Elections 2015 Yaliyojiri Chato: Mkutano wa Mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA/UKAWA, Edward Lowassa

Elections 2015 Yaliyojiri Chato: Mkutano wa Mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA/UKAWA, Edward Lowassa

MAKAMBA:LOWASA ALIFUKUZWA KAZI,
HAKUJIUZULU!
Katibu mkuu mstaafu wa CCM luteni mst Yussuf Makamba amesema kuwa aliyekua Waziri Mkuu Edward Ngoyai Lowasa alikua ameshafukuzwa kazi kabla ya kujiuzulu.
Makamba ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara wa kampeni za Urais za CCM katika kiwanja cha Kawawa mjini Kigoma.
Akifafanua suala hilo mzee Makamba amesema kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM katika kikao kilichokaa mjini Dodoma, baada ya kuridhika kuwa Lowasa alihusika na kashfa ya Richmond,iliteua watu watatu kwenda kumuona Rais Kikwete kumueleza kuwa kwa maslahi ya nchi na chama amfute kazi Waziri Mkuu wake Edward Lowasa kwakua kamati ya uongozi imeridhika kuwa alimuita na kashfa ya Richmond na kulifedhehesha taifa.
Watu hao watatu walikua katibu mkuu wa CCM wakati huo mzee Makamba, mzee Samuel Malecela na mama Anna Abdallah.
"Tulipofika kwa Rais Kikwete tulikutana na Lowasa nje akitokea ndani kwa Rais, tukaingia na kumkuta bwana mkubwa. Tukapewa kahawa. Kisha tukamueleza kuwa tumetumwa na kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM kuwa Waziri mkuu amehusika na kashfa ya Richmond na kwa heshima ya CCM na taifa amfukuze kazi.
Rais Kikwete akatuuliza,
...hamjakutana nae hapo nje?
Tukajibu...tumekutana nae anatoka...
Akasema...nimekwisha kumwambia kuwa kwa heshima ya taifa na CCM hawezi kuendelea kuwa waziri mkuu tena na kwamba nateua waziri mkuu mwingine...
Makamba alisema kuwa baada ya Rais kumfukuza kazi Lowasa, kesho yake asubuhi Lowasa aliamkia bungeni na alipopewa nafasi ya kujitetea alisema tatizo nu uwaziri mkuu na kwamba amemuandikia barua Rais aachie ngazi.
"Ukweli ni kwamba Rais alishamfukuza kazi Lowasa usiku wa kuamkia siku aliyotangaza kiachia ngazi na kujiuzulu. Lakini tuliamua kumsitiri. Sasa kwakua kaamua kusema, nasi tumekuja kueleza akiba tuliyoweka."

Na Mwandishi wetu,
Kigoma
Hilo sisi halituhusu wala hatuna ubishi nalo. Unaweza kumwacha mkeo mimi nikamuoa na akawa mke bora kabisa labda ulikuwa unanfuja je. Rasi mwaka huu upende usipende ni Lowasa. CCM tumeichokaaa........!!
 
Muelezeni January Makamba na Nape Nnauye wayaone hayo mafuriko nyumbani kwa Magufuli. Kwa kweli nimefurahi na hayo mafuriko kwao Magufuli. Someni ubao wa Buziku. Kama ni kweli hayo maneno hayastahili kutamkwa na mtu mzito kama Magufuli.
 
Geita mjini ijapo mheshimiwa amefika mda unaelekea kwisha, lakini umati wa wapenda mabadiliko waliokuwa wamekusanyika pale uwanja wa magereza ni hatari kweli alivyosema si mapenzi ni mahaba

hakuna wa kumzuia Lowassa kuingia magogoni Oktoba.
 
Lowasa ni mwanga,na kwa kawaida giza haliwezi kushinda mwanga
 
Hatuitaji mtu anayeongea kama kameza cd alafu mwisho wa miaka mitano anaogopa hata kupita mitaa aliyopiga kampeni maana hana alichotekeleza. Uliza meli za ziwa victoria ziko wapi.

Atakuwa ndio rais wa kwanza duniani asiyejua kuongea,yaani mnataka kutuuzia mbuzi kwenye gunia hivihivi!!!
 
Picha mkubwa, maneno hayavunji mfupa

hivi ww unafikiri Magufuli anaweza kujaza watu bila DIAMOND, ALLY KIBA, THE COMEDY, YAMOTO BAND, FUTUI NAKINA WEMA?????MAGUFULI ni saiz ya LISSU, ZITTO , JJ MNYIKA.

LOWASSA ni habari nyingine.
 
Kauli za Magufuli kwa Watanzania wenye shida:-

CHATO KWAO:- Kunyeni barabarani msambaze kinyesi kiwe lami!


CHATO KWAO:- Kojoeni mkojo wenu mtumie kama mnashida ya maji.


KIGAMBONI:- Kuvuka kivukoni , pegini mbizi.
 
Ukitaka kujuwa Magufuli ni mzigo kwa Ccm ni mkutano Lowassa aliofanya Chato leo.
Watu hawamtaki magufuli kila mtu lowassa na mabadiliko.
Ina maana kama Lowassa amepata ushindi mkubwa namna hii nyumbani kwa Pombe nani tena wakumzuia asiingie ikulu.

nawashauri CCM wasitishe kampeni zao wasiendelee kupoteza fedha zao tiyari Rais wa JMT kupitia UKAWA Mhe Lowassa ameshapatikana anasubiri kuapishwa tu.
 
Kama jimboni kwake hakuna maji ilhali serikali ni YAO na wanapendeleana majimbo yao. Kweli sifuri kabisa.

Juzi anaahidi watu wa Tabora kuwa atayafungia maji ya mto Malagarasi na kuyaelekezea bwawani kisha yapelekwe Tabora. Hivi mawazo hayo ya kisiasa yanazingatia kwamba mto ni kitu cha asili na kila unapopita kuna uoto na viumbe hai ambavyo vitakufa ikiwa mkondo wa mto utahamishwa?

Hii ni FUTUHI na mchekeshaji wetu ni WA KUKURUPUKA
 
Atakuwa ndio rais wa kwanza duniani asiyejua kuongea,yaani mnataka kutuuzia mbuzi kwenye gunia hivihivi!!!

Kwani huyo anayeyoka hajuo kuongea? Na ndiyo katifikisha hapa. Haya huyo anaepiga kampeni mpaka sasa tarehe ya leo aliyoyasema ahadi zake hawezi kutekeleza. Wa nini sasa. Bora akae kimya tuu maana anaongea sasa kama mpinzani.
 
Back
Top Bottom