Yajayo yanafurahisha. Je, uko tayari?


Tatizo huku elewa hoja ilipojikita. Ukiona jambo ambalo nwanadamu amekifanya ujue liko ndani ya uwezo yake aidha kwa kujua au kwa kutokujua na ukiona jambo ambali mwanadamu amelishindwa na hato liweza ujue liko nje ya uwezo wake,
 

Maendeleo acha yaendelee kutokea ila mwanadamu kutokujua ukomo wa uwezo ni upuuzi ulio komaa.

Mathalani hakuna dawa ya kuzuia uzee bro,hapa wajiitao wana sayansi wame mili upate mmoja tu wa uzee,yaani muonekano,hali ya kuwa uzee ni zaidi ya muonekano,uzee ni zaidi ta umri bali ukizeeka ujue unazeeka akili,moyo mpaka mwili.

Angalia suala la kifo,hakuna anae jua atakufa kwa lipi,hakuna anae jua atakufa lini na atafia wapi ? Bro wanakufa wazima,wanakufa wagonjwa na wanakufa watoto.

Nipo ....
 
Mwanadamu yeyote anapokutana na changamoto ndipo hutumia vizuri uwezo wake wa kufikiri na kutenda
 
Tatizo huku elewa hoja ilipojikita. Ukiona jambo ambalo nwanadamu amekifanya ujue liko ndani ya uwezo yake aidha kwa kujua au kwa kutokujua na ukiona jambo ambali mwanadamu amelishindwa na hato liweza ujue liko nje ya uwezo wake,
Mambo yote yapo ndani ya uwezo wetu.

Lisilowezekana leo litawezekana kesho kwa kutumia Bongo hizihizi zilizoshindwa jana
 
Mambo yote yapo ndani ya uwezo wetu.

Lisilowezekana leo litawezekana kesho kwa kutumia Bongo hizihizi zilizoshindwa jana

Kanuni za uumbaji haziko hivyo. Hivi ushawahi kujiuliza kwanini urefu wa mchana uko vile vile na urefu wa usiku uko vile vile ? Au hili pia huwa mnajifariji ipo siku kwa kutumia akili hizi itawezekana kupeleka masaa mbele au kurudisha nyuma ? Kama hili haliwezekani kwanini kwanini wasijue ya kuwa mengine hayawezekani ?

Kaka huo msemo hautumiki katika kila jambo,japokuwa msemo huu huwa tunautumia sana katika kujifariji.

Hivi kuna mtu anajua umbile halisi la upepo au njaa ? Au hili pia mtakuja kulijua miaka ijayo ?
 
Mambo yote yapo ndani ya uwezo wetu.

Lisilowezekana leo litawezekana kesho kwa kutumia Bongo hizihizi zilizoshindwa jana

Hii kauli inaonyesha ni jinsi gani huitumii akili yako vilivyo na hutafakari mambo katika uhalisia na hili tatizo wanalo wengi wanasayansi na wanafalasafa pia.
 
Unaweza ukaprove kuwa hakuna mtu aliye kufa kabla ya sku zake??



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je waafrica hatukutani na changamoto tukazitatua mpaka tutatuliwe

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwafrika kafunikwa na starehe zilizo tayari zaidi huku akidhani kuna msaada nje ya maarifa na kujituma,,, dini pia huchangia kwa sababu jambo dogo tu mtu anamwambia "namwachia Mungu, hao wanasayansi wanaingilia kazi ya Mungu, uwezo wetu una mipaka, Mungu ndio muweza wa yote, Mungu atatenda, Mungu ndio kila kitu, Mungu atasaidia nk ;"

Sasa matumaini hewa ya namna hiyo yanazidi kutuchelewesha

Pia Mwafrika hana jadi ya kupanga mipango ya muda mrefu/kufikiri hatma ya vitukuu wake na vitukuu wa vitukuu wake, au kufikiri hatma ya dunia na ulimwengu kwa ujumla huko baadae

Jambo hili lilichangizwa na linaendelea kwa sababu ya jamii fulani ya wanadamu walikuwa wamewahi kuendelea, hivyo jamii hiyo baada ya kuingia kwenye jamii yetu ikaweka taratibu zao zenye kuwanufaisha wao vizazi na vizazi

Wenzetu wanawaandaa watoto wao tangu wanakua huku serikali zao zikiweka mazingira mazuri kwaajili ya kuwapokea watoto hao walioandaliwa vyema kiakili na kimwili, tena wakiwatazama kwa ukaribu ili wajue huyu anapenda nini na huyu anapenda nini

Kwani wewe ungekuwa unafanya kazi uliyokuwa unaipenda tangu utotoni unafikiri ungepatwa na msongo wa mawazo? Au ungeiba? Je, ungedhulumu? Au ungeweza kutohudhuria kazini kwa visingizio lukuki? Ungeharibu kazi yako au serikali ingeenda kuchukua waajiri nje?

