Yajue Makabila Yanayopatikana Tanzania Visiwani ( Zanzibar )

MKURABITA

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2010
Posts
317
Reaction score
126
Wadau,

Naomba mnisaidie hili swala, Hivi Zanzibar kuna makabila kama ilivyo Bara? Na kama yapo ni mangapi.?

Kuhusu Lugha Ukanda wa Pwani.

 
Kitabu cha historia cha zamani cha darasa la tano, historia ya jamii za waafrika hadi mwaka 1880, kiasema zenji kulikuwa kuna makabila ya wahadimu, watumbatu ,wamvita na jingine nimelisahau, ila wazenji wengine wanakataa wanadai haya si makabila ila ni jamii tu.

Kumbuka waafrika wa asili waliokuwa zanzibar miaka mingi nahisi walichukuliwa utumwani wakauzwa arabuni au elsewhere na wale walioko kule ni wale watumwa waliopelekwa kule kufanya kazi kwenye mashamba ya mikarafuu na minazi ili kuwa wakwezi na kutengeneza mbata (labda ndio maana weusi wengi kule wana asili ya unyamwezi) au watu walioenda zanzibar kutafuta maisha(mfano abeid karume inadaiwa alitoka malawi).

Istand to be corrected
 
Wadau, naomba mnisaidie. Hivi Zanzibar kuna makabila kama ilivyo Bara? kama wachaga, wahaya, jaruo, wakwere n.k. Na kama yapo ni mangapi.

Nadhani yapo sabab kuna lahaja toafuti za kiswahili zinazungumzwa hata ndani ya zenj. hizo lahaja za kiswahili zinaweza kuchukuliwa kama makabila.
 

Kwa hiyo kimsingi Zanzibar ilikuwa shamba la karafuu. Sasa hili shamba la karafuu linawezaje kuwa na makabila?

Mkuu wa shamba hili la karafuu sasa hivi anaitwa Daktari Shein. Msaidizi wake wa karibu au katibu muhtasi anaitwa Sefu Sharifa Hamadi.
 
Zanzibar hakuna makabila kuna Watu wanaotoka Kisiwa cha Unguja na kisiwa cha Pemba na Wenyewe wanajuwana kwa Lugha ya Kiswahili chao wanachozungumza Mtu wa Unguja ndie anayezungumza Kiswahili Fasaha kuliko Mtu kutoka kisiwa cha pemba wenyewe kwa

wenyewe hutaniana, kwa kusema wewe watoka Pemba mimi natoka unguja. au Wewe ni mpemba na mimi ni Muunguja hakuna kitu kabila. Ila kulikuwa na Waarabu walioleta Biashara

ya utumwa kuwachukuwa watu kutoka Tanganyika kuwaleta Visiwani Pemba na Unguja na baadhi yao ndio hao waliokuwepo mpaka hivi sasa wengi wa Watu wanaotoka Visiwa vya Unguja na Pemba wanatoka huku Tanzania bara.
 
jamani mbona nasikia 'waarabu wa pemba hujuana kwa vilemba?' hakuna waarabu huko, au uarabu si kabila?
 
yapo makabila.. ma 3 nafkri kama sikosei
 
Kwikwikwi.

Kutoka na research zangu yapo makabila. Neno kabila ni neno lilokopwa kutoka kwenye kiarabu (family group characterised by a common family name). Hivyo basi watu kuzungumza lugha moja haina maana kuwa hakuna makabila. Ukoo unaotumia jina moja unatosha kuunda kabila.

Maisha ya waAfrika yalikuwa yapo kwenye ukoo. Lakini upangaji wa makabila ya sasa yametokana na ujio wa wakoloni. Wakoloni walikusanya watu wenye kuzungumza lugha moja na kuita kabila. Lakini hivyo sisi wenyewe tulivyojigawa.

Kwa mfano kabila la wahaya lilianzishwa na wakoloni. Lakini ndani ya wahaya kuna wa Kanyigo, kuna wanyambo n.k

Kule Nigeria kuna waIbo. Lakini hili halikuwa kabila moja mpaka wakoloni walipogawa watu kwa kutumia lugha.

