Je waafrica hatukutani na changamoto tukazitatua mpaka tutatuliwe
Sent using
Jamii Forums mobile app
Mwafrika kafunikwa na starehe zilizo tayari zaidi huku akidhani kuna msaada nje ya maarifa na kujituma,,, dini pia huchangia kwa sababu jambo dogo tu mtu anamwambia "namwachia Mungu, hao wanasayansi wanaingilia kazi ya Mungu, uwezo wetu una mipaka, Mungu ndio muweza wa yote, Mungu atatenda, Mungu ndio kila kitu, Mungu atasaidia nk ;"
Sasa matumaini hewa ya namna hiyo yanazidi kutuchelewesha
Pia Mwafrika hana jadi ya kupanga mipango ya muda mrefu/kufikiri hatma ya vitukuu wake na vitukuu wa vitukuu wake, au kufikiri hatma ya dunia na ulimwengu kwa ujumla huko baadae
Jambo hili lilichangizwa na linaendelea kwa sababu ya jamii fulani ya wanadamu walikuwa wamewahi kuendelea, hivyo jamii hiyo baada ya kuingia kwenye jamii yetu ikaweka taratibu zao zenye kuwanufaisha wao vizazi na vizazi
Wenzetu wanawaandaa watoto wao tangu wanakua huku serikali zao zikiweka mazingira mazuri kwaajili ya kuwapokea watoto hao walioandaliwa vyema kiakili na kimwili, tena wakiwatazama kwa ukaribu ili wajue huyu anapenda nini na huyu anapenda nini
Kwani wewe ungekuwa unafanya kazi uliyokuwa unaipenda tangu utotoni unafikiri ungepatwa na msongo wa mawazo? Au ungeiba? Je, ungedhulumu? Au ungeweza kutohudhuria kazini kwa visingizio lukuki? Ungeharibu kazi yako au serikali ingeenda kuchukua waajiri nje?
Amini nakwambia, kama kila mwanadamu angefanya ile kazi/kipawa aliyokuwa anaipenda tangu mwanzo asingeifanya kwa manung'uniko.
Kufanya kile ukipendacho huleta matokeo ya wewe kuifanya hiyo kazi kwa bidii bila kusimamiwa
Huleta matokeo ya maongezeko mazuri kwenye jamii hivyo kuondoa upungufu wa ukosefu wa huduma fulani
Huleta matokeo ya wewe mhusika kuwa na afya nzuri ya akili na mwili
Huleta matokeo ya uchumi wa dunia kukua bila kutumia nguvu nyingi
Huleta matokeo ya uaminifu na upendo kazini na kubwa kuliko yote, walimu wangefanya kazi kwa wepesi zaidi huku wakisaidiwa na wanafunzi wao kwa kuwa wanachofundishwa wanakipenda na wakiwa majumbani mwao hupenda kukirudiarudia kwa vitendo.
Shule tungekuwa tunapita kwa kipindi kifupi alafu tunaelekea kwenye kazi zetu kwa furaha.
Mambo yapo Afrika sana lakini kwa mabara mengine yapo kwa uchache alafu wanajitahidi kupigana nayo ilihali kwetu ndio yamegeuzwa kama fursa.
Mtu ananunua cheo utegemee afanyeje kwenye hiyo ofisi?
Hana fani na kazi fulani lakini anainunua [emoji23]
Kwakweli Afrika tulifelishwa lakini sisi wenyewe tukaendelea kujifelisha
Kwa Afrika viongozi waliopo wametumiwa na kutumika kuharibu wananchi wao akili ili wao (viongozi wetu) wafaidi chini ya 10% ya matunda ya Afrika huku waliotutawala wakifaidi juu ya 80% ya keki ya Afrika.
Kwahiyo jibu la haraka kuhusu swali lako ni kwamba, Afrika hatutatuliwi changamoto bali wanazidi kutusokomezea kwenye matatizo zaidi.
Hata wewe huwezi kumpiga tafu jirani yako awe levo zako au akuzidi.
Kitakachotuokoa Waafrika labda tupate viongozi wazuri alafu haya mataifa makubwa yaingia kwenye mgogoro mkubwa wastani