Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe leo Januari 11, 2022. SP Jumanne Malangahe amaliza kutoa ushahidi. Kesi yaahirishwa hadi Januari 13, 2022

Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe leo Januari 11, 2022. SP Jumanne Malangahe amaliza kutoa ushahidi. Kesi yaahirishwa hadi Januari 13, 2022

Mwaka jana nakumbuka, kuna mtuhumiwa mmoja alisema alimuona Urio akiletwa kituo cha polisi, na aliteswa kama wao.

Sasa leo, imejulikana Urio ni informer. Kumbe kile kipondo alichokuwa anapigwa Urio lilikuwa ni igizo! Du!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Alafu Urio ni komando tena luten wa JWTZ aliyeko kazin mpaka muda huu
 
Haya sasa DPP ameamua kuacha wasiojulikana waanikwe wazi na hatimaye wamejulikana.

Mdude na Magoti wasingeweza kamwe kumjua mtesi wao lakini kupitia kesi hii ya mchongo wamemuona kwa macho mbele ya kizimba
Halafu Kibatala asivyo na dogo atamleta Mdude mahakamani kama shahidi wa utetezi.
 
Kinachoshangaza, aliyewapa information ya mpango wa ugaidi Afande Urio, sio shahidi kwenye hii kesi na mahakama haina maelezo yake...

Huyu Urio angekuwa mtu muhimu sana mahakamani kwenye hii kesi

Sio tu hivo mkuu. Yaani inaonekana kesi nzima imetokana na taarifa (sio maelezo) ya Urio. Na wao sasa hawana hata ushahidi wa meseji au sauti ya Mbowe!! Wanasema watuhumiwa kabla hawajaenda Moro hawakuwa wakijua watashiriki uhalifu lakini wakiwa wanaenda Moshi walijua. Kwa hiyo inaonekana hawana pia ushahidi wa Mbowe kutoa maelezo kwa watuhumiwa na huku wakishtakiwa kama vile walikaa vikao na kupanga!! Wameshtakiwa kwa “hearsay”.

Cha ajabu zaidi ni shahid J4 kuiambia mahakama kuwa hakuna voice wala text records kuhusu uhalifu. Na kwa kutomleta Urio (labda kama watamleta baadae), wanafanya tuhuma nzima kama za kufikirika tu. Hivi angesema “sijui kama zipo” badala ya “hatuna taarifa”, kungekuwa na ubaya gani?

Tuna askari wa vyeo vya juu kabisa wakitoa majibu mepesi kwa mambo makubwa, ikoje huku chini kabisa??? Hatari sana!!!
 
