Chabruma
JF-Expert Member
- Sep 19, 2013
- 5,660
- 1,780
Wadau mpooooo? Kama kawaida nianze kwa kuwatakia kila la kheri na shughuli zenu za kila siku na nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia afya njema siku ya leo. Wale wagonjwa kama kawaida yetu tuendelee kumwomba Mwenyezi Mungu ili awaponye haraka. Wale waliotangulia mbele ya haki tumuombe Mwenyezi Mungu awaondolee adhabu za kaburi na awaandalie makazi mema huko waendako.
Wadau, baada ya jana Mheshimiwa Sammuel John Sitta kushinda kwa kishindo katika kinyang'anyiro cha nafasi ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum baada ya kupata kura 487 na kumshinda kwa mbali mpinzani wake Hashim Rungwe aliyepata kura 69, leo ni uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti. Kwa mujibu wa kanuni, kwa vile Mwenyekiti ametoka Tanzania Bara, Kinyang'anyiro cha Makamu Mwenyekiti kitakuwa ni kwa Wazanzibari pekee. Aidha, kwa mujibu wa Makubaliano yaliyofikiwa pale mjengoni, kwa vile Mwenyekiti ni mwanaume wa kutoka Tanzania Bara, Makamu Mwenyekiti atakuwa mwanamke kutoka Zanzibar. Hii ni kusema kuwa uchaguzi wa leo watu wenye sifa ya kugombea kwa mujibu wa kanuni na makubaliano ni wabunge wanawake kutoka Zanzibar.
Mpaka sasa, bado sijapata orodha ya wabunge waliochukua fomu, nitaendelea kufuatilia na nikipata taarifa za uhakika nitawajuza. Ila katika pitapita yangu, nimekutana jina la Samiha Sululu kama sijakosema. Jina hili ndo linatajwa sana kuwa ndiye atakayekuwa Makamu Mwenyekiti. Sitashangaa kusikia hapo baadaye kuwa ni mgombea pekee aliyechukua fomu na kukidhi vigezo na hivyo kutumia kura ya Ndiyo (kura ya wazi) kumpitisha.
Kama ilivyo ada, natarajia kuungana na wadau wengi katika tukio hili. Kwa sasa wapo wengi ambao ni vigumu kuwataja wakiongozwa na Mkuu Skype, kbm, Mkuu ya Kaya, Pasco, Deo Corleone, OKWI BOBAN SUNZU, Simiyu Yetu na wengine wengi ambao mniwie radhi kwa kutowataja. Kwa sasa tuendelee kufuatilia maoni ya wadau juu ya ushindi wa Sitta huku tukitafakari majukumu yaliyo mbele yake. Kama kawaida Mods wataendelea kuweka mambo sawa ili wadau wapate mtiririko ulio sawia. Hadi hapo baadaye, Stay Connected."
================================================================
UPDATES 1
Wadau, taarifa ambazo nilizipata mapema leo ni kuwa hadi muda wa kurejesha fomu unamalizika, kulikuwa na wanawake wawili ambao walikuwa wamechukua fomu za kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum. Wagombea hao ni Samia Suluhu wa na Amina Abdallah Amour. Bado naendelea kusaka taarifa ili kujua kama wamerejesha ndani ya muda uliopangwa na wamekidhi vigezo. Ila kwa sasa tujue tu kuwa mtifuano hapo baadaye ni kati ya Samiha Suluhu wa CCM na Amina Ally wa CUF.
UPDATES 2
matokeo yanatangazwa kama ifuatavyo;
Idadi ya wabunge wote ni 629
Waliopiga kura ni. 523
Kura zilizoharibika ni. 7
Amina Abdallah Amour. 126 (24.1%)
Samia Hassan Suluhu. 390 (74.6%)
Kwa matokeo hayo, Samia Suluhu Hassan ametangazwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum