Mimi bado sielewi kitu, mbona naona kama mashahidi wa mashitaka ushahidi wao unafanana (kamata, kula, safirisha, weka ndani, andika) tofauti ni mashahidi, nini kinatafutwa maana sioni kutegwa kwa makombora, mabomu na mahandaki.
Nikiangalia ambacho mashahidi tayari wamesema, huko mbele ushahidi unaendelea kuwa dhaifu! Walianza na ukubwa wa vyeo na watu waliohusika moja kwa moja kukamata. Sasa wamekuja kwenye shahidi zilizo kwa watu ambao hawakuhusika au hawajui jambo zima. Mashahidi muhimu wameshakataa kusikia kulikuwa na njama. Wamekataa forensic investigation ilifanyika, wamekataa kuwa na ushahidi wa text au voice msgs, finger prints, lab test!! Polisi wanakataa hata kuwa na informer, wanajifanya waliwafahamu watuhumiwa wakati wa ukamataji!!
Shahidi ninayetaka kumsikia sasa ni Urio - aliyepelekea kesi kufunguliwa. Huyo labda ndio atakuwa na ushahidi wa maana!!