande hizo mbili unazoongelea ni zipi? Nauliza kwa sababu mpaka hapa sijaweza kujua uko upande gani na hao wengine unaotaka kujadiliana nao umewaweka upande gani? umejuaje kuwa hawako upande wako?
ambayo ukweli utapatikana baada ya logical analysis na kila mtu akakubali.
Sawa, logical analysis! ni ipi hiyo au tusubiri bado iko njiani inakuja? Si heri ungetuasa tusichangie kwanza tusubiri uweke mlo mezani ndio tusogee? Hapa JF, amini usiamini, tuna subra ya ajabu.
 
Shayu amependekeza zitumike nguvu kwa wanaodai kusikilizwa, kwa sababau unayaamini mawazo yko. lakini hiyo haita kuwa haki. unapotaka nguvu zitumike unaonyesha kulazimisha kisichotakiwa. Harith Ghassany kwenye kitabu kwaheri ukoloni kwa heri uhuru, ameandika mahojiano ya wazee, baadhi yao wamesema Zanzibar ni koloni la Tanganyika. hii sntensi naikubai kwa sababu
1. wazanzibar hawakuwa tayari kwa muungano ukisoma hicho kitabu
2. hata sasa tunatumia nguvu kama nyerere alivotumia nguvu na ujanja kuziunganisha.
mimi ni mbara lakini naona kweli hatutendi haki katika hili
 
Last edited by a moderator:
Swali la kujiuliza Tanganyika itatoa mamlaka yake kiasi gani bila kukinzana na mamlaka ya serikali ya shirikisho ukizingatia udogo wa zanzibar? Equalization of power itakuwa wapi hapa? Ili kuwe na balance ni lazima serikali ya shirikisho iwe na mamlaka sawa kutoka kila upande ili kuwe na balance of power . Ni muhimu kutambua kwamba serikali hizi mbili ya Shirikisho na ya Tanganyika lazima zita collide tu. Na ziki collide sidhani kama tanganyika itabaki salama hakuna msalia mtume hapa. Msijaribu mifumo ambayo hamna uhakika nayo. Nasema tena udogo wa zanzibar unazuia uwezekano wa taifa hili kuwa shirikisho.
Kwenye "ground" hakuna vitu kama hivyo, hivyo vinabakia huko huko kwenye vitabu badala yake muungano wowote ule katika nadharia unatakiwa uwe wa ki-justice!

Anayestahiki kutoa 10 atoe kumi, anayestahiki kutoa 100 atoe mia na kwenye kupokea ndiyo iwe hivyo hivyo, halafu hii justice inafuatana na compromise; mimi nakubali kuacha hiki yule naye anakubali kuacha kile hapo ndiyo kutakuwa na muungano.

Kwa makusudi au bahati mbaya vitu vyote viwili hivyo hatuvioni katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Walioziunganishi hizi nchi nao walitakiwa walione hili ila tatizo ni mentality "za Kiafrika" ah huko mbele mambo yatakaa sawa tu.
 
Back
Top Bottom