Amini nakwambia, kama kila mwanadamu angefanya ile kazi/kipawa aliyokuwa anaipenda tangu mwanzo asingeifanya kwa manung'uniko.

Kufanya kile ukipendacho huleta matokeo ya wewe kuifanya hiyo kazi kwa bidii bila kusimamiwa
Huleta matokeo ya maongezeko mazuri kwenye jamii hivyo kuondoa upungufu wa ukosefu wa huduma fulani
Huleta matokeo ya wewe mhusika kuwa na afya nzuri ya akili na mwili
Huleta matokeo ya uchumi wa dunia kukua bila kutumia nguvu nyingi
Huleta matokeo ya uaminifu na upendo kazini na kubwa kuliko yote, walimu wangefanya kazi kwa wepesi zaidi huku wakisaidiwa na wanafunzi wao kwa kuwa wanachofundishwa wanakipenda na wakiwa majumbani mwao hupenda kukirudiarudia kwa vitendo.
Shule tungekuwa tunapita kwa kipindi kifupi alafu tunaelekea kwenye kazi zetu kwa furaha.

Mambo yapo Afrika sana lakini kwa mabara mengine yapo kwa uchache alafu wanajitahidi kupigana nayo ilihali kwetu ndio yamegeuzwa kama fursa.

Mtu ananunua cheo utegemee afanyeje kwenye hiyo ofisi?

Hana fani na kazi fulani lakini anainunua [emoji23]

Kwakweli Afrika tulifelishwa lakini sisi wenyewe tukaendelea kujifelisha

Kwa Afrika viongozi waliopo wametumiwa na kutumika kuharibu wananchi wao akili ili wao (viongozi wetu) wafaidi chini ya 10% ya matunda ya Afrika huku waliotutawala wakifaidi juu ya 80% ya keki ya Afrika.

Kwahiyo jibu la haraka kuhusu swali lako ni kwamba, Afrika hatutatuliwi changamoto bali wanazidi kutusokomezea kwenye matatizo zaidi.

Hata wewe huwezi kumpiga tafu jirani yako awe levo zako au akuzidi.

Kitakachotuokoa Waafrika labda tupate viongozi wazuri alafu haya mataifa makubwa yaingia kwenye mgogoro mkubwa wastani
 
Kwanini unaamini hatuwezi kuondoa usiku?

Swala la masaa liache lilivyo maana kiuhalisia hamna kitu kama hicho. Kuna maeneo ukikaa hamna mabadiliko haya ya saa moja, saa mbili, saa tatu na kuendelea

Huu ni utaratibu tuliojiwekea hapa duniani
 
Kwanini unaamini hatuwezi kuondoa usiku?

Swala la masaa liache lilivyo maana kiuhalisia hamna kitu kama hicho. Kuna maeneo ukikaa hamna mabadiliko haya ya saa moja, saa mbili, saa tatu na kuendelea

Huu ni utaratibu tuliojiwekea hapa duniani

Una maanisha hakuna muda au ? Haoa sijakuelewa.

Pili huwezi kuelezea usiku bila kuzungumzia masaa.

Yaani ni kama vike ilivyo binadamu hawezi kuwa bila moyo na mfano wake.

Ina maana kuna sehemu hakuna usiku na mchana au ?

Naomba ufafanuzi vizuri wa kauli yako.
 
Ndio yapo maeneo ni giza tu miaka na miaka kama ilivyo kwamba kuna maeneo ni nuru tu miaka na miaka

Usiku na mchana ni utaratibu tu wa kutofautisha pande mbili za dunia. Upande ambao unamulikwa na jua na ule upande ambao mwanga huo wa jua hauwezi kumulika kwasababu ya kivuli cha dunia

Kuna satellite ambazo zipo angani zinatembea na mchana tu week, miezi na miaka

Pia kuna anga ukikaa hutoona nuru miaka maelfu na maelfu


Hii labda iwe mada nyingine sasa
 

Nitajie hayo maeneo kaka ambayo ni giza miaka yote na ni nuru miaka yote.

Na kama nu giza na ni nuru tupu,hii kauli yako ya miaka yote umeipata wapi ?
 
Tatizo huku elewa hoja ilipojikita. Ukiona jambo ambalo nwanadamu amekifanya ujue liko ndani ya uwezo yake aidha kwa kujua au kwa kutokujua na ukiona jambo ambali mwanadamu amelishindwa na hato liweza ujue liko nje ya uwezo wake,
Kuna mambo mengi yalikuwa yana shindikana now yana wezekan so muda ni mwamuzi wa kila kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu embu jaribu kufikiri kila mmoja duniani tunge kuwa na mawazo Kam yako unafikiri tungefika hapa.kujaribu ndo kume tufikisha hapa na bado tuna endelea.Mungu katupa marifa ndo haya tunaya tumia.je unajua kiwango na kikomo cha marifa tuliyo pewa?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…