Yaliyofichika kwenye Mti wa Krismas, usithubutu kuununua

Yaliyofichika kwenye Mti wa Krismas, usithubutu kuununua

Mti ulio bora wa Krismasi unanunuliwa. Ukipambwa kwa madoido yenye kung’ara pamoja na kumetameta, unasimamishwa karibu na dirisha. Maduka yanajazana wanunuzi wakisaka zawadi na vile viduchu vinasubiri kwa hamu kubwa ya Baba Krismasi Santa.

Ni mshughuliko na ni homa ya Krismasi 'Christmas fever, umewahi kufikiri kabla? Je, Biblia au Yesu aliwahipo kusababisha homa ya Krismasi?

Je, Krismasi Ina Ushahidi wa Biblia?

Neno ‘Krismasi’ halipo ndani ya Biblia. Biblia ilifunga midomo ya sherehe yote inayohusiana na Krismasi, isipokuwa kwa kitu kimoja; upambaji wa mti. Biblia wYenyewe inashutumu upambaji wa miti (ya Krismasi):

“Mila za watu si chochote, wanakata mti kutokana na msitu, na mchongaji anauchonga kwa patasi yake, wanaupamba kwa fedha na dhahabu, wanaugandanisha kwa nyundo na misumari ili usipate kutikisika” (Jeremia 10-3,4).

Wazungu wa ki-Pagani kabla ya Ukristo, waliamini miujiza kwamba miti ya kijani ina nguvu maalum za ulinzi. Hakika, matumizi ya Miti ya Krismasi imeanza hivi karibuni tu mwa karne ya 17 huko Strasbourg, Ufaransa na kutoka huko ukaenea hadi Ujerumani, Uingereza na baadaye Marekani.

“Ibada ya miti ilikuwa ni jambo la kawaida kwa dini miongoni mwa watu wa (Teutonic) na Scandinavia wa Ulaya ya kaskazini kabla ya kuingia kwenye Ukristo…

Walowezi wa ki-Jerumani walileta mila za Mti wa Krismasi kwenye makoloni ya Kimarekani mnamo karne ya 17. Kufikia karne ya 19, matumizi yake yalienea sehemu tofauti”.

Usinunue mti wa Krismasi unafifiza imani kwa familia yako na watoto wako, mti huo unabeba roho za kipagani.

View attachment 2850683
😂Hivi we ni dini gani
 
Imani yako ya kishirikina, mti una ubaya gani? Waafrika kuwaza uchawi tuu.
 
20231223_104133.jpg
 
Una hakika umeshamaliza kuelimisha wati wa dini yako mkuu,kwanini usiwaache wenye dini yao wapate raha kama ambavyo huwa unapata raha maulid?
 
Tabia za KU GOOGLE na kuamini ulicho gogo opo siku utakuwa Gwajoma. Gwaji ali gogo makala iliosema KORONA ni 5 G hivyo watu wasitumie 5G kumbe ulikuwa ujinga uliowekwa mitandaoni , Yeye akauchukua na kuanza kuuhubiri ule ujinga. Mda ni msema ukweli wote tunajua Gwajima alihubiri ujinga na hupokewa na wajinga kirahisi kwa sababu hawana uwezo wa kupima ukweli.
Wewe umetumia kipimo gani kupima kushuka kwa imani kwenye familia ?. Miti yenyewe mingine imeundwa kwa plastic how can a plastic absorve your spiritual power . Yaani lotoi wewe unaliogopa,
duniani humu!
 
ahhh naona mti huu unakuumiza sana.brother usiumie sana hizi ni bwembwe tu za sherehe.
Mjinga huyo hayo mapambo tu ya sherehe

Kama yakivyo mapambo mengine.Mtu anafanya birthday au kuoa au kuolewa ukumbi hupambwa

Sasa hizo sherehe za kibinaadamu unapamwa ukumbi sembuse sehemu ya kumbukumbu ya kuzaliwa Yesu iwe kanisani au popote. YESU ni Mheshimiwa sehemu ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake lazima ipambwe iwe kwa maua au Christmas tree nk

Maua na miti yote ni Mali ya Mungu sio shetani au wapagani.Mleta maada ana pepo mchafu anaamini kuna miti ya shetani au wapagani hivyo haitakiwi kutumika kupambwa kanisani Shetani na wapagani hawajawahi umba mti wowote ukiwemo mti wa Krismasi .Christmas Tree mwenye hati miliki nao ni Mungu sio wapagani au Shetani hivyo waweza tumika kanisani kama pambo siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa Yesu

Shida mleta mada kajazwa ujinga na kidini chake kuwa kuna mimea au miti ni mali za shetani au wapagani akasome kitabu cha mwanzo Mungu ndie aliyeumba miti yote ikiwem o Christmas tree .Miungu haikuumba hiyo miti na haina mamlaka ya kuibinafsisha kuifanya ya kwao yenyewe kama miungu au wafuasi wa hiyo.miungu wawe wapagani au mleta mada
 
Back
Top Bottom