Shadeeya
JF-Expert Member
- Mar 12, 2014
- 49,759
- 118,798
🙈🙈🙈
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
🙈🙈🙈
Kumekucha.
Kwenye droo ya jana,tumeona Simba itakavyopambana na Tout Puissant Mazembe.
Kwakweli sote tunajua historia ya Tout Puissant, ni timu ambayo ina rekodi nzuri sana kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika. Waswahili wa bara wanasema historia haidanganyi. Lakini kiuhalisia sio kila historia itazungumza ukweli wa baadae. Muda ndiyo hakimu wa Haki.
Hata hivyo Kumekuwa na vigelegele vingi mtaani juu ya mageuzi ya soka kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ambayo SSC imeweza kuyaonesha, hili ni jambo zuri lakini ni wakati sasa wa kuutazama ukweli kwa Big Picture na kuacha Fantasy zote behind.
----------------------------
UKWELI MCHUNGU KUHUSU SIMBA.
Tumeona jinsi ambavyo simba ilivyopoteza michezo yote ya ugenini. Ni kipigo baada ya kipigo na kufanya jumla magoli kuwa 12 kwa ugenini tu. Simba imeonesha uwezo wa chini sana kwa mechi za ugenini na kitu kikubwa ambacho tumekiona ni wachezaji kushindwa kujiamini wakiwa ugenini.
Na hili linaonekana hata kocha ameshindwa kulipatia ufumbuzi tatizo hili.
Inasikitisha sana kuona wachezaji wanategemea kushinda nyumbani tu, na kuwa kikapu cha mipira ugenini. Tuliona JS Saoura alivyomdindia As Vita pale Kongo na kufungana 2-2, huu ndiyo mpira, mchagua jembe si mkulima.
Tout Puissant ni timu yenye wachezaji wazuri, kasi nguvu na akili en plus Expérience ya michuano hii. Nimesema tunaacha fantasy zote na kuuangalia ukweli uliyo Uchi.
Simba ikicheza na Tout Puissant kama ilivyocheza na Vita ugenini au JS Saoura kule Algérie basi tutegemee kadhaa na aibu kubwa kwa kasi na uchu wa kombe walionao
Tout Puissant.
Simba itaweza kupigwa goli hata kumi kule kongo ikiwa haitobadilika. Huyu kocha wa sasa hajawahi kueleweka kwa mechi zake za ugenini na ikumbukwe kwamba round hii unatakiwa kubalance kati ya ugenini na nyumbani ili uweze kufanikiwa.
Simba itaweza kubadili matokeo na kuandika Historia mpya ikiwa,
1. Atapatikana mwana saikolojia ili awaandae wachezaji kisaikolojia kwamba wanauwezo wa kufanya lolote.
2. Kocha aangalie formula ambayo itazaa goli ugenini, ni lazima kushinda angalau goli ugenini hata akifungwa but awe na goli la ugenini. Formula alizotumia zote kwenye makundi hajafanikiwa kupata goli ugenini hata moja. This is BS.
3. Wachezaji ambao hawana experience na michuano ya kimataifa wasipangwe. Goli ambalo Chama alilifunga linahitaji utulivu wa akili na confidence kubwa kwa dakika kama zile, lakini mtoto Chama alitulia na akaweka mpira wavuni, kwa wachezaji wetu ambao hawana experience wangepaisha juu. Chama huyu huyu ndiyo aliyeipeleka Simba kwenye makundi kwa dakika zilezile. Experience Matters a lot.
4, Mo anatakiwa kusajili wachezaji sio chini ya watatu ambao ni pure international wenye sifa na experience nzuri kimataifa kwa ajili ya michuano ya kimataifa inayokuja. Tumeona faida ya Chama kwenye game zenye namba tasa.
Ninaamini wachezaji wazuri hawawezi kukataa kwa sababu tayari Simba imejiweka kwa position nzuri kimataifa. Kwa muktadha huo timu itaweza kufika mpaka fainali na kutoa fursa kwa klabu nyingine nyumbani.
Imefika wakati sasa tuwekeze kwenye soka.
Tofauti na hapo, Mtaka nyingi nasaba, hupata mwingi msiba
Tout Puissant- Nguvu kama Zote.
Thursday 21, March 2019.
-----------------
MK54
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]Porojo tupu.