Sasa ukija pwani ya Afrika mashariki, tayari kulikuwa na city-states. Katika city-states hizi tayari watu walikuwa wanaishi kwa koo zao na kutumia kiswahili.

Wakati wagiriki wanatembelea Azania, zaidi ya miaka 2000 iliyopita tayari city states hizi zilikuwepo na watu walikuwa wanazungumza kiswahili. Hivyo si kweli nadharia mnazozitoa hapa.

Katika kitabu chake cha Isimu ya Lugha, Father Nkwera anasema kuwa wakati Ibn Batuta anatembelea East Africa alikuta watu wanalonga kiswahili.

Na ni mkoloni aliyechagua kiswahili cha unguja kuwa ni standard swahili. Na hii ndio sababu mtu wa unguja anaona kuwa kiswahili chake ni bora. Lakini hakuna ubora wowote ule kwa sababu kiswahili kilichozungumzwa katika city-state zingine zilikuwa ni lugha kamili katika states hizo.
 

Nashukuru sana wadau kwa michango yenu nimepata kuelimika.
 
Jamani Zanzibar kuna makabila wahamiaji kama Waluguru, Wachaga., Sukuma,NYamwezi, Watumbatu, Wapare nimeshuhudia Demu wangu yeye ni Mchaga lakini tokea enzi zile baba mzaa babu yake alizaliwa kule na sasa wao ukiwaona ni Zanzibar piwa lakini ukimchimba anakwambia yeye ni mchaga ila hapajui Kilimanjaro na kabisa na majina ya Ukoo hawatumii kwahiyo kwa urahisi uwezi kumjua mpaka umchimbe. WE NEED CHANGES :A S angry:
 
Wadau, naomba mnisaidie. Hivi Zanzibar kuna makabila kama ilivyo Bara? kama wachaga, wahaya, jaruo, wakwere n.k. Na kama yapo ni mangapi.



Mkuu Zakumi, maelezo yako kwa swali la Mkurabita yanatia mwangaza kwenye swala zima la historia ya Kiswahili chetu na makabila. Lakini hata hivyo naona maelezo yako yanakwepesha swala la msingi ndani ya swali lake, kama jinsi nilivyolielewa mimi na baadhi ya wachangiaji wengine hapo juu.

Mkurabita ameuliza na kutolea mfano utofauti wa kikabila pragmatically, kama vile Wachaga, Wahaya, Wajaruo na Wakwere. Basi kwa jinsi nilivyomuelewa mimi anachotaka kujua ni lugha zipi hizo (mimi sizifahamu) mbali na lahaja au lafudhi mbalimbali za Kiswahili zilizopo Zanzibar na Tanzania Bara (kama zipo au zilikuwepo huko Zanzibar). Tukumbuke kwamba regional accents zipo kila pahala duniani. Akina Bush wa Texas hawana lafudhi sawa na kina Palin huko Alaska, vivyo hivyo watu wa NY wanaongea tofauti na watu wa Miami. Ma-scouser wa Liverpool ni tofauti na ma-cockney wa London, Waspanish wa Madrid nitofauti kabisa na waongeao kihispania kule Venezuela n.k. Hizi ni variations au lahaja za lugha na zinatokana na mkusanyiko wa koo mbalimbali zenye kutumia lugha hiyo. Hivyo maelezo yako kwa jinsi nilivyoyaelewa mimi yamejikita katika kuelezea asili na tofauti hizi katika Kiswahili. Wakati swali la Mkurabita nikutaka kujua uwepo wa lugha nyinginezo za Kibantu (au asili nyingine) mbali na Kiswahili. Lakini kwasabau Kiswahili nayo ni lugha, na kama ndiyo pekee iliyokuwepo/iliyopo Zanzibar, basi uniwie radhi maana maelezo yako yanatosheleza kabisa, yakwamba lugha hiyo huko Zanzibar ni Kiswahili (ila kwa koo tofauti tofauti na lahaja tofauti tofauti).

