Dunia nzima imekiri AFCON imepiga hatua kubwa sana. Mbali na soka zuri, Morroco imeweka alama kwenye maandalizi, miundombinu ya soka na nje.
Tazama yale madude, uwanja mkali. Chek picha za nje ya majengo na miundombinu nje ya uwanja.
Kimsingi kitu kizuri huendelezwa kuwa bora zaidi.
Njoo hapa kwetu sasa, utadhani nchi ilikuwa kwenye vita kwa miaka 50. Nimepita hapa Temeke ulipo uwanja mkuu wa nchi- masikini daaah. Kabla hujafika Temeke kwenye soka unapokelewa hapo Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, unajiuliza hii ndio nchi yenye uhuru kwa zaidi ya miaka 60? Ndio nchi tunayoambia mabeberu watatuibia rasilimali?
Njoo sasa Magufuli bus terminal, tujumba kama mahandaki ya vita au wametoka kuchakwazwa na Israel ndio wameanza kujipanga.
Ukiwasikiliza sasa viongozi wetu wakiwa wanasoma karatasi ya maendeleo yetu. Unaweza kusema Morroco waje kujifunza hapa. Kasikilize nwanwa na tantalila za David Kafulila au Kitila Mkumbo-ujanja ujanja tu na takwimu za kubumba.
Naamini timu zote zikija hapa zitakiri zenyewe, kama hawa jamaa hawakujinda walituleta kutafuta nini huku?!
Ushauri
Serikali itenge fungu la bajeti za kuficha taswira ya nchi. Media zipewe fungu zisirushe picha za nje ya uwanja, humo Magomeni, Ubungo, Kinondoni wasifike