Yaliyojiri Bungeni Dodoma: Jumatatu, Tarehe 10 Machi 2014

Yaliyojiri Bungeni Dodoma: Jumatatu, Tarehe 10 Machi 2014

Wadau, amani iwe nanyi.

Kama kawaida yetu tutaendelea kuwaletea mtiririko wa mijadala Bungeni Dodoma. Kwa sasa Bunge lipo kwenye mchakato wa kukamilisha kupitisha vifungu vya Kanuni za Bunge. Mtakumbuka kuwa vifungu vyote 87 vimepitishwa isipokuwa kifungu cha 37 na 38 ambavyo kwa ujumla wake vinahusu ufanywaji wa maamuzi ndani ya Bunge Maalum. Mjadala hapa ni ama matumizi ya Kura ya Wazi au ya Siri. Mtakumbuka kuwa siku ya Ijumaa ya tarehe 7 Machi, Mwenyekiti Kificho aliunda Kamati ya Mashauriano kuhusu vipengele hivyo. Kamati bado haijamaliza kazi yake na leo wanaendelea na mashauriano. Semina kwa siku ya leo itaendelea kuanzia saa 5 Asubuhi mara baada ya Kamati ya Mashauriano kumaliza kazi yake.

kama kawaida, nitakuwa sambamba na wadau wengine kuwaletea updates zote. Natarajia kupata ushirikiano kutoka kwa mdau wetu ambaye ni Mbunge wa Bunge hili Maalum, Simiyu Yetu. Pia kwenye Mjadala, natarajia kuwaona akina Skype na MaishaPesa. ​Stay Connected

======================================================================================
UPDATES 1

Wadau, semina imechelewa kuanza kwa vile Kamati ya Mashauriano ilikuwa inaendelea na kikao chake. Kwa sasa kikao kimemalizika na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo akiwemo James Mbatia, Steven Wasira, Askofu Donald Mtetemela na Sheikh Jongo wameingia Ukumbini. Ni wazi kuwa muda si mrefu Semina itaanza. Tuwe na subira

ok poa kaka
 
Mkuu, nakubaliana na wewe kabisa. Ila katika suala la katiba, misimamo ya kichama si muhimu. Muhimu hapa ni maridhiano

Mkuu ni kweli maridhiano yanatakiwa lakini
Hivi mnaweza kuridhiana ili kuvunja sheria?
Maoni yaliyopo kwenye tume ni maoni ya
Wananchi ambayo kimsingi yameshakuwa sheria
Sasa siyatekelezwe tu mashauriano ya nini
Mbona wananchi hawahusishwi kwenye hayo
Mashauriano?
 
Mwalimu Ezekiel Oluoch anapendekeza ipigwe kura ya Siri ili kuamua aina ya kura inayotakiwa.
 
Oluwoch anatoa ushauri kua wapige kura kuamua aina ya kura itakayotumika kwa kua kamati ya maridhiano wameshindwa kuamua, anaiomba sekretarieti iandae karatasi wapige kura, full stop.
 
mbona wabunge wa ccm hawataki kura ya siri kuna nn kimejificha
 
Mwl Oluochi anadai ipigwe kura ya siri kuamua kura ya maamuzi itakuaje
 
Haya hali imeanza kuchafuka, wajumbe wanaropoka ovyo hapa
 
Mwenyekiti anapangua hoja ya mjumbe aliyependekeza bunge lisimame hadi muafaka ufike kuepusha kutafunwa kodi zetu. Mwenyekiti anasema haiwezekani kwa kua eti rais alilifungua

Mwenyekiti ajamuelewa kafulila! Kafulila anamaana Kuwait semina ivunjwe sio bunge!!
 
Kuna mwanamke mjumbe analazimisha kura ya wazi, amezomewa
 
kwa kweli kuna watu hawako serious.na.hawaonei watanzania wa.hali.ya chini huruma....wagonjwa hawana.madawa...watoto wanakaa chini...walimu hawajalipwa malimbikizo.yao ....
halafu wao.wanaleta huu upumbavu wa.kukutana kwa dakika.15 kisha bunge.liahirishwe?......iwekwe kanunu pia wasipokutana kwa.masaa minimum nane.kwa siku kwa.kazi.waliyotumwa na watanzania wasipewe posho ya siku hiyo uone kama wataendelea tena.na.huu utoto
 
Huyu mama mjtmbe analazimisha kura ya wazi eti kwa madai kua wananchi tumekubali, aaa aisee!
 
Tanzania ni nchi ya ajabu sana has a ccm kwani kama wanachosimamia kina maslahi si wawape Uhuru watu wafanye bila kulindwa kama Obama
 
Mng'ong'o anadai kamati ya maridhiano ipewe muda.pia anadai wananchi wanataka kura ya wazi
 
Kuna mbunge anasema kuwa wazo la Oluoch ni jema ila lina tatizo pia. Badala ya kutumia kura ya siri kuamua aina ya kura itakayotumika, mbunge anapendekeza ipigwe kura ya wazi kuamua ama kura ya wazi au ya Siri itumike
 
Back
Top Bottom