Yajue Makabila Yanayopatikana Tanzania Visiwani ( Zanzibar )

Yajue Makabila Yanayopatikana Tanzania Visiwani ( Zanzibar )

Kuna makabila mengi pamoja na WAHA, WANYAMWEZI na WASUKUMA. Wapemba au Waunguja siyo makabila ila ni watu wanaoishi Pemba na Unguja kama vile uanze kusema kuna kabila la Wamorogoro, Wairinga, Watabora nk

mbona sijawahi sikia mtu anaongea ki-iringa au kimorogoro huwa nasikia anaongea kibena,kihehe au kinyakyusa ila huwa naskia mtu anaongea kipemba
halafu kumbukumbu zangu zinaonesha kipemba ndio kilisanifiwa na kutuletea kiswahili hichi tukitumiacho kama lugha ya taifa
hivi hii haitoshi kuamini kuna kabila la wapemba
 
Last weekend nilikua Zanzibar nikauliza same question kwa mwenyeji wangu,
Alichonijibu ni kua makabila ya wenyeji yapo, na kilugha chao ni kiswahili cha ajabu sana ambacho kinatofautiana kati ya kabila moja na jingine, ila mgeni hawezi kugundua.
Akatoa mfano kuna kabila nimelisahau wao jiwe wanaita jibwe.
Hao mnaowaita wasukuma, wamakonde n.k kule ni wazamiaji tu,
Ni sawa na wengine tunavyojiachia hapa Dsm wakati kijijini kwetu Nanjilinji wanatuhitaji tukaendeleze kijiji.
 
Inasemekana Zanzibar ilianza ustaarabu na biashara na nchi za mbali tangia 2500-2400 BC.

Wakifanya biashara na Waarabu na haswa kutoka Yemen, Ghuba ya Uajemi Iran (na haswa Washiraz), na west India inasemekana kutoka Goa mwanzoni mwa karne ya kwanza AD.

Vilevile kuna Wangazija toka Komoro, Watumbatu (Wamakunduchi) "Wahadimu" Wapemba, Wanyamwezi, Wanyanyembe, Wamauli, Mazrui, Wahiyao,Wamakonde, Wamakua, Wandonde, Wandengereko, Wangoni, Wangindo, Wamatengo n.k.

Ila kwa sasa makabila makubwa kabisa yaliyopo sasa hivi Zanzibar ni CCM na CUF


Watu Maarufu:
  • Sheikh Abdulla Saleh Farsy, Islamic Scholars and the Chief Kadhi of Zanzibar, Inspector General of primary schools on Zanzibar and Pemba.
  • Hamed bin Mohammed el Marjebi (Tippu Tip) Ivory merchant
  • Siti binti Sadi, Singer
  • Barghash bin Said, The third Sultan of Zanzibar
  • Freddie Mercury (born Farrokh Bulsara) of the rock band Queen
  • Murtaza Alidina, scholar
  • Farouque Abdillahi, was Princess Diana's designer
  • Farouk Topan, Mwandishi wa riwaya
  • Said Khamis, Mwandishi wa riwaya
  • Adam Shafi Adam, Mwandishi wa riwaya
  • Mohamed Suleiman Mohamed, Mwandishi wa riwaya
  • Said Ahmed Mohamed, Mwandishi wa riwaya
  • Abeid Amani Karume, Rais wa kwanza Zanzibar
  • Mwinyi Aboud Jumbe, Rais wa pili Zanzibar
  • Abdulrahman Muhammad Babu, Mwanasiasa
  • John Okello, Mamruki wa Kivita
 
Wasukuma wanaishi Sukumaland, Wanyamwezi wanaishi Nyamwezi, Waluguru wanaishi milima ya uluguru .... au vipi?
 
Naomba nielimishwe, Zanzibar kuna makabila mangapi? Ukiachia kuzungumza lugha ya Kiswahili, wana lugha zao za asili? Na kwann wazanzibar wanapenda kujiona waarabu kuliko wabantu? Asanteni.
 
Zanzibar ina wazanzibar wao wanapenda kujiita wazanzibar, ukiangalia walio wengi kama three to four generations wana asili ya bara, arabuni na ngazija. Kuna wengine wamechanganya damu za makundi hayo matatu na kuamua kujiita wazanzibar halisi. Lakini kama tungeweza kufanya geneology ungegudua kuwa wengi wana asili ya wabara, hasa wale wanaotokana na vizazi vya watu waliokamatwa na Tip Tippu...kuanzia Kigoma, Tabora, Dodoma hadi maeneo ya Pwani. Ukiangalia morphology yao unaweza kujua.
Lakini usisahau waaarabu, sijui kama uarabu ni kabila au race.
 
Hili neno Kabila nyie linawasaidia nini, mbona hamkuwi? Kabila lako lina kazi gani now days? Nyerere alisema mnaulizana makbila kwani mnataka kutambika?
Zanzibar hakuna kabila wala ukabila, kuna wazanzibari tu. Hata ile "shiraz" hivi sasa haina umuhimu. Ni Mzanzibari tu ndiyo muhimu.
 
Naomba nielimishwe, Zanzibar kuna makabila mangapi? Ukiachia kuzungumza lugha ya Kiswahili, wana lugha zao za asili? Na kwann wazanzibar wanapenda kujiona waarabu kuliko wabantu? Asanteni.
Pole sana ndugu yangu kwa kutaka kujua jambo usilolijua.Zanzibar kuna makabila pengine mengi zaidi ya hayo yalioko tanganyika lakini hayatumiki katika jamii iliostaarabika na ilioendelea.Kutumika kwa makabila ambayo tuliyaondowa wakati wa mapinduzi ni kutuambia turejeshe ukabila jambo ambalo limeshasahaulika.Kumbuka kua zanzibar ni kisiwa na Wahamiaji wa kisiwa huwa ni wafanya biashara au wavuvi kutoka nchi mbali mbali.Kwa mfano washihiri waliingia zanzibar kwa ajili ya kuuza nguru na wakahamia na wakaowa na mpaka leo hii wapo.Wakomoro waliingia zanaibar kwa biashara na mpaka leo hii wapo na makabila yao yote yapo.Waarabu waliingia zanzibar na wakahamia na wakaowa na mpaka leo hii wapo na makabila yao yote yapo.Watanganyika kutoka mwambao wa pwani,Tanga,mafia n.k walikuja zanzibar kwa kuvua na wakaowa na mpaka leo hii wapo na makabila yao yote yapo.Na kwa upande wa lugha hicho kiswahili unachongea leo hii na kujivunia kuwa ni lugha ya Taifa ndio lugha asili ya Zanzibar na kwa vile Wazanzibari ndio waliokuwa wenyeji wa kisiwa hawakutaka lugha yao ibadilishwe na wageni walio kua wakija kuhamia.Lakini mpaka leo hii baadhi ya makabila yanaongea lugha zao majumbani mwao tu na sipengine popote.
 
Ntachojua mie huku kama makabila basi ni kwa yale yanayotokana na mashamba, mfano Makunduchi kuna wamakunduchi, Tumbatu kuna watumbatu, Donge kuna wadonge, n.k. kuhusu lugha kuna zile kwenye lugha tunaita lahaja, mana Mimi wa mjini akiongea mmakunduchi kikwao sioni ndani hata kwa mikwaju
 
Back
Top Bottom