MAHOJIANO KATI YA WAKILI WA UTETEZI PETER KIBATALA NA
SHAHIDI Na. 08 WA JAMUHURI KATIKA KESI YA MBOWE NA
WENZAKE. TAR. 10 na 11 Januari 2022. Imeandaliwa na kuhaririwa na Dr. Chris Cyrilo
Imeandikwa kutoka mahakamani na Boniface Jackob
Mahojiano ya tarehe 10 Januari 2022
Kibatala : Nafahamu wewe ni shaidi mzoefu
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Unafahamu kuwa wanaofuatilia kesi hii wanafuatilia wajibu wa
utendaji kazi wa Jeshi la Polisi?
Shahidi: Mie natimiza majukumu yangu kama shahidi, suala la watu
wanasema nini huko, siyo kazi yangu
Kibatala: Unafahamu unatakiwa kuwa na adabu unapokuwa kwenye
kizimba cha Mahakama na mchakato huu?
Shahidi: Nafahamu
Kibatala: Na unafahamu kuwa unapoambiwa uje Mahakamani siku fulani
lazima uje?
Kibatala: Uliambiwa kwamba mheshimiwa Jaji alitoa amri katika Mahakama
ya wazi kuwa 14 December 2021 alisema ukija Tarehe 15 December 2021
kuwa uje na uthibitisho?
Shahidi: Niliambiwa lakini nilikuwa njiani
Kibatala: Haya iambie Mahakama ulifanya hivyo ulipokuwa Mahakamani
kutoa uthibitisho kuwa ulikuwa unaumwa
Shahidi: Sikufanya
Kibatala: Kuna siku yoyote ile ambayo ulinyoosha mkono kumwambia
Mheshimiwa Jaji nafahamu kuna amri yako?
Shahidi: Sikunyoosha mkono
Kibatala: Kwahiyo tukuchukuliaje sasa, kwamba umeizoea sana Mahakama?
Shahidi: Si kweli kwamba nimeizoea Mahakama
Kibatala: Haya tulikuwa na likizo ya Mahakama ya wiki mbili, Je! Ulishawahi
kuandika barua kupitia mawakili wako kuwa una sababu fulani?
Shahidi: SiKufanya
Kibatala: Umefanya kazi kwa miaka mingapi huko polisi?
Shahidi: Miaka 20
Kibatala: Tukupime kwa uzoefu wako?
Shahidi: Mie mwanadamu, huwezi kunipiga kwa kukosea jambo moja
Kibatala: Wakati wa upelelezi ulikuwa ASP sasa hivi umepanda cheo. Je!
Ulipanda cheo lini?
Shahidi: Mwaka Jana Mwezi Sita
Kibatala: Ni sahihi umepandishwa cheo baada ya kufanya hizi shughuli
ambazo zilipelekea hawa (watuhumiwa) kupelekwa Mahakamani?
Shahidi: Ni kweli matukio yalikuwa yameshatokea
Kibatala: Kingai alikuwa nani wakati huo wa 2020?
Shahidi: Alikuwa ACP
Kibatala: Na sasa ni nani?
Shahidi: Ni ACP
Kibatala: Kwenye Mkoa alikuwa ni nani?
Shahidi: Mpelelezi wa mkoa
Kibatala: Sasa
Shahidi: Ni kamanda wa polisi wa mkoa
Kibatala: Nilisikia mlikuwa mnafanya kazi na Mahita. Mahita alikuwa nani?
Shahidi: Alikuwa Assistant Inspector
Kibatala: Sasa hivi ana cheo gani?
Shahidi: Inspector
Kibatala: Amepanda cheo au ameshuka cheo?
Shahidi: Amepanda Cheo
Kibatala: Na Goodluck na yeye alikuwa nani?
Shahidi: Alikuwa Constable
Kibatala: Na yeye ni nani sasa hivi?
Shahidi: Yupo kozi anasoma
Kibatala: Nilisikia unasema kuwa wakati Bwire anakamatwa ulikwepo?
Shahidi: Ndiyo nilikwepo
Kibatala: Kuna mtu yoyote ana mawasiliano ya dereva?
Shahidi: Mimi sikuchukua mawasiliano
Kibatala: Namba zake, Route yake, namba ya Daladala?
Shahidi: Hakuna Details
Kibatala: Nilisikia kuna Askari ulisema aliwekwa ku-intercept ile Daladala. Je unataarifa za Huyo Traffic?
Shahidi: Sina
Kibatala: Je kazi aliyoifanya ilikuwa ya msingi au haikuwa ya msingi?
Shahidi: Alifanya shughuli ya Muhimu
Kibatala: Kwa ushahidi wako wewe ulisema kwamba Bwire alipofanyiwa
search (upekuzi) alikutwa na simu mbili za Techno na Bundi?
Shahidi: Ndiyo nilizungumzia ila nikasema kuhusu disposal yake watakuja
kuzungumzia wengine
Kibatala: Wakati wanazichukua palikuwa na shahidi huru mwingine?
Shahidi: Hapakuwa na shahidi huru yoyote
Kibatala: PGO inaelekeza nini kuhusu kuchukuliwa mali ya mshitakiwa?
Shahidi: Inasema kuwa lazima pawe na mashahidi huru
Kibatala: Ila kwa Jambo hili hamkuona umuhimu wa shahidi huru?
Ulimwambia mheshimiwa Jaji kwanini hapakuwa na shahidi huru.?
Shahidi: Sikusema. Mimi sikushughulika na hizo simu
Kibatala: Nilisikia ulihusika kukamatwa na Muhina na Khalid, kwa ufahamu
wako walikaa ndani muda gani wakiwa wamebebeshwa kesi ya ugaidi
mpaka nyie mlipoamua muwaachie huru?
Shahidi: Mwaka mmoja
Kibatala: Baada ya upelelezi kukamilika ndiyo mkagundua kuwa hawakuwa
na kosa?
Shahidi: Taratibu zinataka wakae ndani mpaka upelelezi unapokamilika
Kibatala: Jeshi la Polisi limepanga kuwafidia nini?
Shahidi: Miye siwezi kuingolea hilo
Kibatala: Ushawahi kufuatilia juu ya afya zao hasa Muhina ambaye
amepata stress Disorder ambayo mlimsababishia nyie wakiongozwa na
wewe?
Shahidi: Walikuwa ni wahalifu
 
... that cross-exam ilikuwa balaa kubwa kaka! Anahitaji ulinzi wa jeshi la mbinguni haswa! Maombi maalumu kwa jopo la utetezi; iwe mchana iwe usiku tusiwasahau katika maombi Gabrieli na jeshi lake wakatangulie vita hivi; stadi wa kazi na directives zikitoka moja kwa moja Kiti cha Enzi!
Ameen
 
Back
Top Bottom