Yale matamko ya Ubalozi wa Marekani kuhusu COVID-19 nchini yameishia wapi?

Yale matamko ya Ubalozi wa Marekani kuhusu COVID-19 nchini yameishia wapi?

Kweli kabsa anachosema sicho anachokifanya sasa anajizodoa mwenyewe kila uchao wanarusha picha kuonyesha hicho wanachokiamini nyomi la watu dunia inamuona na kumshangaa umati ule hakuna tahadhari yetote za kiafya zinafuata hata yeye hana mask sasa mwendawazimu sijui ni nani hapo kama si yeye!
Hivi huoni Jana Magu kwenda na maic yake kanisani si strategy ya kujilinda na corona? Wewe puyanga tu tutakufukia
 
Ukiona mzungu Yuko mahali na havai barakoa ujue hakuna Corona,

Angalia juzi Dom mkutano wa TAG.
 
Mungu ni mwema sana katika nchi yetu ya Tanzania. Ametenda na atazidi kutenda hata kwa yale ambayo hatujui.
Mungu kapunguza dharau kwa binadamu wa nchi kama yetu.
Nimejifunza jambo mmoja kubwa kuwa mataifa makubwa yenye tekinologia kubwa yapo mambo hawajui au kizazi hiki kimezembea mambo ya msingi kwa muda mrefu.
 
We unasema marekani, mbona humsemi kigogo aliyefia kutangaza vifo vya ajali za gari ni corona, mpaka kaikimbia akaunti yake kaja na nyingine siku hizi.

Marekani ilikuja kugundua yule balozi mwanamke ni mliberali, wakamfurusha, balozi m republic alipokuja, kasafisha kabisa kuwa Tanzania ni salama na yeye aliingia ikulu bila barakoa
Watz mnajifanya mnajuwa sana,yaani unakuta na mtu mmoja na kwenye chumba ambacho kinaruhusu mkae atleast one mita apart bado unataka avae barakoa,yaani nini hapo?
 
Ukiona mzungu Yuko mahali na havai barakoa ujue hakuna Corona,

Angalia juzi Dom mkutano wa TAG.
Wewe mjinga tu.Una vaa barakoa ukiwa pekee yako au upo na watu wawili watatu na mpo atleast one meter apart unavaa barakoa ya nini?wewe unadhani wazungu wanakariri Mambo Kama wanaccm?
 
Kwa mtu anayechanganua masuala kwa undani utagundua kuwa matamko ya Ubalozi wa Marekani kuhusu kile walichokuwa wanakiita ''Hali mbaya ya maambukizo nchini'' kimepotea baada ya tamko lao la mwisho la mwezi Mei 2020.

Nadhani Ubalozi wa Marekani umegundua kuwa matamko hayo yalikuwa hayaisaidii Marekani kwa sababu walichokuwa wanakisema kilikuwa hakionekani kwenye uhalisia lakini kikubwa zaidi, balozi zingine kama za umoja wa Ulaya zilikuwa kimya.

Matamko ya mara kwa mara ya Ubalozi wa Marekani yalimuibua mwandishi kutoka Uholanzi wa kampuni ya habari, VOICE OF AMERICA aitwaye Ruud Elmendorp kufanya uchunguzi wa kina nchini ili kujua ukweli. Alitembelea mpaka makaburi mbali mbali nchini mara kwa mara hasa yaliyopo Dar es Salaam kuona kama kuna shughuli nyingi za mazishi lakini aligundua hakuna shughuli hizo.

Ukitaka kusoma habari na kuangalia video yake ya Uchunguzi unaweza kugonga LINK hii >>>COVID-19 Diaries: Can Tanzania Really Be Coronavirus-Free?

Kuna msema usemao, ''mficha maradhi kifo humuumbua''. Hii ina maana kuwa kama serikali ya Tanzania ilikuwa inaficha maradhi yatokanayo na COVID-19 basi vifo vya watu wengi vingeiumbua serikali.

Baada ya maambukizi ya COVID-19 kuanza kusambaa kwa kasi katika nchi za Afrika, nchi nyigi za Afrika zilijikuta zikifuata mfumo uliokuwa umependekezwa na WHO katika kukabiliana na janga hili lakini Serikali ya Tanzania iliamua kufuata mfumo tofauti ambao ulizishangaza nchi nyingi duniani lakini pia umesababisha kuzolota zaidi kwa mahusiano ya serikali ya Tanzania na serikali ya Kenya.

