Yaliyojiri Bungeni Dodoma: Jumatatu, Tarehe 10 Machi 2014

Lipumba anataka wajumbe wapewe muda hadi kesho saa tatu asubuhi ili wapitie nakala za kanuni walizopewa ili kuona kama inashabihiana na yale waliyokubaliana
 
Lipumba anapendekeza wajumbe wapate fursa ya kuzisoma....ili kesho liitwe bunge la katiba na sio semina....kikao kinaelekea kuahirishwa
 
Kama nilivyotangulia kusema lipumba kazunguka weeeeee kisha kasema bunge liahirishwe hadi kesho saa 3 asubuhi
 
Mbowe nae yaleyale, tuahirishe bunge eti tukapitie kanuni, aaaaaagh kero tupu
 
Mbowe naye anaongea. Anasema kuwa pamoja na kuiamini kamati, anaunga hoja ya alipumba ya kuahirisha Bunge hadi kesho saa 3 Asubuhi. Sasa anakaribishwa Vuai Ali Vuai. Naye anaungana na Lipumba
 
Vuai Ali vuai nae anapendekeza yale yale ya mbowe na Lipumba
 
Aiseeee hawa wanasiasa hawa!!!!!!!!!!!!!!!!!! jamani kodi ni mzigo ujue? sasa imebaki kazi moja tu huku mtaani, siisemi maana niakua traced kwa IP Address yangu
 
Mbowe nae yaleyale, tuahirishe bunge eti tukapitie kanuni, aaaaaagh kero tupu
Mkuu, pamoja na hayo, ila wana hoja ya muhimu hapa. Lengo ni kila mmoja aridhike na kile kilichomo kwenye Kanuni. Si unajua hawa jamaa hawaaminiani?
 
Kama nilivyotangulia kusema lipumba kazunguka weeeeee kisha kasema bunge liahirishwe hadi kesho saa 3 asubuhi
Kificho anarudia majina yaleyale. Lipumba, Mbowe, Vuai, Mbatia,..., anazingatia mno majina maarufu utadhani anapanga timu ya mpira ambayo akina Messi na Ronaldo hawawezi kukosekana!
 
Mimi nishaondoka kwenye tv saa nyingi napata ka lite kabaridi tu
 
Mbatia nae walewale anaunga mkono hoja ya lipumba na mbowe, tayari wametafuna laki tatu zangu hapo.
 
Mbatia nae anasema hoja ya kuahirisha semina ni muhimu....ili wajumbe wakapitie kanuni hizo
 
kuna uwezekano bunge likaarishwa mpaka kesho
 
Hivi kwa nini wajumbe wasio wabunge mbona hawapewi nafasi hata kidogo?
 
Vuai Ali vuai nae anapendekeza yale yale ya mbowe na Lipumba
Mkuu, hawa wote wanaoongea ni wajumbe wa Kamati ya Mashauriano. Wanayoongea ndiyo waliyokubaliana. Sitegemei kuona usaliti. Ila wasiwasi wangu ni nini kitajitokeza iwapo itabainika kuwa kuna dosari kwenye hizo Kanuni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…