kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,677
Mkuu kbm​ nimekupata. Karibu sana leo
swaiba yako "Simiyu Yetu" yuko wapi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu kbm​ nimekupata. Karibu sana leo
Mkuu nimeshajongea twende pamoja mpaka ukumbini tutakuwa wote wala usijali tupo bega kwa bega na chabruma na wengine kibao.swaiba yako "Simiyu Yetu" yuko wapi?
Amani kwako mkuu chabruma kumeshakucha salama japo kwa sasa dodoma kamvua cha kiaina kipo ila kazi inafanyika tupo pamoja mkuu.
Nafahamu kuwa bavicha wengi mnanigwaya na kunichukia kwa kuwapa ukweli ntaendelea kuwagonga za uso sana bavicha wote mtaipata tu mwaka huu kazi imeshaanza jana tumempata mzee wa viwango leo tutampata samia kila kitu kinakuwa ok.Sitapenda kusoma updates za Simiyu Yao!! Maana huyo jamaa ameharibiwa na magamba. Sijui ndo ID anayoingia nayo Mkwe.re?!!
Habari njema mkuu nimechelewa kidogo kuingia jukwaani siunajua vikao vya mikakati dodoma vingi kweli ila sasa mambo yako vema tunakwenda kumchagua samia mkuu.Muheshimiwa Simiyu, habari yako bana!
Ha ha ha ha ha ha ha! Kwa niaba yake tafadhali pamoja sana.Chabruma unahitajika eneo hili, tafadhali jitokeze.
Nategemea kuwaona skype,chabruma na mkuu wa kaya mwanzo mwisho,pamoja sana.Wadau mpooooo? Kama kawaida nianze kwa kuwatakia kila la kheri na shughuli zenu za kila siku na nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia afya njema siku ya leo. Wale wagonjwa kama kawaida yetu tuendelee kumwomba Mwenyezi Mungu ili awaponye haraka. Wale waliotangulia mbele ya haki tumuombe Mwenyezi Mungu awaondolee adhabu za kaburi na awaandalie makazi mema huko waendako.
Wadau, baada ya jana Mheshimiwa Sammuel John Sitta kushinda kwa kishindo katika kinyang'anyiro cha nafasi ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum baada ya kupata kura 487 na kumshinda kwa mbali mpinzani wake Hashim Rungwe aliyepata kura 69, leo ni uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti. Kwa mujibu wa kanuni, kwa vile Mwenyekiti ametoka Tanzania Bara, Kinyang'anyiro cha Makamu Mwenyekiti kitakuwa ni kwa Wazanzibari pekee. Aidha, kwa mujibu wa Makubaliano yaliyofikiwa pale mjengoni, kwa vile Mwenyekiti ni mwanaume wa kutoka Tanzania Bara, Makamu Mwenyekiti atakuwa mwanamke kutoka Zanzibar. Hii ni kusema kuwa uchaguzi wa leo watu wenye sifa ya kugombea kwa mujibu wa kanuni na makubaliano ni wabunge wanawake kutoka Zanzibar.
Mpaka sasa, bado sijapata orodha ya wabunge waliochukua fomu, nitaendelea kufuatilia na nikipata taarifa za uhakika nitawajuza. Ila katika pitapita yangu, nimekutana jina la Samiha Sululu kama sijakosema. Jina hili ndo linatajwa sana kuwa ndiye atakayekuwa Makamu Mwenyekiti. Sitashangaa kusikia hapo baadaye kuwa ni mgombea pekee aliyechukua fomu na kukidhi vigezo na hivyo kutumia kura ya Ndiyo (kura ya wazi) kumpitisha.
Kama ilivyo ada, natarajia kuungana na wadau wengi katika tukio hili. Kwa sasa wapo wengi ambao ni vigumu kuwataja wakiongozwa na Mkuu Skype, Mkuu ya Kaya, Pasco, Deo Corleone, OKWI BOBAN SUNZU, Simiyu Yetu na wengine wengi ambao mniwie radhi kwa kutowataja. Kwa sasa tuendelee kufuatilia maoni ya wadau juu ya ushindi wa Sitta huku tukitafakari majukumu yaliyo mbele yake. Kama kawaida Mods wataendelea kuweka mambo sawa ili wadau wapate mtiririko ulio sawia. Hadi hapo baadaye, Stay Connected.
Habari njema mkuu nimechelewa kidogo kuingia jukwaani siunajua vikao vya mikakati dodoma vingi kweli ila sasa mambo yako vema tunakwenda kumchagua samia mkuu.
mungu akupe afya ili twende pamoja mkuu.
Habari njema mkuu nimechelewa kidogo kuingia jukwaani siunajua vikao vya mikakati dodoma vingi kweli ila sasa mambo yako vema tunakwenda kumchagua samia mkuu.
mungu akupe afya ili twende pamoja mkuu.
Sitapenda kusoma updates za Simiyu Yao!! Maana huyo jamaa ameharibiwa na magamba. Sijui ndo ID anayoingia nayo Mkwe.re?!!
habari zenu wooote wana jf humu jukwaani,
naombeni mnijuze kikao leo kitaanza mda gani?? na ni lini mheshimiwa sitta ataanza majukumu yake rasmi ya kuliongoza bunge la katiba???
Lakini muheshimiwa kwa nini unapenda kubishana sana na watu wanakwenda kinyume na itikadi zako? Huoni kua unajishushia hadhi? Nadhani ungejaribu kuiga busara za mzee Kificho au una maoni gani?
Hapana mkuu unanisingizia mimi na wakwere wapi na wapi.Wewe humjui dada Simiyu Yetu, sisi tunamjua ila siyo ID mkwer.e
Mkuu nashukuru kwa ushauri ngoja niachane nao make wanapenda uchokozi usio na maana.Lakini muheshimiwa kwa nini unapenda kubishana sana na watu wanakwenda kinyume na itikadi zako? Huoni kua unajishushia hadhi? Nadhani ungejaribu kuiga busara za mzee Kificho au una maoni gani?