Yaliyojiri katika kesi ya Mbowe 26 Jan 2022. Shahidi wa 12 Luteni Denis Urio kuendelea kutoa ushahidi wake

Hapana Sina mamlaka hayo.
Ila mbowe atajifunga mwenyewe
Kwanini alikuwa anajificha ficha mawasiliano yake na urio?
Sasa mwenzie ndio kawa wa kwanza kumpigia Simu DCI.
Hayo ya kusema urio aliteswa kituoni NI ujanja tu.
Maana yeye ndo aliyechoma utambi.
Muambie jaji sasa amfunge Mbowe kwa hayo maneno ya Urio ili wewe na Kinuju mkale kitimoto huku mnakenua meno yote 32 nje
 
Mkuu jmushi1
Mashahidi wa mashtaka hawana muunganiko. Wanapingana pingana sana...
Tuwasubiri akina Adamoo watakavyorarua na kuruka ushahidi wa Kingai na kundi lake la "Wasiojulikana"
Kwa kifupi, ni kina Kingai na Urio tu ndo waliokuwa wanafahamu kuhusu ugaidi. Kwa ushahidi uliopo, siyo Mbowe wala wale wanajeshi walikuwa wakifahamu mpango wowote wa kufanya uhalifu.

Halafu haiwezekani eti hao ndo waende kufanya huo uhalifu wa kukata miti na kulipuwa vituo vya mafuta mikoa yote na eti kuhamasisha maandamano. Yani wewe wananchi waandamane kusapoti ugaidi wa miti kukatwa na vituo kulipuliwa?

Hawa waliopanga hii kesi wote ni wajinga wa kutupwa na wameli cost Taifa letu pesa za kuendesha kesi. Achilia mbali maisha ya hao wanajeshi ambao walikuwa wakihangaika kutafuta vipato vya kuendesha maisha yao na familia zao.

Bado waliwatesa mno ili wakubali kesi ya mchongo.
 
kipi kilichoanza kutokea kuteswa kwa urio.
Au urio kumpigia Simu DCI boaz kumwambia mipango ya mbowe?

Unatuuliza sisi wakati ww ndio umetumwa huku mitandaoni kuja kupotosha? Hujui lolote wala mwenendo mzima wa hiyo kesi ya kihuni, bali huu utoto wa leo wa Urio ndio umeona wa kukutoa. Ww baki unapima upepo lakini hadi sasa tunaona ushahidi wa kipuuzi ukiendelea huko mahakamani.
 
Na Yale ya kukutana mikocheni?
Na vipi miamala ya fedha aliyofanya mbowe
Vipi mawasiliano yao.
Kumbuka kabla ya kutokea mateso kule mbweni kamanda urio alimpigia simu DCI boaz akaenda mpaka ofisini kwake akakutana na afande kingai wakapeana MAELEZO ya kumfuatilia mbowe.
Hapo hakuna mtu yeyote aliyekamatwa
Hayo ya kumpigia simu huenda ndio kaelekezwa aseme!
 
Je watakubali kumpinga kamanda wao?
He watakubali waonekane NI wasaliti machoni kwa mbowe?
Maana ukisema akina adamoo Hawana makosa Ina maana lengo lao lilikuwa moja na kamanda urio kumkamatisha MBOWE.
Hawa akina adamoo na wenzake kimsingi hawana kesi kama hata baada ya kuajiriwa na mbowe waliendelea kuripoti kwa luteni urio
 
Ametia aibu sana!!! Yaani apate habari mbaya kama hizo alafu akubali kuzifanyia majaribio? Je ingetokea kweli?
Yaani hizi mambo zinachekesha sana sometimes. Walikuwa tayari kuumiza watu kirahisi tu. Yaani mtu kapanga makubwa namna hiyo halafu mnampa na watu wa kutekeleza kirahisi tu na ufuatiliaji wa kimaandazi namna hiyo. Hivi kama watu wako serious si wanafanya tukio na kutokomea? Anaulizwa ulifanya mawasiliano tena na yule aliyebaki Dar? Eti sikuona haja kwa sababu wale wengine wameshakamatwa[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Kesi ya michomgo itaenda kutisha kesho
Urio hana ushahidi zaidi ya miamala ya Airtel na tigo,

Au kusema niliahidiwa kupewa cheo ndo ushahidi?
 
Aliyetengeneza hyo kesi ni mbowe mwenyewe.
Anapiga simu kwa namba binafsi,akipigiwa apokei,anatuma hela kwa njia ya wakala.
Kwanini alikuwa anajificha ficha mawasiliano yake na urio?

Anajificha kwa Urio mtu mwenye nyota 2?!. Mbowe alishapata walinzi binafsi aliowataka, huo muda wa kupigwa mizinga na wanajeshi wenye njaa kali hakuwa nao. Isitoshe chini ya milioni moja kuna kipi cha kuficha hata akituma kwa wakala? Ukitazama hata hela aliyotumiwa huyo Urio ni hela ya mtu mwenye njaa kali. Ingekuwa ni bilioni mbili wangalau tungesema ni hela ya maana.

Mbowe hakutaka mawasiliano tena na Urio maana aliona ni wale wasumbufu wa hela za kuganga njaa. Subiri siku ukipata hela halafu jamaa yako mliyekulia huko kijijini awe anakupigia simu za mara kwa mara kukuomba heka ya kula, kisa amukusaidia kununua shamba huko bush uone hata kama utakuwa na huo muda mchafu wa kuwasiliana naye.
 
Yupo kama washabiki wa simba kipindi cha kwanza walishangilia Sana kipindi cha pili wakalishwa ndizi
 
Watakubali kumpinga kamanda wao kwani anawalisha au anawatunzia familia zao? Hivi unaongea nini dogo?
watakubali kumpinga kamanda wao?
He watakubali waonekane NI wasaliti machoni kwa mbowe?
Maana ukisema akina adamoo Hawana makosa Ina maana lengo lao lilikuwa moja na kamanda urio kumkamatisha MBOWE.
 
Hivi hawa watu wako serious na mambo ya ugaidi kweli? Kama huyu Luteni alitoa taarifa kwa DCI na wakakubaliana aendelee na utaratibu kama walivyokubaliana na Mbowe basi kazi tunayo.
Hao makomando Mbowe alikuwa anawafahamu? Kwa nn wasipeleke polisi wapelelezi wakawa undercover kama ndiyo makomando ili kupata ushahidi mzuri?
 
hakuna voice rekodi wakati mfumo unaweza na ulirekodi?
Yaani urekodi.. Habari yako? Za siku? Tutafutane... Basii
unajua maana ya ushahidi?
Yaani yawepo maneno au record kwamba sasa mabomu ya kulipua tumepata.. Eeh tayari tuna mashine 15 za kukata miti nk kisha tumpe flani kazi hii sehemu fulani nk
Yakiwepo maneno yenye mfano huo au uelekeo huo.. Mwanga wa ugaidi unaanza kuonekana
 
Makomandoo hawafukuzwi kazi. Tambua hilo. Akifukuzwa au hilo likitokea, ni straight kifungoni. Hao wengine unaodhani walifukuzwa, walitumwa huko mtaani, tactically, ili kutimiza malengo.

Read between the alphabetical letters!
Ndo maana walijibu kwamba mwanajeshi hawezi kuwa raia ila raia anaweza kuwa mwanajeshi!
Gaidi kitanzini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…