Yaliyojiri European Champions League : Tottenham 0 - Ajax 1 (Semi Finals First Leg)

Yaliyojiri European Champions League : Tottenham 0 - Ajax 1 (Semi Finals First Leg)

Wa usiku huu naaaaah
Jumatano leo ndio itakuwa bombaaa.. kunoga
 
Ajax wakifanikiwa kutinga fainali basi watakuwa wameungana na kaka khaswa baba zao akina Rijkaard, adger davids, Danny Blind ,tijan babangida, kanu na wengine sikuwataja ambao misimu miwili ya 95 na 96 waliweza kushinda taji hilo mwaka 95 baada ya kupata bao la jioni la Patrick Kluivert akiwa bado mbichi miaka 19 tu na kupeleka furaha katika jiji la Amsterdam. Mwaka uliofuatia walitinga pia ila bahati haikuwa yao baada ya kutolewa kwa changamoto ya mikwaju ya penalty dhidi ya kibibi kizee cha turin kilichokuwa na captain gianluca vialli na fabricios ravaneli (babu mamvi ).Kwa ujumla ajax mpira wao wanaujua wenyewe wamekutana na juventus na madrid na kuweza kushinda tena ugenini sio timu ya kubeza.
 
Hawa Tottenham wamekuwa wakishinda kingekewa-ngekewa tu ila kiukweli mpira wao bado. Pochettino uwezo wake umefikia kilele na sidhani kama wanaweza kucheza fainali.
 
Back
Top Bottom