Yale mavitu ya AFCON Morocco, nikiiangalia Tanzania inatia huruma

Vijana wangu, mwanzo mgumu. Ingawa ni kweli miaka ya uhuru haiendani na maendeleo halisi. Na hii yote ni kwa sababu watawala wamewekeza nguvu kubwa kwenye siasa, kuliko maendeleo na mipango miji.
Sisi watu weusi Africa tunaweza kuwa na shida kubwa sana ya kuishi katika utaratibu mzuri wa mpangilio. Kuwa na maendeleo madogo au ya wastani haipaswi kuwa kigezo cha kusindwa kupanga miji vizuri kwa sababu sehemu kubwa ya upangaji miji ni usimamizi wa Sheria na miongozo ya jinsi gani ujenzi ufanyike, barabara tofauti zinapaswa kuwa na ukubwa gani, biashara gani ifanyike wapi n.k
 
Wakienda nje kazi yao kubwa ni kupiga picha na kufanya shopping
Wakirudi huku sasa mipango mingi ya kuongelewa mbele ya waandishi wa habari utekelezaji wake sasa ndio mtihani, baada ya miezi 6 kwisha habari kila kitu kabatini, mimi najiulizaga hata timu za majeshi sikuizi kuzisikia ni kwambali sana, Neti ball toka mashirika kama Bora,THB, NBC,PAMBA MWANZA NK kufa basi kwisha habari kila kitu, kwenye michezo bwana hakuna njia ya mkato ni matayarisho na uwekezaji wa vifaa na wakufunzi bora.
 
Utasikia tupo namba 6 kwa ubora Africa. Tumepeleka timu 4 makundi, Simba namba 5 na takataka zingine. Halafu viwanja ndio hivyo
 
MAMA yetu anatupenda, atarekebisha na Tanzania itakuwa kama Dubai
 
Upo sahihi 100%

Imagine jiji ambalo halina maji wala barabara na uchafu hadi mbele ya mahoteli eti litakuwa mwenyeji wa AFCON.

Kwa East Africa nchi zenye mazingira ya kuandaa AFCON ni Kenya na Rwanda pekee.

Tanzania na Uganda ni rubbish🚮🚮🚮🚮, literally, kama walivyo viongozi wao wauaji
 
Ukipita hapo nnje ya uwanja wa Taifa uone huo ukarabati unaofanyika hapo hutaamini, na wala sijawahi kuona Baraza la michezo la Taifa likiizungumzia hii michuano wala maandalizi zaidi ya porojo kutoka wizarani, hakuna anae zungumzia uhamasishwaji wake ktk utendaji wa mashindano ila utakuja kusikia Ahmed Ally na Ally Kamwe na kisugu na gody yanga ndio wahamasishaji wa Taifa ktk mashindano haya.
 
CCM Chama cha Mataahira
 
Tanzania kila kitu ni kubovu mno, hata hapo Kenya wana nafuu sana. Acheni kujitapa......Tupo nyuma sana. Rais wa ovyo, mawaziri wa ovyo, hawajui kitu. Wewe unafikiri Makonda anafaa kwenye lolote? Majitu mapumbavu, majizi hadi huyo mama lenu.
 
Huwezi kuona aibu kukaribisha ndugu, jamaa na marafiki getoni kisa geto ni duni unalalia maboksi, hakuna masofa ya kukalia wakati mageto ya wasela wengine yamejaza vitu, geto lina thamani ya milioni kumi. Wageni waje tu watakaribishwa na wataambiwa hii ndiyo nchi yetu iko na hali hii myaonayo yaacheni humuhumu. Sisi tutaangalia pichi tu, majengo na barabara watusamehe ndio kwanza tunajitafuta. Sasa kama ule uwanja wa arusha ulioko porini mpaka ujenge majumba na barabara nzuri zikamilike itawezekana vipi kwa muda mfupi uliobaki? Wageni watakula kwenye vibanda vya mama lishe na kulala gesti za wenyeji wanakolala, imetoka hiyo! Bajeti haitoshi kujenga majengo mazuri kuzunguka uwanja na kujenga barabara za kisasa kwenda uwanjani, muda ni mfupi hautoshi kujenga kitongoji/mtaa wa uwanja uonekane kama wa morocco na huko ulaya. Hukohuko porini na mtaa wa mabati chakavu temeke mechi zitachezwa tu. Waleteni wageni wajipigie picha mazingira yetu hatutaona aibu nyumbani kwetu nyumba ni ya udongo juu na chini, ugali bamia
 
Inabidi wageni waje wamefunika pua kama Michael Jackson. Tanzania,Uganda na Kenya ni nchi takataka sana. Hasa hao wawili wa kwanza.
 
Wakati mwingine uwe unafikiri kabla ya kubwabwaja. Moja ya requirement ya kuwa mwandaaji wa hizo tournament lazima kuwe na infrastructures zenye standards, mahoteli ya kutosha, barabara za kutosha, viwanja vizuri na salama n.k. Hayo unayoongea siyo sahihi. Angalia vigezo, hata wakati South Africa wanaandaa kombe la dunia, vigezo vilifuatwa na wakaahidi wanaweza. Simply jibu ni rahisi, kama huna infrastructures za kutosha, mwachie yule mwenye uwezo wa kuandaa, siyo kuleta mambo ya kiswahili. Kuna wengi tu wapo kwenye line wanasubiri na wanaomba waandae.....Siyo lazima muandae ninyi kama hamuwezi. Unashindwa kuelewa nini? Kama huna hoteli za kutosha, wahusika na mashabiki watalala wapi? Ebu wakati mwingine utumie akili kufikiri, mtabaki kuchekwa kwa kufikiria kila jambo kwa Tanzania perspective, fuateni standards....Wengine wetu wapo bado kwenye hangover ya ujamaa. Eti watakula mlenda na ugali.....Ule wewe mwenyewe, hakuna anayekula zaidi yako. Ujinga tu.
 
Mkuu, unamaanisha kwamba hali iliyopo sasa ndio tunashahili kuweponayo?,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…