Yaliyojiri Bungeni Dodoma: Jumatatu, Tarehe 10 Machi 2014

Yaliyojiri Bungeni Dodoma: Jumatatu, Tarehe 10 Machi 2014

Kukosekana kwa rasimu ya kanuni za Bunge la Katiba kumemfanya Mwenyekiti wa Bunge hilo Pandu Ameir Kificho kuliahirisha hadi saa 12 jioni hii hv jamani ni kweli mchana ule mpaka saa kumi na moja walishindwa kutowa copy ya hizo rasimu?akiyamungu huu ni mchezo tunachezewa waTZ mweshimiwa rais okoa kodi zetu mapema ni maoni yangu.


Yani Mi cjui wanataka kufanya nini hata! Serikali legelege ndiyo faida yake hii!
 
Kura ya siri ni lazima liwe na lisiwe lazima Kanuni itamke kura ya siri. Duniani kote kura ya siri ndiyo inayotumika hata kumchagua Mwenyekiti wa Kitongoji. Hata Mhe. Mwenyekiti wa Bunge Maalum, Wahe. Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wasituletee vurugu zisizofaa hata kidogo. KURA YA SIRI NI LAZIMA.

Onyesha wapi wanapitisha katiba kwa kura ya siri.kwa kuwa wewe ni mtaaalamu wa uzoefu duniani geogle us congress votes database uone jinsi wenzako wanavyoweka kumbukmbu ya upigaji kura wa kila mbunge.huwezi kutetea ulaghai huu wa kura za siri.
 
Wadau, amani iwe nanyi.

Kama kawaida yetu tutaendelea kuwaletea mtiririko wa mijadala Bungeni Dodoma. Kwa sasa Bunge lipo kwenye mchakato wa kukamilisha kupitisha vifungu vya Kanuni za Bunge. Mtakumbuka kuwa vifungu vyote 87 vimepitishwa isipokuwa kifungu cha 37 na 38 ambavyo kwa ujumla wake vinahusu ufanywaji wa maamuzi ndani ya Bunge Maalum. Mjadala hapa ni ama matumizi ya Kura ya Wazi au ya Siri. Mtakumbuka kuwa siku ya Ijumaa ya tarehe 7 Machi, Mwenyekiti Kificho aliunda Kamati ya Mashauriano kuhusu vipengele hivyo. Kamati bado haijamaliza kazi yake na leo wanaendelea na mashauriano. Semina kwa siku ya leo itaendelea kuanzia saa 5 Asubuhi mara baada ya Kamati ya Mashauriano kumaliza kazi yake.

kama kawaida, nitakuwa sambamba na wadau wengine kuwaletea updates zote. Natarajia kupata ushirikiano kutoka kwa mdau wetu ambaye ni Mbunge wa Bunge hili Maalum, Simiyu Yetu. Pia kwenye Mjadala, natarajia kuwaona akina Skype na MaishaPesa. ​Stay Connected

======================================================================================
UPDATES 1

Wadau, semina imechelewa kuanza kwa vile Kamati ya Mashauriano ilikuwa inaendelea na kikao chake. Kwa sasa kikao kimemalizika na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo akiwemo James Mbatia, Steven Wasira, Askofu Donald Mtetemela na Sheikh Jongo wameingia Ukumbini. Ni wazi kuwa muda si mrefu Semina itaanza. Tuwe na subira

UPDATES 2
Bunge limeahirishwa hadi saa 10 jioni ambapo wwbunge wataridhia Rasimu ya Kanuni hizo baada ya zoezi la kuzipitisha kukamilika

UPDQTES 3
Wabunge wameanza kuingia abungeni tayari kwa kuanza kikao cha Kupitisha Rasimu ya Kanuni.
attachment.php
attachment.php



UPDATES 4
Mwenyekiti ameingia ukumbini huku idadi kubwa ya wabunge hawapo ukumbini kama picha hiyo hapo chini inavyoonekana
attachment.php


UPDATES 5
Bunge limesimama kwa muda ili kusubiri wabunge wengi waingie ukumbini. Wakati huo huo Rasimu ya Kanuni zinagawiwa kwa wabunge.

UPDATES 6
Bunge limeahirishwa mpaka saa 12 jioni kutokana na zoezi la kudurufu Kanuni za Bunge kutokamilika

hivi jamani mbona maandalizi ya bunge hili yupo rejareja sana, mbona hatuko serious na mambo muhimu kila wakati kuhairisha tutafika?
 
Tanganyika halisi na ni muumini wa serikali 3, yaani 1 ya Tanganyika, nyingine ya Zanzibar na ya 3 ni ya shirikisho la hizi mbili.

Tumeingia kwenye mchakato huu KATIBA MPYA wakati wenzetu Zanzibar tayari ni NCHI. Kazi ipo.
 
Tumeingia kwenye mchakato huu KATIBA MPYA wakati wenzetu Zanzibar tayari ni NCHI. Kazi ipo.

Hata sisi ni nchi, sema uchama ndo unatuponza na baadhi ya watu kama pinda wanaoukana uraia wao hadharani
 
Jaman mashine za kutoleo photocopy za bungen zimefanyeje wadau? Coz nashindwa kuwaelewa, au rim papers hamna?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Umeme wametukatia huku jaman, yaan hii nchi kila sekta inaulemavu wake wa asil.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Inanavyoonekana ccm hawataki katiba mpya, ushauri wangu...CCM Hakuna haja ya kumaliza kodi za watanzania chamsingi rudini kwenye majimbo yenu na muwaambie watz kuwa CCM HATUTAKI KATIBA MPYA
1.INAWABANA WATOTO WETU WASIJE KUWA WATAWALA
2.UWAZIRI WA KUTEULIWA NI MTAAMU SANA KULIKO WA KUGOMBANIA
3.HII NCHI NI YA CCM TU HAKUNA CHAMA AMBACHO KITATAWALA, KWANI HIKI CHAMA KIMETOKA KWA MUNGU.
4. n.k
 
hivi jamani mbona maandalizi ya bunge hili yupo rejareja sana, mbona hatuko serious na mambo muhimu kila wakati kuhairisha tutafika?

Wasomi wa Tanzania hata ukiwaambia wakupe mbinu ya kudhibiti nywele zisirefuke zaidi ya kitana wataunda kamati ya wiki 2 ili waje na jawabu la 'kisomi' mradi kila mtu ana hoja na inaweza kuandikwa ripoti yenye kurasa 300 eti kwa vile tu mwanasheria mkuu aliwahi kusema "kichwa kazi yake si kufugia nywele tu"Kodi zetu wajinga ni chakula chenu wasomi kuleni tu lakini jueni mkizoea kula, nanyi siku moja mtaliwa maana "Ukitaka kula lazima nawe uliwe"HE JK

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Wadau, zikiwa zimebakia dakika tano, wabunge wengi wanaingia ukumbini tayari kwa shughuli iliyo mbele yao
 
Chabruma Chabruma, unanipata mkuu? muda umetimu, hebu niambie nini kinaendelea hapo kwa sasa
 
Last edited by a moderator:
Ninahisi ikifika hiyo saa kumi na mbili kikao kitagubikwa na vurugu hatimaye kuahirishwa hadi kesho.
 
Sasa watapiga kura gani kuamua kama wawe wanapiga kura za wazi au za siri?
 
Mwwnyekiti ameingia ukumbini na sasa yupo kwenye kiti chake
 
Back
Top Bottom