Mkuu Chuakacha, pole kwa kuumizwa na jibu langu, ila kiukweli mimi natoka Kanda ya Ziwa, kabila langu ndilo kabila linaloongoza kwa kupenda wanawake na kupenda watoto, haijalishi ni watoto wako au ni wakusaidiwa, kwa sababu tuna wanawake wengi, na watoto wengi, na hatumaindi kusaidiwa, ila watoto wote ni wetu na tunawapenda!.
Mimi mwenyewe japo naishi Bongo, wife wangu anaishi US, mimi na wife wangu wote ni weusi, ila mmoja wa kabinti kangu kalichozaliwa US ni keupe kutokana na hali ya hewa ya kule!, kabinti haka ndio my favorite kid!, hivyo usimaind sana comments zangu, zingatia tuu hoja zangu za msingi!.
Watanzania tumejaaliwa fursa kibao nchini mwetu, ila sisi ni wavivu, kuanzia kufikiri hadi kutenda!, tunapenda sana kulala tuu bila kufanya kitu, wakitokea wageni kuchangamkia fursa badala ya kushukuru, wamekuja kufanya kile sisi tulichoshindwa, tunaishia kulalamika na kuwalalamikia!, na tukiachiwa kufanya, tunaishia kushindwa!.
Fanya kazi, get rich, or die trying!.
Paskali