Yajue makundi manne ya dawa za kulevya & madhara yake

Yajue makundi manne ya dawa za kulevya & madhara yake

madabadaba

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2017
Posts
288
Reaction score
178
Kemikali yoyote au mchanganyiko ambao huleta mabadiliko ya kihisia na ufahamu ni dawa za kulevya.
Matumizi ya dawa za kulevya huleta utegemezi na usugu.

Utegemezi ni hali ya kushindwa kuishi maisha ya kawaida mpaka utumie dawa ya kulevya. Utegemezi huo huwa wa kisaikolojia na kiafya.

Kuna makundi manne ya dawa za kulevya

1. VIPUMBAZA

Vipumbaza ni aina ya dawa za kulevya ambazo hupunguza kasi ya ufanyaji kazi wa mfumo wa ufahamu. Mfano wa dawa hizi ni;
_ Pombe
_ Heroin
_ Mandrax nk

Unapotumia vipumbaza;
_ Kasi ya ufanyaji kazi wa mfump wa ufahamu hupungua.
_ Mapigo ya moyo hupungua.
_ Shinikink la damu hushuka
sana.
_ Kiwango kidogo huleta furaha
kubwa.
_ Kiwango kikubwa huleta
kizunguzungu, kuongea kwa
kuvuta ulimi, matendo yasiyo
ya busara, kuchanganyikiwa,
ubongo kushindwa kuratibu
mifumo mbalimbali ya mwili.


2. VICHANGAMSHO.

Hizi ni dawa za kulevya zinazoongeza kasi ya ufanyaji kazi wa mfumo wa fahamu.
Mfano wa dawa hizi ni;
_ Mirungi
_ Nicotine
_ Vidonge vya kupunguza hamu
ya kula.
_ Cocaine
_ Caffeine nk
Dawa hizi husababisha yafuatayo;
_ Kuongezeka kwa mapigo ya
moyo.
_ Ubongo kushindwa kuendesha
mifumo ya fahamu.
_ Kutokulala
_ Wasiwasi nk.


3. VILETA NJOZI.

hizi ni aina ya dawa zinazosababisha mtumiaji kuona maono au kusikia vitu visipokuwepo. Mfano wa dawa hizi ni;
_ Bangi
_ Uyoga (peyote, mescaline,
psilocybin)
_ LCD

Unapotumia vileta njozi mambo yafuatayo huonekana;
_ unasikia na kuona vitu
visivyokuwepo.
_ Kujiona unapaa.
_ Kuongezeka ukubwa wa
mboni ya jicho.
_ kubadilisha utambuzi nk


4. VIYEYUSHI.

Aina mbalimbali ya kemikali ambazo mvuke wake huweza kutumika kama kilevi. Mfano wa dawa hizi ni!
_ Petrol
_ Dawa za kuuwa wadudu
_ Dawa za kuondoa rangi za
kucha
_ Dawa za ganzi kama Nitrous
oxide, Propane, butane,
helium nk.

Matumizi ya viyeyushi husababisha yafuatayo;
_ Kuumwa na kichwa
_ Ongezeko ia hisia na
mwanga
_ Kupata njozi
_ Kizunguzungu
_ Mwili kukosa nguvu na hats
kuzimia nk


MADHARA (kijamii)

Watumiaji hukosa busara na umakini maishani hivyo kusababisha;
_ Magomvi na wazazi na
wanandoa.
_ Kushindwa kutunza familia
_ Ujambazi
_ Mauaji ya kikatili
_ Wizi nk

MADHARA (kiuchumi)

_ Kupungua kwa nguvu kazi
kwenye familia na taifa.
_ Kutumika vibaya kwa
rasilimali za familia na taifa
ktk kuwatibu waathirika.
_ Hasara itokanayo na uharibifu
wa Mali unaofanywa na
waathirika (ajali, fujo nk)

MADHARA (kiafya)

Utumiaji wa dawa za kulevya huambatana na matatizo mengi ya kiafya kama;

_ Saratani ya mapafu na damu
_ Kupungua kwa uwezo wa
damu kuchukua hewa (oxygen)
_ Kuharibika kwa mfumo wa
fahamu kunakoambatana na
ukiziwi, kichaa, kupungua
uwezo wa kukumbuka na
kufikiri, luppoza nk.

Pamoja na madhara hayo kwanini watu hawaachi kutumia dawa za kulevya?

Nawasilisha.
 
Kumbe bamgi haina madhara asante mtoa mada
 

Attachments

  • conspiracyfiles-20171218-0001.jpg
    conspiracyfiles-20171218-0001.jpg
    118.6 KB · Views: 1,042
Eti unajiona unapaa utasababisha watu watest aisee [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Vipi madhara ya ugoro?
Ugoro ni kama sigara yaani tobbaco.
tofauti sigara unavuta lakini ugoro unabwia!
tofauti katika madhara hutofatiana
ingawa zote ni nicotine.
Ugoro huwezi kuwa na madhara ya mojakwamoja kama ulivyo ugoro!
ugoro hauna naweza kusema side effect yake labda itachelewa kukufikia mtumiaji ukitofautisha na sigara.
kwa ushauri wangu bora kutumia ugoro kuliko sigara.ila isiwe ugoro wa kihindi kama pariki au manikchand ule unaleta kansa haraka kuliko sigara yenyewe.tumia ugoro wa magadi tu
 
Ugoro ni kama sigara yaani tobbaco.
tofauti sigara unavuta lakini ugoro unabwia!
tofauti katika madhara hutofatiana
ingawa zote ni nicotine.
Ugoro huwezi kuwa na madhara ya mojakwamoja kama ulivyo ugoro!
ugoro hauna naweza kusema side effect yake labda itachelewa kukufikia mtumiaji ukitofautisha na sigara.
kwa ushauri wangu bora kutumia ugoro kuliko sigara.ila isiwe ugoro wa kihindi kama pariki au manikchand ule unaleta kansa haraka kuliko sigara yenyewe.tumia ugoro wa magadi tu
Mkuu nakusii usishauri watu watumie UGORO,
Chondechonde.
 
Back
Top Bottom