Yaliyojiri Bungeni Dodoma: Jumanne, Tarehe 11 Machi 2014

Yaliyojiri Bungeni Dodoma: Jumanne, Tarehe 11 Machi 2014

Kikao cha bunge leo asubuhi kimeisha saa 4; 23, ambapo wamezipitisha kanuni za kuliongoza bunge hilo baada ya kumenyana kwa siku 21.

Kabla ya kuahirishwa kwa kikao hicho, Mch. Mtikila alitoa malalamiko yake kwa kuongea bila kurusiwa kuwa kwanini tangu jana anaomba kuongea hapewi nafasi ambapo mwenyekiti huyo wa muda alidai kuwa muda hautoshi kuwaruhusu wote walioomba kuongea kupewa nafasi.

Mimi nakaa najiuliza inakuwaje aseme muda hautoshi wakati leo hawakuwa na shughuli nyingine zaidi ya hiyo na ndiyo maana kaahirisha kikao kabla ya muda? Kwani angempa Mtikila muda aongee na hao wengine aliodai kuwanyima nafasi halafu wamalize saa saba mchana kama ilivyo kawaida yao ingeathiri nini? Au kuna jambo jingine nyuma ya pazia?
 
Huu ni mchakato wa kutengeneza katiba ya kikundi fulani, kasoro kama hizi ndiyzo zitasababisha kupatikana kwa katiba mbovu isiyo na sura ya kitaifa.
 
Mkuu, Ole Sendeka hajambo na amejaa tele. Ile kanuni ya upigaji kura ilishapita baada ya kufanyika marekebisho kidogo. Kwamba badala ya kusema kuwa maamuzi yataamuliwa kwa kura ya siri, imeandikwa kuwa yataamuliwa kwa kupiga kura ambayo itaamuliwa na Bunge amaalum. Ni hayo tu mkuu

Mkuu Chabruma, Kama wamepitisha kanuni hizo bila ya kuamua namna gani kura itapigwa, nafikiri wameahirisha tatizo tu. Ni muhimu saana kanuni zingeweka wazi kuwa : Maamuzi yataamuliwa kwa kupiga kura ya siri (au wazi) kulingana na makubaliano kuliko hivi walivyoiacha. Kimsingi nafikiri kama wameshndwa kuamua juu ya suala hili basi sheria iliyoanzisha bunge la katiba inatakiwa ifuatwe ambako imeeleza kuwa kura ya siri ndio itatumika.
 
Kwa hiyo hapo kesho, kura za kumchagua Mwenyekiti wa Kudumu wa Bungela la Katiba zitakuwa za dhahiri au za kificho?
 
Kwa hiyo hapo kesho, kura za kumchagua Mwenyekiti wa Kudumu wa Bungela la Katiba zitakuwa za dhahiri au za kificho?

Kwa kurejea namna alivyochaguliwa kificho ndivyo atakavyochaguliwa mwenyekiti wa kudumu kesho yaani kwa kura ya SIRI.
 
Atleast mesesi imemfikia walengwa,kwamba upendeleo hautakiwi
 
Si kila mtu ambaye tabia yake mbaya anaweza kuicha., Pandu Kificho ametoa nafasi kwa makundi mbali mbali kulingana na uwiano wa watu 600 waliomo bungeni ili kuweza kuunga mkono azimio la kanuni., makundi yote wameridhika sasa porojo la nini? ivi watu 600 wangepewa nafasi wote waunge mkono au kukataa unafkiri ingechukua miaka mingapi?
 
Mods
Nawashukuru kwa kuunganisha uzi huu hapa sikutembelea jukwaa hili kabla ya ku post.

Together we Can.
Long live JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Kwa hiyo hapo kesho, kura za kumchagua Mwenyekiti wa Kudumu wa Bungela la Katiba zitakuwa za dhahiri au za kificho?

Bila shaka zitakua za ''kificho'' kama alivyochaguliwa KIFICHO.
 
Mtikila leo asubuhi wakati wa kupitisha kanuni za Bunge maalum asimama na kumtaka M/kiti wa muda Bunge maalum la katiba,A.Kificho ampe nafasi ya kusema.Amwambia anambagua,hamtendei haki.
 
Mjumbe wa bunge malumu la katiba mh mtikila amemlalamikia mwenyekiti wa bunge malumu kuwa ateki haki ya kusikiliza wajumbe wote amesema haki ya kusikilizwa ni haki yake ya msingi
 
kwa hiyo mwenyekiti wa bunge la katiba kesho atachaguliwa kwa kura ya wazi?
 
Back
Top Bottom