Yaliyojiri katika Chaguzi Ndogo: Uchaguzi wa ubunge jimbo la Dimani na madiwani Tanzania Bara

Míe nasema 2020 vyama vyote vya siasa vianze kuweka msimamo sasa hivi kwamba hawatashiriki uchaguzi iwe Zanzibar au tanganyika mpaka tume huru ya uchaguzi zipatikane, yalio fanyika Zanzibar polisi pamoja na Zambië kuvamia vituo na kuwafukuza mawakala na kuingiza wapiga kura mamluki.

Pia usiku kabla siku ya uchaguzi wananchi wamaeneo hayo kuvamiwa na zombie nakupigwa na kupewa vitisho.
 
Acha uwongo CUF haijashinda popote kwani imenyang'anywa hata kile chake cha mleba.
Usilete ushabiki usiokua na maana
 
NINI KIMETOKEA KWENYE UCHAGUZI WA MARUDIO?
Na. Julius S. Mtatiro (23 Jan 2017).

Goodmorning. Katika uchaguzi huu mdogo CUF ilikuwa inatetea kata 1 ya Kimwani Muleba na CHADEMA ilikuwa inatetea kata 1 ya Duru, Babati. Kata zingine zote zilikuwa za CCM na zilikuwa zinatetewa na CCM.

Matokeo yanaonesha CCM imetetea viti vyake vyote vya udiwani (takribani 20), CUF imenyang'anywa kiti chake kimoja (Kimwani) na CHADEMA imelinda kiti chake kimoja (Duru).
 
Wakuu leo ndiyo Ile siku ya kujua kama rais Magufuli ama anapendwa ama Tayari raia washamchoka. Tupia hapa kinachojiri katika zoezi la upigaji kura na matokeo, na vipi mwitikio wa wananchi
utapimaje kwa aina ya uchaguz uliopangwa na kudhibitiwa watu fulan kushinda
 

Kiwanja cha ndege Morogoro CUF na CHADEMA mngesimamisha mgombea mmoja ukawa ingeshinda, ccm imeshinda kwa sababu mmegawana kura! Kwa nini mnashindana wenyewe kwa wenyewe? ukawa una maana gani sasa?
Kata ya Kijichi kura zote za upinzani zingewekwa kwa mgombea mmoja wa upinzani CCM ingeanguka,
Si kwamba ccm inapendwa la hasha , upinzani unapendwa zaidi ila ni vinara wa kugawana kura
 
KILIO CHETU NI TUME HURU YA UCHAGUZI TU, PIA POLISI WAFANYE KAZI YAO NA SIYO KUNYANYASA WAPIGA KURA AU KUPENDELEA UPANDE MMOJA NA SI VINGINEVYO!!!!!!!!!!!
 
hapa linahitajika litolewa tamko kulinda demokrasia .
 
Weka jumla ya kura kwa kila chama,kwani kila chama kazi yake kubwa ni kutaka kushika dola na sio kufuata miungano.
 
MATOKEO YA UCHAGUZI MDOGO WA MADIWANI KANDA YA KUSINI

HALMASHAURI YA WILAYA MBINGA
Kata ya Maguu
Waliojiandikisha 6903
Waliopiga kura 4101 (59.41%)
Kura zilizoharibika 29 (0.6%)
CCM: 2355 (57.43%)
CHADEMA: 1717 (41.86)

MANISPAA YA SONGEA.
Kata ya Tanga
Waliojiandikiaha :4870
Waliopiga Kura :2618 (53.76%)
Kura zilizoharibika :9 (0.3%)
ACT :8 (0.3%)
CCM :1819 (69.48%)
CDM :770. (29.41%)
CUF :12 (0.46%)
Kata hii tumeipoteza

Mwaka 2015 Matokeo yalikuwa hivi;
*Halmashauri ya Mbinga*
Kata ya Maguu
CCM. 3,783
CDM. 358

*Manispaa ya Songea*
Kata ya Tanga
CDM. 1,904
CCM. 1,739

Philbert Ngatunga
Katibu Kanda ya Kusini (CHADEMA)
+255787158788
 
Sijaelewa ni mwaka gani huo maana hapo chini umeandika matokeo ya Mwaka 2015! na hayo ya juu ni mwaka gani haswa? Wapinzani bila kutumia mfumo wa Gambia ule wa goroli mtapigwa sana tu.. Songea kuna kata ya Tanga? Upinzani pia unatakiwa uachane na Mafisadi Kwa mwenendo huu wa Sasa Mbowe aachie hana sifa tena za Uongozi Madeni yamemuelemea.... Akipata madaraka ndio alipanga kuyalipa?
 
Kumbe ulikuwa hujui jana kulikuwa na uchaguzi? Pia kama hujui kama Songea Mjini kuna kata inaitwa Tanga basi ungeuliza
 
Kumbe ulikuwa hujui jana kulikuwa na uchaguzi? Pia kama hujui kama Songea Mjini kuna kata inaitwa Tanga basi ungeuliza
Sipo Songea Man...! na swali mbona nimeuliza na nilitarajia Jibu zuri kutoka kwako na sio Mavi man! na kama huwezi jibu haina noma Man... Unalolifahamu wewe si kwamba wote tutalifahamu pia elimu pana sana. Me huwa Napenda Timu inayoshinda tu.. Siwezi kuteseka Man.

Ukiweka Habari ishibishe kabisa ili kuepuka other circumstance my advice tu kama utayachukua...
 
Subiri siku ifungwe uhame. Ukifanya analysis utajua ni timu gani inapanda kiwango kila awamu ya uchaguzi.
 
Subiri siku ifungwe uhame. Ukifanya analysis utajua ni timu gani inapanda kiwango kila awamu ya uchaguzi.
Mambo ya chenga twawala lakini kutufunga wametufunga niliyaachia zenji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…