Basi kaeni kimya muache siasa. Sio kulia lia kama watoto. Nani kawaambia muende si mngesusa TADEA wakafanya wenyewe.kwa niliyo yaona kwenye Uchaguzi huu Mdogo hakuna haja tena ya kuwa na Vyama vingi. ni bora CCM ikabaki yenyewe... .maana huu sio uchaguzi
Mkuu ndio lililobaki tuu. Kuna SAA unyama unalipwa kwa unyama, na hasa hawa waliopewa dhamana na kukiuka wajibu wao.Umezungumza jambo la muhimu sana na kama likifuatwa litaleta majibu mazuri ,tatizo wenzetu wanatumia nguvu sisi tunahubiri mambo ya Mungu na tuna tarajia matokeo chanya ktk Dunia yenye Watu wanaoishi kinyam
Kwikwi acha uongo unaleta taarifa za 2012Dimani kumegundulika masunduku ya kura kuna ballot paper tayari zipo zimeekewa tiki na chumba number 6 kuna masunduku hewa tayari yameingia maeneo ya fuoni na mazombi wametanda tayari wengine wamekamatwa
View attachment 462698
Siku hizi watu kujigeuzs kiwanda cha uongo hata hawaoni shida kabisaaKwikwi acha uongo unaleta taarifa za 2012
Polisi wanapochafua amani watu walindwe na nani?
Kwikwikwi nimeliumbua hilooooooooo!!!
Wakuu leo ndiyo Ile siku ya kujua kama rais Magufuli ama anapendwa ama Tayari raia washamchoka. Tupia hapa kinachojiri katika zoezi la upigaji kura na matokeo, na vipi mwitikio wa wananchi
Sijaona picha......Leo ndo leo uchaguzi wa ubunge jimbo la Dimani Zanzibar na uchaguzi wa madiwani kata 20 Tanzania bara.
Ni chaguzi zitazotoa mwelekeo na mabadiliko na ukubalikaji wa vyama tangu uchaguzi mkuu wa 2015.
Karibuni tupeane updates na matukio yanayojiri huko.
.......Updates...........
* Uchaguzi wa Ubunge unafanyika kwenye jimbo la Dimani, Wilaya ya Magharibi “B”, Mkoa wa Mjini Magharibi – Zanzibar
Uchaguzi wa madiwani unafanyika kwenye kata Ishirini (20) katika Halmashauri Kumi na Tisa (19) za Tanzania Bara, kata hizo ni...
1. Ngarenanyuki (Meru DC, Arusha),
2. Igombavanu (Mufindi DC, Iringa),
3. Ikweha (Mufindi DC, Iringa),
4. Kiwanja cha Ndege (Morogoro MC, Morogoro),
5. Ihumwa(Dodoma MC, Dodoma),
6. Kijichi (Temeke MC, Dar es Salaam),
7. Kahumulwa (Sengerema DC, Mwanza)
8. Maguu (Mbinga DC, Ruvuma),
9. Ng’hambi (Mpwapwa DC, Dodoma),
10. Kimwani (Muleba DC, Kagera),
11. Kinampundu (Mkalama DC, Singida),
12. Isagehe (Kahama TC, Shinyanga),
13. Kasansa (Mpimbwe DC, Katavi),
14. Duru (Babati DC, Manyara),
15. Malya (Kwimba D.C, Mwanza),
16. Misugusugu (Kibaha TC, Pwani),
17. Mateves (Arusha D.C, Arusha),
18. Nkome (Geita DC, Geita),
19. Lembeni (Mwanga DC, Kilimanjaro) na
20. Tanga (Songea MC, Ruvuma)
--
siyoi koroi, Uchaguzi udiwani Kata ya Ngarenanyuki DED na ccm wapora daftari la wapiga kura.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru Bwana Christopher Kazeri anatembelea vituo akiwa ameambatana na viongozi wa ccm.
Sheria za uchaguzi haziruhusu viongozi wa vyama vya siasa kupiga kambi kwenye vituo vya uchaguzi.
Hii imeweza kutokea Ngarenanyuki tu mkurugenzi wa halmashauri ambaye ni msimamizi wa uchaguzu kutembea na viongozi wa ccm.
mkurugenzi akiwa ameambatana na makada wa ccm wamewanyang'anya mawakala wa vyama daftari lenye majina ya wapiga kura.
