Mimi siyo mtoa mada, Naomba kuongezea nyama kidogo..
Baadhi ya majina hapo juu ni ya kichaga, mengine siyo. Ni kule tu kushindwa kung'amua. Nb; kumbuka Ukristu ulileta mengi- haswa katika U-Lutheri.
Majina yote yanayoanziwa na "Eli/kuishiwa na "Eli" siyo ya Kichagga/ kiasili. Ni kughushi majina ya asili kwa kuongezea utamaduni wa kimagharibi unaonasibishwa na dini-Lutheran.
Ndiposa, Waluteri ndio wa kwanza katika Tanganyika na sasa Tanzania kutumia lugha za asili katika ibada na liturgia zao. Ukitembea-haswa vijijini siku za Jumapili katika makanisa ya Walutheri basi unaweza kuwasikia wakiendesha Ibada zao kwa Lugha zao.
Neno 'Eli' limetoholewa kutoka kiebrania "Elohim", yaani Mungu.
Pendaeli-Penda Mungu/ Mpende Mungu"
Eliapenda-Mungu apenda.
Eliasikia. Eliatosha. Elinaja na orodha inaendelea..
Wapare wana ya kwao, Natanaeli, Fahamueli, Elihuruma..concept ni dhana na U-Lutheri.
Asalaam, KikulachoChako.
Cc-
2013 .