Maamuzi ya serikali sio kwamba yalizua mjadala mkubwa na mkali kwa jumuiya za kimataifa peke yake bali pia hata hapa nchini. Jukwaa la Jamiiforums halikubaki nyuma katika mjadala huo ambapo thread hii;

GONGA LINK>>>Janga la COVID-19: Naipongeza Serikali kwa kukataa kuiga baadhi ya mbinu za ’Nchi za Magharibi’ , iliyofunguliwa mwezi wa tatu ilichochea mjadala mkubwa na mkali kuhusu maamuzi ya serikali.

Mwana Jamiiforums Nyani Ngabu alikuwa ni mmoja wa Watanzania wa mwanzo kukubaliana na mtazamo wa Rais Magufuli katika mapambano ya Korona. Mwezi wa tatu alileta mada yenye kichwa cha habari, ''Kirusi kinachotisha kuliko Corona ni uoga/hofu. Baadhi ya wanajamii walipingana naye sana kuhusu mtazamo wake wengine wakimshambulia yeye badala ya hoja yake.

Mada yake hiyo inapatikana hapa, GONGA LINK>>>Kirusi kinachotisha kuliko Corona ni uoga/ hofu

Mwanajamiiforums mwingine Mzee Mwanakijiji alileta pia mada mwezi wa tatu kuhusu kile ambacho alikuwa anakiita maamuzi ya Rais Magufuli kuhusu Corona ni bahati na nasibu lakini akamalizia kwa kuuliza ITALIPA?

Ukitaka kusoma thread hiyo GONGA LINK>>>HOJA NDANI YA HOJA: Rais Magufuli na bahati nasibu ya korona - ITALIPA?

Mijadala hii ilikuwa inakolezwa na matamko yaliyokuwa yanatolewa mara kwa mara na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ambayo yalikuwa yakionyesha ''kuna hali mbaya'' ya maambukizi na vifo nchini.

Kwa sasa imepita miezi 6 tokea mijadala mikali itokee nchini na nje ya nchi kuhusu maamuzi ya Rais Magufuli kuhusiana na korona. Kinachoshangaza kwa sasa hata matamko ya Ubalozi wa Marekani nchini hayatolewi tena na hata wale ambao walikuwa wanakubaliana nayo huku wakimshutumu Rais Magufuli wamebadilisha mwelekeo kimya kimya baada ya kushindwa kupambana na ukweli halisi.

Je, Matamko ya Ubalozi wa Marekani yalikuwa yana malengo gani?

Kama matamko hayo yalikuwa yana malengo, Je, malengo yake yametimia ndio maana hayatolewi tena?

Je, waliokuwa wanakubaliana na matamko ya Ubalozi wa Marekani wamepotelea wapi?
video: Coronavirus in numbers

Coronavirus: Cover-up fears as reviews of Covid-19 deaths among NHS staff to be kept secret

Exclusive: Findings from more than 620 reviews of health and care staff deaths to remain hidden

Shaun LinternHealth Corres
 
Corona imepaishwa sana, hususan huko Marekani.

Na sababu kuu ni uchaguzi wao mkuu wa mwezi Novemba mwaka huu.

Inatumiwa kama fimbo ya kisiasa ya kumchapia Rais Donald Trump.

Ila kwa sasa ninachokiona huko Marekani ni kuna ‘pandemic fatigue’.

Watu wammeanza kuzichoka hizo habari za Corona.

Kama ugonjwa ungekuwa ni hatari kama tulivyoaminishwa, basi sisi tungeathirika kupita maelezo.

Hata huyo Tundu Lissu mwenyewe naona amekubaliana na hali halisi.

Kwenye matembezi yake huko kusaka wadhamini hachukui tahadhari zozote zile zilizopendekezwa na bado anaonekana mzima mwenye afya tele.

Dunia nzima, labda ukitoa Tanzania, imelishwa tango pori.
Wewe unaamini kuwa vifo vinavyosemekana vilitokana na corona USA na duniani kwa ujumla vilikuwa exagarated?
 
Kwa mtu anayechanganua masuala kwa undani utagundua kuwa matamko ya Ubalozi wa Marekani kuhusu kile walichokuwa wanakiita ''Hali mbaya ya maambukizo nchini'' kimepotea baada ya tamko lao la mwisho la mwezi Mei 2020.