Waacheni vijana wa Simba wakifanya even mambo yao na wataalam wao.
Hatua waliyopo ni nzuri sana na hakuna cha mazembe wala mazombe.
Sijawahi kuona Mkenya akiitakia mema Tanzania.
Vyura safari hii hamuambulii kitu mtatoka patupu,sanasana mtaambulia majungu cup! winner.Na ww upo kwenye kapu la Simba!!?
subirini kichapo kikali kutoka kwa hao unaowaita mazombi
Mna kelele nyingi hatukai mjini tukatulia kila kona kelele zenu maninaVyura safari hii hamuambulii kitu mtatoka patupu,sanasana mtaambulia majungu cup! winner.
Sent using Jamii Forums mobile app
Azam NI nyutro (hatuna upande) ...lakini ;;Binamu mungekuwa nyie mungetupa hiyo sapoti?
Kuna mashabiki, wapenzi na wadau wa mpira, kutokana na bandiko la jamaa nadhani mashabiki hawawezi kumuelewa huyu jamaa.japokuwa mimi ni mshabiki dam dam wa simba naomba... nikupongeze kwa andiko hili pure profesional na kwa kuonyesha hauko kishabiki ukaweka na mikakati mizuri kwa mpangilio ulioeleweka ....namini watauona huu uzi.....
ukweli mchungu naombeni maji
Punguza ukilaza wewe,kwani timu ikisema inaenda kucheza defensive approach INA maana MTU akipata nafasi ya kufunga atarudisha mpira nyuma kwa kipa wake??Plan ni kuongeza nguvu ya ziada ktk hiko ulichokipanga!!Hivyo Simba waliamua kuongeza nguvu ya ziada ktk mechi za nyumbani,na wenzetu wamefanikiwa kwa plan hizihizi,Al Ahly bingwa Mara 8 kafungwa ugenini Mara 35,kashinda chache sana.Zote hizo ni plans tu ndugu.Kwahiyo plan ilikuwa kushinda game zote za home, na kufungwa zote za ugenini, is that what you mean ?
Wenye macho wameona na kusikia, wewe endeleza ubishi.
Hii ni sms kwa SSC, kama inakuumiza, pole.
But game za ugenini timu ilifungwa kwa poor performance na kwa taarifa yako nilikuwa uwanjani katika mji wa Bechar kule Algeria, niliona magoli yote.
Tout Puissant ni timu ngumu lakini itafungika endapo simba itabadili mtazamo.
Hizo ngonjera tulizisikia tokea mwezi wa 12 mwaka jana. Mtabadilisha santuri sana. Hiyo mnayotumia imechubuka.Mwisho mwezi ujao 😎😎
Punguza ukilaza wewe,kwani timu ikisema inaenda kucheza defensive approach INA maana MTU akipata nafasi ya kufunga atarudisha mpira nyuma kwa kipa wake??Plan ni kuongeza nguvu ya ziada ktk hiko ulichokipanga!!Hivyo Simba waliamua kuongeza nguvu ya ziada ktk mechi za nyumbani,na wenzetu wamefanikiwa kwa plan hizihizi,Al Ahly bingwa Mara 8 kafungwa ugenini Mara 35,kashinda chache sana.Zote hizo ni plans tu ndugu.
Na kuhusu kufungwa unataka kusema Barcelona walipanga kufungwa 4-0 na PSG kule Paris??hakuna MTU anayepanga akafungwe.Ila MTU huchagua kuelekeza nguvu zaidi wapi na kwa sababu gani.
Umeshaambiwa approach ya knockout stage ni tofauti na league.Umeshaambiwa alichofanya Simba dhidi ya Mbabane na Nkana ugenini,yote Yale ni matokeo ya Plan and Approach.
Hata Hivyo umezungumza point nzuri tu,tatizo unachanganya na uchura ndani yake ndio maana tunakushambulia,tunashambulia uchura wako sio point zako
Sent using Jamii Forums mobile app
Kesho Simba tuna mechi,karibu hiyo kwanza tutamalizia na ya jumamosiTukutane Taifa Jumamosi.
Baada ya mechi ya marudiano na Mazembe nitarudi katika Uzi wako
Historia ya As Vita umeimaliza kabla ya kufuatilia ya mazembeFuatilia Historia ya Tout Puisant na fuatilia historia ya nyie kucheza ugenini.