Yaliyojiri Bungeni Dodoma: Jumatatu, Tarehe 10 Machi 2014

Lakini siamini kama kule ndani kuna mtoto
 
Chabruma nipe update toka hapo mjengoni maana kuna tafrani imezuka ghafla hapo na watu wa tv wamekata sauti ghafla, nisaidie kwa hili ili tupate mtiririko mzuri.
 
Last edited by a moderator:
Wanabodi,

Mwenyekiti wa muda wa Bunge maalum la Katiba anataka kuhairisha kikao kwani rasimu haijatimia, wajumbe wengi hadi ilipofika saa kumi kamili viti vingi vilikuwa wazi

Mkuu hapo kwenye neno "rasimu" badilisha weka neno "akidi"

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Hapo hakuna kitu ndugu yangu, walio wengi hawana nia na katiba mpya bali wanataka chama chao kiendelee kubaki madarakani. Yote yanayoendelea hapo hayanishangazi kwani nilipoona CCM wamejazana humo kwenye bunge hili hali hii niliitarajia. Nchi zetu nyingi za kiafrika ni ngumu kuandika katiba ya wote bila kwanza kutokea machafuko haswa kama chama kinachotawala ni kikongwa kwenye nchi hiyo.
 
Je mtoto mdogo amefikaje kwenye bunge maalumu la katiba? Je wabunge wanaona muhimu wa kuwapo hapo bungeni kwa masilahi ya Watanzania?
 
Kikao kimeahirishwa hadi Saa kumi na mbili jioni
 
Chabruma nipe update toka hapo mjengoni maana kuna tafrani imezuka ghafla hapo na watu wa tv wamekata sauti ghafla, nisaidie kwa hili ili tupate mtiririko mzuri.
Mkuu, James Mbatia alikuwa anaomba muongozo kuwa mpaka sasa hawajagawiwa kanuni. Hivyo akawa anahoji wataridhia vipi azimio la Kanuni wakati kanuni zenyewe hawana. mwenyekiti akamjibu kuwa Kanuni zilichelewq kufika na awali alitaka bunge liahirishwe kwa dakika kadhaa ili kusubiri kanuni hizo na hatimaye kugawiwa. Ila wabunge wakazomea. Baada ya maneno hayo ya Mwenyekiti, Mkosamali akasimama na kulalamika iweje Mbatia apewe muda wa kuongea na yeye amenyimwa? Ndipo kejeli za maneno zilipoanza wengi wakimuita Mkosamali kwa maneno ya kejeli
 
Kikao kimehairishwa hadi saa 12 jioni........kazi ipo
 
Kikao kiahirishwa kwa muda hadi saa kumi na mbili kamili, sababu ni kukosekana kwa nakala za kutosha za kanuni kwa wajumbe wote, aaaa hahahahaaaaa hili bunge hili?
 
naona wamearisha bunge mpaka saa kumi na mbili
 
Wahafidhina vs wazalendo,kazi kubwa mh kificho amesema urudufishaji wa kanuni bado haujakamilika mpaka muda huo utakua umekamilika.hivyo bunge litaendelea.mimi naona leo zitapigwa
 
Nashauri waajiriwe na walipwe mshahara kama wafanyakazi wa serikali ambaye hataki aachie wengine.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…