Swala jingine, nakubaliana nawe kuwe maisha ya Waafrika yalikuwa yapo kwenye koo.Si hivyo tu, bali mpaka sasa koo nyingi bado zinaendelea kuwepo. Mkuu ningelipenda utoe maelezo pale unaposema kuwa upangaji wa makabila uliopo sasa hivi umetokana na ujio wa wakoloni. Je, unataka kutueleza kuwa kabla ya wakoloni kuja, koo hizi unazosisema zilikuwa zimetapakaa huku na kule kila pahala ila wakoloni ndiyo walizikusanya? Mfano, baadhi ya Wahaya na Wasukuma bila kujali chimbuko lao walikuwa Pwani na Nyanda za kusini na wengine kanda za maziwa makuu, ila wakoloni ndiyo waliwakusanya na kuwaweka pamoja wote kanda za ziwa Victoria? (kama mfano). Na si kwamba, hizi koo zinazoongea lugha moja na kuelewana (achilia mbali Kiswahili) zilikuwa zimejikusanya kanda mbalimbali kwa common interest kabla ya hata hao wakoloni kuja?!

Vinginevyo, nashukuru kwa mwangaza wa maelezo yako hapo juu.

Steve Dii
 
Nashukuru kwa kunielewa vema mkuu, hili ndo hasa lilikuwa lengo la swali langu.
 


Zakumi na Steve Dii mnapoints nzuri. Ingekuwa vizuri sana kama watanzania wengine tungekuwa na mwelekeo wenu.

Ukiangalia kwa undani unaweza kuona kuwa JKN alikuwa anajitahidi sana kuifanya Tanzania iwe Nation-state sio a Nation made up of states kama walivyotuacha waingereza, alikuwa anajaribu kuifanya Tanzania iwe kama Zanzibar ambako makabila yame-disolve kwenye uzanzibar.

Nafahamu kuwa kulikuwa na wamtan'gata, watumbatu, wanguja, na mengine lakini sasa hakuna. Pamoja na kuwa wenyewe wanaita jamii kwa ujumla kulikuwa na hall marks zote za makabila. Historia inaonesha hivyo.

Hata wazanzibari wa sasa ukiangalia kuna wengi ni wahamiaji toka bara, lakini ukiwauliza nyie kabila gani wanasema hawajui, lakini wamewahi kusikia kuwa baba au mama ni wa kabila fulani toka bara, au kabila fulani toka shelisheli and alike. Uzuri ni kwamba Zanzibar ni state, na watu wake ni wazanzibar, inagawa siku hizo wanasiasa wameanza kuwagawa kwa upemba na uunguja.

Huku bara misingi aliyoiacha JKNyerere sasa ina nyufa nyingi, umeanza udini na ukabila, kasi ya kuunda Nation state imepungua, tumeanza kuunda nation with states in it.
 
@ original pastor weye huwezi kupata demu wa kizenj hata siku moja labda useme ulikwenda zenj ukakutana na mnyamwezi mwenzio ambae amekwenda sawa na weye. Wacha kujipakazia weye **** nini?
 
Hao watu wanaodai kuwa hizo ni jamii tu na si makabila, hawaelewi maana ya neno kabila "Kabila" kama alivyo eleza Zakumi ni neno lililokopwa kutoka kwenye Kiarabu... Na maana yake ni mkusanyiko wa jamii za wahamihaji (nomadic families of the same blood). Tunapotaja koo hizi zinapatikana ndani ya kabila moja...!

Zanzibar makabila yapo mfano kuna Watumbatu, Wahadimu, Wapemba na Wadiba Gonga hapa unaweza kupata mwanga kidogo.
 
@ original pastor weye huwezi kupata demu wa kizenj hata siku moja labda useme ulikwenda zenj ukakutana na mnyamwezi mwenzio ambae amekwenda sawa na weye. Wacha kujipakazia weye **** nini?
Hawapatikani kivipi mkuu...? Ina maana ukipeleka posa kwa kuwa wewe unatokea bara upewi mke?
 
Nimeulizwa hili swali nikachemka,eti huko Zanzibar kuna makabila mangapi au ni Wapemba na Waunguja?
 
Kuna makabila mengi pamoja na WAHA, WANYAMWEZI na WASUKUMA. Wapemba au Waunguja siyo makabila ila ni watu wanaoishi Pemba na Unguja kama vile uanze kusema kuna kabila la Wamorogoro, Wairinga, Watabora nk
 
Waunguja, wagunja, washiraji, washihiri......................
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…