Nadhani Ubalozi wa Marekani umegundua kuwa matamko hayo yalikuwa hayaisaidii Marekani kwa sababu walichokuwa wanakisema kilikuwa hakionekani kwenye uhalisia lakini kikubwa zaidi, balozi zingine kama za umoja wa Ulaya zilikuwa kimya.

Matamko ya mara kwa mara ya Ubalozi wa Marekani yalimuibua mwandishi kutoka Uholanzi wa kampuni ya habari, VOICE OF AMERICA aitwaye Ruud Elmendorp kufanya uchunguzi wa kina nchini ili kujua ukweli. Alitembelea mpaka makaburi mbali mbali nchini mara kwa mara hasa yaliyopo Dar es Salaam kuona kama kuna shughuli nyingi za mazishi lakini aligundua hakuna shughuli hizo.

Ukitaka kusoma habari na kuangalia video yake ya Uchunguzi unaweza kugonga LINK hii >>>COVID-19 Diaries: Can Tanzania Really Be Coronavirus-Free?

Kuna msema usemao, ''mficha maradhi kifo humuumbua''. Hii ina maana kuwa kama serikali ya Tanzania ilikuwa inaficha maradhi yatokanayo na COVID-19 basi vifo vya watu wengi vingeiumbua serikali.

Baada ya maambukizi ya COVID-19 kuanza kusambaa kwa kasi katika nchi za Afrika, nchi nyigi za Afrika zilijikuta zikifuata mfumo uliokuwa umependekezwa na WHO katika kukabiliana na janga hili lakini Serikali ya Tanzania iliamua kufuata mfumo tofauti ambao ulizishangaza nchi nyingi duniani lakini pia umesababisha kuzolota zaidi kwa mahusiano ya serikali ya Tanzania na serikali ya Kenya.

Maamuzi ya serikali sio kwamba yalizua mjadala mkubwa na mkali kwa jumuiya za kimataifa peke yake bali pia hata hapa nchini. Jukwaa la Jamiiforums halikubaki nyuma katika mjadala huo ambapo thread hii;

GONGA LINK>>>Janga la COVID-19: Naipongeza Serikali kwa kukataa kuiga baadhi ya mbinu za ’Nchi za Magharibi’ , iliyofunguliwa mwezi wa tatu ilichochea mjadala mkubwa na mkali kuhusu maamuzi ya serikali.

Mwana Jamiiforums Nyani Ngabu alikuwa ni mmoja wa Watanzania wa mwanzo kukubaliana na mtazamo wa Rais Magufuli katika mapambano ya Korona. Mwezi wa tatu alileta mada yenye kichwa cha habari, ''Kirusi kinachotisha kuliko Corona ni uoga/hofu. Baadhi ya wanajamii walipingana naye sana kuhusu mtazamo wake wengine wakimshambulia yeye badala ya hoja yake.

Mada yake hiyo inapatikana hapa, GONGA LINK>>>Kirusi kinachotisha kuliko Corona ni uoga/ hofu

Mwanajamiiforums mwingine Mzee Mwanakijiji alileta pia mada mwezi wa tatu kuhusu kile ambacho alikuwa anakiita maamuzi ya Rais Magufuli kuhusu Corona ni bahati na nasibu lakini akamalizia kwa kuuliza ITALIPA?

Ukitaka kusoma thread hiyo GONGA LINK>>>HOJA NDANI YA HOJA: Rais Magufuli na bahati nasibu ya korona - ITALIPA?

Mijadala hii ilikuwa inakolezwa na matamko yaliyokuwa yanatolewa mara kwa mara na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ambayo yalikuwa yakionyesha ''kuna hali mbaya'' ya maambukizi na vifo nchini.

Kwa sasa imepita miezi 6 tokea mijadala mikali itokee nchini na nje ya nchi kuhusu maamuzi ya Rais Magufuli kuhusiana na korona. Kinachoshangaza kwa sasa hata matamko ya Ubalozi wa Marekani nchini hayatolewi tena na hata wale ambao walikuwa wanakubaliana nayo huku wakimshutumu Rais Magufuli wamebadilisha mwelekeo kimya kimya baada ya kushindwa kupambana na ukweli halisi.

Je, Matamko ya Ubalozi wa Marekani yalikuwa yana malengo gani?

Kama matamko hayo yalikuwa yana malengo, Je, malengo yake yametimia ndio maana hayatolewi tena?

Je, waliokuwa wanakubaliana na matamko ya Ubalozi wa Marekani wamepotelea wapi?
Chadema watapinga! Yule mama rafiki yao alikuwa bure kabisa!
 