Safari ya demokrasia kwa nchi yetu bado sana.
Hii haikubaliki popote.
Tume ya taifa ya uchaguzi kwa mtindo huu huu uchaguzi hauwezi kuwa huru na haki.
--
Francis12, UPDATES MCHAGUZI MDOGO JIMBO LA DIMANI Z'BAR.
Kumetokea mgogoro kati ya mawakala wa CUF na Askari Polisi. Hali hii imepelekea mawakala wa CUF kuondolewa kwa nguvu kwenye vyumba vya kupigia kura na hivyo mawakala wa CCM kubaki peke yao.
Sababu za mgogoro huu ni kama ifuatavyo:
-Mawakala wa CUF amegundua baadhi ya masanduku yamejazwa kura ambazo zimeshapigwa tiki kwa mgombea wa CCM.
-Mawakala wa CUF wamegundua kuwa kuna watu hawamo ndani ya daftari la kupiga kura ila wamekuja kupiga kura na wameruhusiwa kupiga licha ya majina yao kukosekana kwenye daftari.
-Chumba number 6 kituo cha Kibondeni, imegundilikana kwamba masunduku yote yaliyopo yamejazwa kura ambazo zimeshapigwa tayari.
-Wapiga kura wengi jimbo la Dimani ni hewa.
-Police wameanza kupiga watu maeneo ya Fuoni kituo cha Kibondeni baada ya watu hao kudai kuna kura feki kwenye kituo hicho.
-Katika kituo hicho cha Fuoni mabasi yamekua yakisomba watu na kuwaleta kupiga kura. Watu hao si wakazi wa jimbo la Dimani. Picha hapo chini inaonesha moja ya mabasi yanayotumika kusomba watu na kuwapeleka vituoni kupiga kura.
Kwikwi unatafuta sababu sababu nyepesi. Sasa wewe unaleta taarifa za uongo. Sasa hivi nakula sahani na wewe. Unaleta Taarifa za kupotosha. Nitakuumbua mpaka utajiona mwehu.
Wakati KC kayeyukaSijui ACT tutaambulia japo kata moja? We deserve at least one
Wewe utakuwa RAIA wa Nchi jiraniAwamu ya magufuli imezika kabisa misingi ya muasisi wa taifa hili wa haki na usawa. Na kinachoonekana wazi ndani ya taifa la Tanzania ni kiu ya kiwango kikubwa ya kumwaga damu.
Mwenye update za Zanzibar jamani maana nasikia hali sio shwari huko
Kipimo cha maDEDUKAWA Wanapumulia mipira!
Mkipigwa hamkawii kusema mmeibiwa kura[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]Lembeni, Mateves,kijichi,kiwanja cha ndege,kahama na Geita CHADEMA wameshashinda hata kabla ya uchaguzi, watangazwe tu washndi hakuna namna!
Ninamuelewa Trump sasaREF/AB/T/001/2017 22/01/2017
Mkurugenzi wa Uchaguzi,
Tume ya Taifa ya Uchaguzi,
Dar Es Salaam
YAH: UCHAGUZI WA VURUGU
Tafadhali husika na mada ya barua hii kama inavyojieleza hapo juu.
Mhe. Mkurugenzi wa Uchaguzi, kama Mgombea wa Ubunge kwa tiketi ya THE CIVIC UNITED FRONT CUF- Chama Cha Wananchi) napenda kueleza kwako ukiukwaji wa Sheria na taratibu za uchaguzi unaofanywa katika vituo mbali mbali vya uchaguzi kama ifuatavyo:-
1. Kutolewa kwa Mawakala wa Upigaji Kura wa Chama Cha CUF kinyume na sheria ya Tume yaTaifa ya Uchaguzi Na. 1 ya mwaka 1985 (Sura ya 343), na Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Na. 4 ya mwaka 1979 (Sura ya 292): Katika hali isiyotarajiwa, Mawakala wa Chama changu wametolewa na kudhalilishwa katika vituo vya kupigia kura, Kwa Mfano: Abeid Majid Abeid (Bweleo, Chumba Na. 1), Yunus Masoud Gharib (Bweleo, Chumba Na. 2), Abdi Mustafa Habib (Uwandani, Chumba Na. 6) wametolewa katika vituo vya uchaguzi. Pia tumeshuhudia mawakala wa vyama vyengine wasiokuwa wa CCM wametolewa katika vituo vyao vya kupigia kura, Kwa Mfano: Shani Khatib Khamis (NRA, Fumba, Chumba Na. 2), Mbarouk Ali Haji (NRA, Uwandani, Chumba Na. 3), Ibrahim Muharam Mwinyi (NRA, Uwandani, Chumba Na. 4), Suleiman Othman Omar (CHAUMMA, Kisakasaka, Chumba Na. 2), Masoud Khamis Ramadhan (CHAUMMA, Uwandani, Chumba Na. 3) wote wametolewa kwenye vituo bila ya sababu za msingi kwa lengo maalumu la kukinufaisha Chama Cha CCM.
