Yajue makundi manne ya dawa za kulevya & madhara yake

Yajue makundi manne ya dawa za kulevya & madhara yake

Kemikali yoyote au mchanganyiko ambao huleta mabadiliko ya kihisia na ufahamu ni dawa za kulevya.
Matumizi ya dawa za kulevya huleta utegemezi na usugu.

Utegemezi ni hali ya kushindwa kuishi maisha ya kawaida mpaka utumie dawa ya kulevya. Utegemezi huo huwa wa kisaikolojia na kiafya.

Kuna makundi manne ya dawa za kulevya

1. VIPUMBAZA

Vipumbaza ni aina ya dawa za kulevya ambazo hupunguza kasi ya ufanyaji kazi wa mfumo wa ufahamu. Mfano wa dawa hizi ni;
_ Pombe
_ Heroin
_ Mandrax nk

Unapotumia vipumbaza;
_ Kasi ya ufanyaji kazi wa mfump wa ufahamu hupungua.
_ Mapigo ya moyo hupungua.
_ Shinikink la damu hushuka
sana.
_ Kiwango kidogo huleta furaha
kubwa.
_ Kiwango kikubwa huleta
kizunguzungu, kuongea kwa
kuvuta ulimi, matendo yasiyo
ya busara, kuchanganyikiwa,
ubongo kushindwa kuratibu
mifumo mbalimbali ya mwili.

2. VICHANGAMSHO.

Hizi ni dawa za kulevya zinazoongeza kasi ya ufanyaji kazi wa mfumo wa fahamu.
Mfano wa dawa hizi ni;
_ Mirungi
_ Nicotine
_ Vidonge vya kupunguza hamu
ya kula.
_ Cocaine
_ Caffeine nk
Dawa hizi husababisha yafuatayo;
_ Kuongezeka kwa mapigo ya
moyo.
_ Ubongo kushindwa kuendesha
mifumo ya fahamu.
_ Kutokulala
_ Wasiwasi nk.

3. VILETA NJOZI.

hizi ni aina ya dawa zinazosababisha mtumiaji kuona maono au kusikia vitu visipokuwepo. Mfano wa dawa hizi ni;
_ Bangi
_ Uyoga (peyote, mescaline,
psilocybin)
_ LCD

Unapotumia vileta njozi mambo yafuatayo huonekana;
_ unasikia na kuona vitu
visivyokuwepo.
_ Kujiona unapaa.
_ Kuongezeka ukubwa wa
mboni ya jicho.
_ kubadilisha utambuzi nk

4. VIYEYUSHI.

Aina mbalimbali ya kemikali ambazo mvuke wake huweza kutumika kama kilevi. Mfano wa dawa hizi ni!
_ Petrol
_ Dawa za kuuwa wadudu
_ Dawa za kuondoa rangi za
kucha
_ Dawa za ganzi kama Nitrous
oxide, Propane, butane,
helium nk.

Matumizi ya viyeyushi husababisha yafuatayo;
_ Kuumwa na kichwa
_ Ongezeko ia hisia na
mwanga
_ Kupata njozi
_ Kizunguzungu
_ Mwili kukosa nguvu na hats
kuzimia nk

MADHARA (kijamii)

Watumiaji hukosa busara na umakini maishani hivyo kusababisha;
_ Magomvi na wazazi na
wanandoa.
_ Kushindwa kutunza familia
_ Ujambazi
_ Mauaji ya kikatili
_ Wizi nk

MADHARA (kiuchumi)

_ Kupungua kwa nguvu kazi
kwenye familia na taifa.
_ Kutumika vibaya kwa
rasilimali za familia na taifa
ktk kuwatibu waathirika.
_ Hasara itokanayo na uharibifu
wa Mali unaofanywa na
waathirika (ajali, fujo nk)

MADHARA (kiafya)

Utumiaji wa dawa za kulevya huambatana na matatizo mengi ya kiafya kama;

_ Saratani ya mapafu na damu
_ Kupungua kwa uwezo wa
damu kuchukua hewa (oxygen)
_ Kuharibika kwa mfumo wa
fahamu kunakoambatana na
ukiziwi, kichaa, kupungua
uwezo wa kukumbuka na
kufikiri, luppoza nk.

Pamoja na madhara hayo kwanini watu hawaachi kutumia dawa za kulevya?

Nawasilisha.
 
Acha matusi ya reja reja kwa hiyo tukiwa tunakunywa pombe tunapumbaa

Faida ya pombe ni nyingi kuliko hasara
Kijamii na kiuchumi
 
Acha matusi ya reja reja kwa hiyo tukiwa tunakunywa pombe tunapumbaa

Faida ya pombe ni nyingi kuliko hasara
Kijamii na kiuchumi
Pombe imeathiri watu wengi kiafya, kijamii, na kiuchumi.
Kama ni faida lbd ni kodi inayotozwa na serikali kwa viwanda vya uzalishaji na usambazaji.

Kwa walevi no majanga.
 
Kumbe bangi uleta maono? Safi sanaa na kusikia vitu visivyo sikika na binadam wa kawaida,nataka kuona malaika kwa kupitia bangi na kusikia sauti za mashetani pia
Umesoma madhara yake ??
Usitafute maono kwa kuvuta bangi, hutabaki salama kichwani kama ilivyomfanya mrembo Wema [emoji15] [emoji15] [emoji23] [emoji23]
 
Cannabis au bangi haifanyi mboni ya jicho kuwa kubwa moja na nyingine magic mashroom au uyoga ni dawa nzuri ya depression 100% faster than pharma product imefanyiwa uchunguzi mwaka huu na kuonesha kuwa effective zaidi ya dawa nyingine alafu tunatambua kuwa cannabis au bangi inatambuliwa kwa sasa na WHO kuwa haina madhara kwahiyo ni safe.
 
Nafikiri nahitaji hii kitu mida hii
685e4673a38cba6f45aa0d2aa102f565.jpg
 
Pombe imeathiri watu wengi kiafya, kijamii, na kiuchumi.
Kama ni faida lbd ni kodi inayotozwa na serikali kwa viwanda vya uzalishaji na usambazaji.

Kwa walevi no majanga.
Kila kitu kinaathari mkuu na kikubwa ni kufanya kile kinachokupa furaha na unachokifurahia ili mradi kiwe legal
(Cocaine,heroine na izo mandrax hizi sizisapoti kabisa) at least bangi unakuwa productive

Pombe ina historia kubwa sana katika maisha ya mwanadamu
 
Cannabis au bangi haifanyi mboni ya jicho kuwa kubwa moja na nyingine magic mashroom au uyoga ni dawa nzuri ya depression 100% faster than pharma product imefanyiwa uchunguzi mwaka huu na kuonesha kuwa effective zaidi ya dawa nyingine alafu tunatambua kuwa cannabis au bangi inatambuliwa kwa sasa na WHO kuwa haina madhara kwahiyo ni safe.
Inaitumiaga mkuu?
 
Kila kitu kinaathari mkuu na kikubwa ni kufanya kile kinachokupa furaha na unachokifurahia ili mradi kiwe legal
(Cocaine,heroine na izo mandrax hizi sizisapoti kabisa) at least bangi unakuwa productive

Pombe ina historia kubwa sana katika maisha ya mwanadamu
Kwa hiyo unashauri watu walewe pombo?
 
Back
Top Bottom