Kuna harusi nilienda ya ndugu zangu, mama mkwe alikuwa hampendi bibi harusi yaani mkwewe! Hilo limama mkwe lika enda kuchukua mike likaanza kuimba ule uwimbo wa kichaga 'kiwaro apa ndenga '. Ile ndoa haikukaa wakaachana! Na lile li mama mkwe mume wake akafa! Na ndoa za watoto wake woote zikavunjika....wajukuu wake wote yule mama wamegeuka mateja! Kasoro wajukuu wa yule dada aliyo imbiwa huo uwimbo tu ndiyo wenye hekima na busara! Tujichunge sana vinywa vyetu mdomo unaumba! Mola mkubwa sana!Ndenga ni Janga
Mbora = barakaMborooo -mbowe au muro
HahahaaMiss chagga - nakupenda pesa
We una balaa hakika[emoji12] [emoji12] [emoji12]Elbashite maana yake mtoto mpendwa,kipenzi wa Raisi.
Ahsante kwa Nasaha, Isis.Tujichunge sana vinywa vyetu mdomo unaumba! Mola mkubwa sana!
Ndiyo maana unaambiwa jitamkie mambo mema!Ahsante kwa Nasaha, Isis.
Mdomo unaumba katika mabaya pekee au hata katika masuala mema?. Utasikia, usimcheke..utakuja kuzaa kama yule. Is it true?.
Naomba kuuliza. Ukimcheka mtu bora, mwenye mafanikio katika material thing's (tajiri), kiongozi, watu wenye hekima/busara (kwa mazoea ya akili ya ki-Afrika). Je, utakuja kuzaa kama hao?.
Nomba unitoe tongotongo katika hilo.
Asalaam.
Mimi siyo mtoa mada, Naomba kuongezea nyama kidogo..Mtoa mada hayo ni majina ya kichaga au ya kipare....!!?
Ahsante kwa kunifunulia Juzuu..Ndiyo maana unaambiwa jitamkie mambo mema!
Mimi mwenyewe ninayo hiyo nguvu!
Nikikutamkia mema yanakuwa na nikikutamkia mabaya yanayokea!
Ni vipaji ambavyo watu wachache wanavyo na hawajui na wengine wanajijua!
Asante kwa elimu ndugu.....Mimi siyo mtoa mada, Naomba kuongezea nyama kidogo..
Baadhi ya majina hapo juu ni ya kichaga, mengine siyo. Ni kule tu kushindwa kung'amua. Nb; kumbuka Ukristu ulileta mengi- haswa katika U-Lutheri.
Majina yote yanayoanziwa na "Eli/kuishiwa na "Eli" siyo ya Kichagga/ kiasili. Ni kughushi majina ya asili kwa kuongezea utamaduni wa kimagharibi unaonasibishwa na dini-Lutheran.
Ndiposa, Waluteri ndio wa kwanza katika Tanganyika na sasa Tanzania kutumia lugha za asili katika ibada na liturgia zao. Ukitembea-haswa vijijini siku za Jumapili katika makanisa ya Walutheri basi unaweza kuwasikia wakiendesha Ibada zao kwa Lugha zao.
Neno 'Eli' limetoholewa kutoka kiebrania "Elohim", yaani Mungu.
Pendaeli-Penda Mungu/ Mpende Mungu"
Eliapenda-Mungu apenda.
Eliasikia. Eliatosha. Elinaja na orodha inaendelea..
Wapare wana ya kwao, Natanaeli, Fahamueli, Elihuruma..concept ni dhana na U-Lutheri.
Asalaam, KikulachoChako.
Cc- 2013 .
Mungu anajuaEliaichi maana yake nini?