Elections 2015 Yaliyojiri Chato: Mkutano wa Mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA/UKAWA, Edward Lowassa

Elections 2015 Yaliyojiri Chato: Mkutano wa Mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA/UKAWA, Edward Lowassa

Angeandika mtu mwingine ningetafakari kidogo lakini wewe kiazi mmalangu huna kitu.

Hiki alichokiweka mleta mada kinaendana na hizi picha je ni kweli mleta mada KIAZI au ni wewe ndio KIAZI?
chato.jpg

chato3.jpg

chato2.jpg
 
AZAM tv imewahoji waakazi wa Geita njiani kuhudhuria mkutano wa Lowassa, wote wamekiponda chama cha CCM hasa issue ya maji na wachimbaji wadogo wadogo. Mabadiliko lazima.
 
Hapa wote tuna akili, hivi kweli mnamsikia Lowasa akiongea? Kweli kila mtu anaweza patwa na chochote na hujafa umeumbika, kweli Lowasa anaweza kuongea jamani, mimi namkubali sana lakin naona kama jamani hebu tuwe fair kwa nchi yetu labda kama ni wasaidizi tu wataendesha nchi. Hakuna mtu anamweza kufurahia kuona mwenzake anaumwa lakin honestly anahitaji mapumziko. Nimesikiliza akiongea Geita there is nothing unaweza kusikia. Namuombea Mungu ampe afya njema InshaAllah.

Ajuwaye mungu kwa mgonjwa kuwa mzima na mzima kuwa mgonjwa na hakuna binadamu anayeijua kesho
 
Mnatupigia propaganda humu ndani kumbe jamaa kashindwa kuongea bana, kisa mike hazisikiki vizuri. Lisu kaahidi watarudi tena wakiwawamejiandaa vizuri UKAWA kazi mnayo mwaka huu CDM chama nichokipenda kinakwenda kupotea kwenye ramabi za siasa hivihivi....

Yah ccm inatoweka hivi hivi daaah
 
Nyie jamani msipende kudanganywa na maccm, hebu Magufuli aitishe walau mikutano miwili tuu na waambiwe watu hakuta kuwa na wasanii ndio mtauona mziki wake ulivyo mgumu. Mikutano yote ya CCM inaonekana na watu wengi ni kwa vile kuna wasanii basi. Hiyo ndio sababu CCM iko tayari kuwalipa kiwango chochote wasanii ili kuficha aibu.
Hali halisi bila wasanii ni kama hivi
https://www.facebook.com/peter.datti/posts/1667488713467547
 
Alipindisha lami kupeleka nyumbani kwao,walivyo hoji,akawambia kama mnataka lami,tandaza kinyesi barabarani mpite,eneo lile walimnyima kura wakati anagombea ubunge!
 
Hapa wote tuna akili, hivi kweli mnamsikia Lowasa akiongea? Kweli kila mtu anaweza patwa na chochote na hujafa umeumbika, kweli Lowasa anaweza kuongea jamani, mimi namkubali sana lakin naona kama jamani hebu tuwe fair kwa nchi yetu labda kama ni wasaidizi tu wataendesha nchi. Hakuna mtu anamweza kufurahia kuona mwenzake anaumwa lakin honestly anahitaji mapumziko. Nimesikiliza akiongea Geita there is nothing unaweza kusikia. Namuombea Mungu ampe afya njema InshaAllah.

Mgonjwa wa leo ndio mzima wa kesho,mzima wa leo marehemu wa kesho,jamani nauliza,hivi Mwaisapile alikuwa anatibu maradhi gani?JPM alionekana akipata dozi ya kikombe.
 
Geita mjini ijapo mheshimiwa amefika mda unaelekea kwisha, lakini umati wa wapenda mabadiliko waliokuwa wamekusanyika pale uwanja wa magereza ni hatari kweli alivyosema si mapenzi ni mahaba
 
CCM ikishindwa inabidi wamlaumu mtunzi wa huu wimbo wa CCM ni ile ile. Sasa kama ni ile ile haiwezi kushinda maana matatizo yatakuwa ni yale yale, kweli mwaka huu CCM mtaisoma namba:A S-frusty:
 
Kitu kilichonipa ghadhabu ni kuona watu wa Kigoma mjini wakipiga kelele ya kutaka huduma ya maji yaani sijui lini hali itakua sawa kama mpaka leo huduma muhimu kama maji bado ni kero ya jumla na kila wakija hawa wakoloni weusi wanatoa ahadi wanapotea.
 
Back
Top Bottom