wewekussa
Member
- Mar 8, 2014
- 59
- 8
Wadau, amani iwe nanyi.
Kama kawaida yetu tutaendelea kuwaletea mtiririko wa mijadala Bungeni Dodoma. Kwa sasa Bunge lipo kwenye mchakato wa kukamilisha kupitisha vifungu vya Kanuni za Bunge. Mtakumbuka kuwa vifungu vyote 87 vimepitishwa isipokuwa kifungu cha 37 na 38 ambavyo kwa ujumla wake vinahusu ufanywaji wa maamuzi ndani ya Bunge Maalum. Mjadala hapa ni ama matumizi ya Kura ya Wazi au ya Siri. Mtakumbuka kuwa siku ya Ijumaa ya tarehe 7 Machi, Mwenyekiti Kificho aliunda Kamati ya Mashauriano kuhusu vipengele hivyo. Kamati bado haijamaliza kazi yake na leo wanaendelea na mashauriano. Semina kwa siku ya leo itaendelea kuanzia saa 5 Asubuhi mara baada ya Kamati ya Mashauriano kumaliza kazi yake.
kama kawaida, nitakuwa sambamba na wadau wengine kuwaletea updates zote. Natarajia kupata ushirikiano kutoka kwa mdau wetu ambaye ni Mbunge wa Bunge hili Maalum, Simiyu Yetu. Pia kwenye Mjadala, natarajia kuwaona akina Skype na MaishaPesa. ​Stay Connected
======================================================================================
UPDATES 1
Wadau, semina imechelewa kuanza kwa vile Kamati ya Mashauriano ilikuwa inaendelea na kikao chake. Kwa sasa kikao kimemalizika na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo akiwemo James Mbatia, Steven Wasira, Askofu Donald Mtetemela na Sheikh Jongo wameingia Ukumbini. Ni wazi kuwa muda si mrefu Semina itaanza. Tuwe na subira
ok poa kaka