2. Kubadilishwa kwa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura (DKWK): Itakumbukwa kwamba tarehe 25/10/2015 kulifanyika uchaguzi wa Mbunge wa Dimani na Chama Changu kilipatiwa Nakala ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, ni jambo la makusudi ambalo limeratibiwa na Tume yako kuandaa Daftari jipya ambalo leo wamepatiwa wasimamizi wa Vyumba vya Uchaguzi likiwa tofauti na lile lililotumikguzi Mkuu wa Oktoba,2015.Vile vile Mawakala, wangu wamegunduwa katika baadhi ya maeneo, wapiga kura halali wametolewa katika vyumba vya kupigia kura wakikoseshwa haki zao za msingi za kuchagua Mbunge wa Jimbo lao la Dimani huku wakishuhudia makundi ya wapiga kura kutoka nje ya shehia zao wanaruhusiwa kupiga kura.
3. Kuruhusiwa kwa Wapiga Kura Haramu kupiga kura: Katika hali ya kusikitisha, wapiga kura kadhaa wameripotiwa kupewa shahada za kupigia za watu wengine na kuruhusiwa kupiga kura na wasimamizi wa vituo vya uchaguzi!
4. Uchaguzi kukabidhiwa na kuendeshwa na Jeshi la Polisi na kuingiliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania: Kwa mujibu wa Sheia ya Uchaguzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ndio yenye mamlaka ya kusimamia na kuendesha uchaguzi hapa Nchini; hali inayoonekana katika vituo vyote vya uchaguzi ni kuachiwa Polisi na JWTZ kuendesha uchaguzi na kufanya wanavyotaka wakati wote kwa mfano:Tumeliona gari la JWTZ Na: 3579 JW 14 likichukuwa makundi ya watu wasiokuwa wapigakura wa Dimani na kuwapeleka katika vituo vya kupigia kura vya Fuoni Kibondeni na Kituo cha Skuli ya Sekondari ya Fuoni. Jeshi la Polisi nalo ndilo lenye kazi ya kuwatoa Mawakala pamoja na wapiga kura halali katika viyuo vya kupigia kura kinyume na taratibu za uchagzuzi.
Uchaguzi unaoendeshwa kwa mtindo huu hauwezi kuitwa uchaguzi wa haki na huru na hauwezi kuakisi maamuzi ya wapiga kura.
5. Upigaji wa kura wa Wafu: Tumegunduwa katika vituo mbali mbali wanaletwa watu wasiojulikana na kuwapigia kura watu waliofariki.Mfano mzuri ni ule unaonihusu mimi mwenyewe.
Dada yangu khalisi: Samia Khatib Ramadhan ambaye alifariki tarehe 5 Januari,2017,ambaye alikuwa mpiga kura wa Kituo cha kupigia kura cha Skuli ya Dimani,naye amepigiwa kura katika uchaguzi huu mdogo wa jimbo hili ambalo mimi ni Mgombea.Nnachotaka kufahamishwa Mheshimiwa Mkurugenzi ni sheria ipi ya Tume yako inayoruhusu Mfu kupigiwa kura?
Abdulrazak Khatib Ramadhan
Mgombea wa Uchaguzi, Jimbo la Dimani
Nakala:
Msimamizi wa Uchaguzi,
Katibu Mkuu CUF
Katibu CUF- Wilaya ya Magharibi ?B?