johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Watu ni wengi wengi, wengi sana na wamekaa kwa utulivu kabisa wakiwa na huzuni isiyo mfano.
Kadhalika viongozi mbalimbali wako uwanjani tayari kutoa heshima za mwisho.
Updates;
Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wameshaketi katika sehemu walizopangwa na sasa wanasubiriwa viongozi wakuu wa kitaifa.
Kadhalika wakuu wa mikoa wote wameshaketi sehemu zao.
Mwili wa hayati Magufuli umeshaondolewa nyumbani na wakati wowote kuanzia sasa utawasili kiwanjani!
Msafara wenye mwili wa hayati Magufuli ndio unawasili hapa uwanjani!
Sasa unapigwa wimbo wa taifa na watu wote wamesimama wakiongozwa na waziri mkuu!
Ni muda wa viongozi wa dini kusoma dua
Ameanza padre wa Kanisa Katoliki amefuatia shehe wa Bakwata, kisha mchungaji kutoka CCT na mwisho mchungaji kutoka Pentecoste.
Sasa anaongea waziri kutoka ofisi ya makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar ambaye ni mjumbe wa kamati ya mazishi.
=====
MAKAMU WA PILI WA ZANZIBAR AONGOZA KUAGA MWILI WA DKT. MAGUFULI
Makamu wa Pili wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdullah ameongoza shughuli ya kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dkt. John Magufuli katika Uwanja wa Magufuli, Wilaya ya Chato Mkoani Geita
Katika hotuba yake, amesema hakuna mahali ambapo Hayati Dkt. Magufuli hakuacha alama huku akitaja baadhi ya sekta kuwa miundombinu ya barabara, Afya, Shule na ukusanyaji mapato
Amewaomba Watanzania kuendelea kushikamana katika kujenga Taifa akieleza tayari Dkt. Magufuli ameonesha njia, ameacha Taifa likiwa salama na lenye heshima kubwa
Wakazi wa Chato watatoa heshima zao za mwisho, na gari halitozungushwa uwanjani hapo kama ilivyokuwa baadhi ya maeneo mengine