Mkuu propaganda zilizidi uhalisia, na kwa bahati mbaya sana baadhi ya wapinzani wakaibeba kama agenda ili kuwalizisha mabwana zao.

Wapiga propaganda wengi walikuwa wanaishia kusema tu Corona ipo ukiwauliza mtaani kwenu kuna wagonjwa wangapi ? Kimya.
 
Siyo rahisi kwa nchi zote duniani ku-exagarate idadi ya vifo. Ingekuwa ni nchi moja tu au chache tu ningeamini. Lakini tatizo limetokea kwenye nchi zote tena zenye kufuata mirengo mbali mbali ya siasa. Kuhusu Tanzania na Magufuli: Ukweli ni kuwa nchi nyingi za kiafrika hazijaathirika sana na hawa virus kama nchi za Ulaya au Amerika hasa kwa upande wa vifo.

Mpaka sasa hatujui sababu ni nini lakini ni lazima ipo/zipo sababu na huenda baadae zikajulikana. Ukichukulia kwa mfano Tanzania, Kenya na Uganda, hizi nchi kuathirika kwake, hasa upande wa vifo, siyo sana japo tofauti ni kuwa Tanzania walifariki watu wengi kwa mpigo kwa sababu hatukuchukuwa hatua zozote na Kenya wanafariki kwa kupishana kwa sababu wamechukuwa hatua.

Kenya sasa hivi idadi ya vifo ndiyo inakaribia 600 wakati Tanzania hii idadi ya vifo tuliivuka zamani na huenda sasa hivi herd immunity inafanya kazi.

Alichafanya Magufuli (kwa ukaidi na kutojua) ni kuachia virus wasambae na wenye bahati mbaya wafe ili waliobaki wapone kitu ambacho sikiafiki kwa sababu bado angeweza kuzuia idadi kubwa ya vifo vilivyotokea hasa baada ya kuhimiza watu wajilundike nyumba za ibada.
Scientists still puzzled by low corona deaths in Africa
 
Mungu katuepusha kwa miujiza

Vifo vilikuwepo si kwa rate ile iliyosemwa.

Nadhan ki uhalisia sio sisi si mabara mengine wanaojua ni why,

Corona ingekuwepo kwa rate ile iliyokuwa inasemwa, maiti zingelala barabarani
Hata juzi tarehe 11.08.2020 USA wametoa warning kwa raia wake kusafiri kwenda nchi za Kenya, Tanzania etc... Hakuna kilichobadilika.
 
Walikuwa wanadanganywa na wanaharakati uchwara baada ya wao kwenda mitaani nakujionea hali halisi wamegundua kuwa walikuwa wanadanganywa na akina Chakaza G Sam Return Of Undertaker huyu G Sam hata matangazo yake ya vifo vya Covid-19 yamebuma na anaumia sana nasikia sasa hivi anaugonywa wa moyo unamsumbua kwa sababu ya stress.

Ndiyo maana Balozi wa US ameletwa mpya baada ya yule wa mwanzo kuonekana amedanganywa sana. Wamepata fundisho kuwa wanaharakati watz ni wapigaji tu.

Pia walidanganywa na Faru John kuwa amevamiwa na kuvunjwa mguu kumbe uongo kwa sasa hawalipuki tena na matamko yao mpaka wachunguze kwanza isjngekuwa hivyo hilo la Lissu huko Hai wangekuwa wameshatoa tamko!
 
Siyo rahisi kwa nchi zote duniani ku-exagarate idadi ya vifo. Ingekuwa ni nchi moja tu au chache tu ningeamini. Lakini tatizo limetokea kwenye nchi zote tena zenye kufuata mirengo mbali mbali ya siasa. Kuhusu Tanzania na Magufuli:...
Acha uongo kawadanganye wanasaccos wenzako huko. Mlipokuwa mnawadanganya USA kuwa hospitali zetu zimezidiwa?

Tena wewe ulikuwa mstari wa mbele kabisa kusema eti tutaisha tunaojitambua tulikuambia uache uongo ukapaniki lakini tukaendelea kukupa vidoge ili upone ugonjwa wako wa slavery mentality.

Eti leo unakuja na kusema nchi za Afrika azijaathirika sana na kwamba idadi ya vifo ya Kenya ni ndogo kuliko ya Tanzania eti tulishapita tayari. Kawadanganye familia yako.
 
Back
Top Bottom