Yahya Sinwar: Huyu Ndiye Kiongozi Mpya wa Hamas

Yahya Sinwar: Huyu Ndiye Kiongozi Mpya wa Hamas

Huihui2

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
7,021
Reaction score
11,475
MODS: Mumeharibu uzi wangu kwa kuchanganya na habari za uwongo. Narudia ku-post upya. Tafadhali uacheni.

Yahya Sinwar ameteuliwa kuwa Kiongozi Mkuu wa Hamas kumrithi Ismail Haniyeh aliyeuliwa majuzi akiwa Iran na mazishi yake yalifanyika Qatar.

Yahya Sinwar ndiye aliyepanga na kuratibu mauaji ya October 7, 2023 huko Israel Kusini, na kusababisha vita ambavyo mpaka sasa Wapalestina zaidi ya 38,000 kufariki na Wayahudi wapatao 1,200 kuuliwa. Bila kusahau Watanzania 2 pia wamekufa kwenye mgogoro huo

Screenshot_20240807_011632_Chrome.jpg
 
Hamas imemteua YAHYA SINWAR, kiongozi wa kundi la HAMAS linaloungwa mkono na Iran huko Gaza, kuwa Mkuu wake mpya wa Ofisi ya Kisiasa kufuatia mauaji ya mtangulizi wake Ismail Haniyeh wiki iliyopita mjini Tehran.

YAHYA SINWAR alikaa miaka 22 katika magereza ya Israel. Akiwa gerezani alifahamu vyema lugha ya KIEBRANIA, na akawaua Wapalestina waliokuwa watoa habari kwa Israel. Aliamuru kunyongwa kwa Wapalestina wanaoshukiwa kufanya kazi kwa Israel.

Yahya Sinwar yuko JUU ya orodha ya Israeli ya watu wanaofuata kwa mauaji. Ni suala la muda tu. Sinwar anafikiriwa kuwa mastermind wa shambulio la Oktoba 7, na mnamo 2021, alitishia kurusha roketi 1111 katika shambulio la awali dhidi ya Israeli.

Israel ilimuua kiongozi huyo (Ismail Haniyeh) ambaye alikuwa "akijadiliana" kwa ajili ya kusitisha mapigano, na sasa Israel italazimika kukabiliana na kiongozi huyo mwenye msimamo mkali zaidi ambaye anataka kujenga upya uwezo wa kijeshi wa Hamas kwa muda mfupi.

Screenshot_20240807-061516~2.png
 
Hivi sheria za kimataifa zinasemaje pale jirani yako anakuja kwako na kumuua mgeni wako?Nataka kujua sheria na sio hiyo invasion ambayo najua uki react the results is war
 
Huyu Yahya Sinwar ni mtata kupita maelezo.

Alishawahi kukamatwa na kupigwa mvua za kutosha na kwenye magereza ya Israel

Hivyo Israel itarajie kuendelea kupata upinzani mkubwa zaidi kutoka Hamas
 
Mods unganisheni huu uzi
Ule mwingine ulioanzishwa na Uzalendo wa Kitanzania una makosa. Umemtaja Mohamed Ismail kama kiongozi. Manukau "Hamas imemchagua Mohammed Ismail Darwish kuwa kiongozi wake mpya. Hii inafuatia kuuawa kwa kiongozi wa zamani wa kisiasa wa kundi hilo, Ismail Haniyeh, huko Tehran, wiki moja iliyopita."

Huo una misinformation ndiyo unapaswa kuletwa huku.
 
MODS: Mumeharibu uzi wangu kwa kuchanganya na habari za uwongo. Narudia ku-post upya. Tafadhali uacheni.

Yahya Sinwar ameteuliwa kuwa Kiongozi Mkuu wa Hamas kumrithi Ismail Haniyeh aliyeuliwa majuzi akiwa Iran na mazishi yake yalifanyika Qatar.

Yahya Sinwar ndiye aliyepanga na kuratibu mauaji ya October 7, 2023 huko Israel Kusini, na kusababisha vita ambavyo mpaka sasa Wapalestina zaidi ya 38,000 kufariki na Wayahudi wapatao 1,200 kuuliwa. Bila kusahau Watanzania 2 pia wamekufa kwenye mgogoro huo

View attachment 3063369
Bodyguard wa haniyer alikuwa anafanya nini saa 8 usiku kwenye chumba cha Haniyer ?
 
MODS: Mumeharibu uzi wangu kwa kuchanganya na habari za uwongo. Narudia ku-post upya. Tafadhali uacheni.

Yahya Sinwar ameteuliwa kuwa Kiongozi Mkuu wa Hamas kumrithi Ismail Haniyeh aliyeuliwa majuzi akiwa Iran na mazishi yake yalifanyika Qatar.

Yahya Sinwar ndiye aliyepanga na kuratibu mauaji ya October 7, 2023 huko Israel Kusini, na kusababisha vita ambavyo mpaka sasa Wapalestina zaidi ya 38,000 kufariki na Wayahudi wapatao 1,200 kuuliwa. Bila kusahau Watanzania 2 pia wamekufa kwenye mgogoro huo

View attachment 3063369
Tumpe siku ngap
 
Back
Top Bottom