Mzee wa ngano
Senior Member
- May 3, 2012
- 184
- 54
Kikao cha bunge leo asubuhi kimeisha saa 4; 23, ambapo wamezipitisha kanuni za kuliongoza bunge hilo baada ya kumenyana kwa siku 21.
Kabla ya kuahirishwa kwa kikao hicho, Mch. Mtikila alitoa malalamiko yake kwa kuongea bila kurusiwa kuwa kwanini tangu jana anaomba kuongea hapewi nafasi ambapo mwenyekiti huyo wa muda alidai kuwa muda hautoshi kuwaruhusu wote walioomba kuongea kupewa nafasi.
Mimi nakaa najiuliza inakuwaje aseme muda hautoshi wakati leo hawakuwa na shughuli nyingine zaidi ya hiyo na ndiyo maana kaahirisha kikao kabla ya muda? Kwani angempa Mtikila muda aongee na hao wengine aliodai kuwanyima nafasi halafu wamalize saa saba mchana kama ilivyo kawaida yao ingeathiri nini? Au kuna jambo jingine nyuma ya pazia?