Yaleyale yaliyojitokeza kwa Alikiba, Darassa, Aslay, Mavoko, n.k, ndiyo yanataka kujitokeza kwa Harmonize.

kifimbocheza_

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2017
Posts
1,119
Reaction score
1,095
Asalaam Alykuum wakubwa.

Kumekuwa na kasumba moja kwenye kiwanda cha mziki wa bongo flava, kuwa pale inapotekea msanii akawa na spot light kubwa anaanza kupambanishwa na Diamond haijalishi huyo msanii yupo upande gani
Diamond amekuwa kama ndo S.I Unit ya mziki wa bongo flava kuwa kila msanii lazima alinganishwe naye na kupambanishwa iwe kwa heri au kwa shari. Nikikumbuka kipindi Alikiba anafanya come back kwenye sanaa kuliibuka makundi mawili moja likimshabikia huyu jingine yule. Team zilikuwa kubwa sana ikawa Alikiba na Diamond.

Nakumbuka tena kipindi Darassa anaachia mikwaju ya maana kama ngoma yake pendwa ya mziki watu walianza kumfananisha na diamond akaonekana ni bora kuliko diamond mpaka yeye akaonekana upepo kuanza kumpitia akajaa ichwa baada ya hapo imebaki historia tu siyo tena yule Darasa wa mziki na wale watu hawana mda naye tena washamsahau
.
Aslay naye vile vile watu walimvimbisha kichwa na kupewa tambo kuwa yeye ni mkali kuliko Diamond ikapelekea kujiita nguvu ya Umma but kila mtu anajua Aslay siyo yule tena na wale watu awaliomvimbisha kichwa hawana time naye tena ile nguvu ya Umma haipo tena.

Walewale waliojifnya wanamshabikia Alikiba, Darassa, Aslay, ndio hao hao waliomrubuni Rich Mavoko kuwa WCB inamnyonya na yeye ni mkubwa kuliko Diamond so hawezi kuwa chini yake hii ikampelekea Mavoko ajitoe WCB kwa mbwembwe kubwa lakini sasa hawana time naye anaachia ngoma kila iitwapo leo lakini zote ziiiii.

Sasa hivi upepo umerudi kwa Harmonize wanamjaza kuwa ashakuwa mkubwa so kuendelea kuwa chini ya Diamond ni kuendelea kunyonywa, bora ajitoe aanze kijisimamia yeye kama yeye. Bila kusahau kuwa ndio hawa hawa.Dimond alikuza kipaji chake , lakini kwa sasa wamegeuza kibao wanamuona Harmonize ndio mkali hata Dimond hamfikii. kwani Kwa sasa ameshakuwa mkubwa basi haina haja ya kuendelea Kuwa chini ya WCB
.
Upepo huu naona kama ushaanza kumjaa mdogo wangu Harmonize anaonekana kujitenga sana crew ya wasafi anajion
a ashakuwa mkubwa. Nikuhakikishie Harmonize hawa wanaokujaza kichwa hawakutakii mema na siku ukijitoa wasafi baada ya miezi kadhaa hutowasikia tena watahamia kwa msanii mwingne na kuanza kukuponda.

Diamond ni msanii pendwa na anayo maadui wengi na mashabiki wengi sana so hao maadui ndo hutafuta kila mbinu ya kumwngusha ndio, maana kila leo wanakuja na mbinu tofauti tofauti ili tu, kum-frustrate bwana mdogo ila yeye ashaamua kukaza ndio maana mpaka leo yupo hapo. Acha kusikiliza huu upepo maana ni wa mda tu, kumbuka Domo kakutoa wapi kakupiganiaje mpk leo upo hapo. Ukitaka kujua hilo kaangalie upya interview yako ulofanya mara ya kwanza na Millard Ayo itakupa funzo upya. Usipelekwe na huu upepo wa mda ambao baadaye utakugeuka.
 
Ushauri mzuri sana huu

Ila kwa Rich Mavoko sijui alifeli wapi alikuwa msanii bora angepambana kiume kama kina Joh Makini, Nikki wa pili etc etc ila sijui uwoga ulimkuta wapi akaamua kujiunga Wasafi sasa ametoka mambo bado atafute meneja mzuri atatoboa tu rich mavoko
 
Mara mia asingejiunga WCB.
 
Joh makini na nikki wa pili ni wasanii wa nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…