Yaliyojiri katika kesi ya Mbowe 26 Jan 2022. Shahidi wa 12 Luteni Denis Urio kuendelea kutoa ushahidi wake

Naiona Ludovick ndani ya kesi ya Lwakatare kwenye kesi ya Mbowe....nawona IGP Siro na Mwigulu Nchemba kwenye kesi ya Lwaka na Mbowe.
Kinachofurahisha sana ni pale ambapo watu wazima wanapotezea muda watu wenye nguvu ambao wangekua wazalishaji.
 
Mbowe nyumbu kweli, yaani analeta uchaga kwa wanajeshi?
Apeleke ukabila kwa wanasiasa ona Sasa anaenda kunyea debe moja na Sabaya kisa ukabila.
 

Kuhusu Mbowe kushirikiana na hao makomando, sikwamba ilikuwa ni wazo lake direct! Ina maana wapo watu waliokuwa wamechomekwa kumshauri kabla kuhusu kuwatumia ili hii kesi itengenezwe kwa namna inavyoonekana!
Btw maadam bado hatujasikia upande wake, akianza kunguruma, nyeupe haitaonekana nyeusi!
 
SA
Swali, kama hawa makamdoo walikuwa hawajapewa kazi, hawajakutana na mbowe, walijipangaje mpaka waende na bastora?
 
Unajuaje kwamba alikuwa anatafuta walinzi, kama si kutokana na ushahidi wa Lt. Urio? Ikiwa ndivyo, kwa nini usiyaamini maelezo kamili ya shahidi huyu--kwamba haikuwa biashara ya ulinzi binafsi, ila ilikuwa ZAIDI YA HAPO--misheni chafu?

FM kutopokea simu za Lt. Urio mara kwa mara kunaweza kuwa na maana kadhaa. Hakutaka Lt. Urio ajue mwelekeo wake specific kuanzia hapo.

Pili, alikuwa anafuta ushahidi wa kimawasiliano incase chochote kikija kutokea baadaye. Refer kauli ya FM kupitia Messenger, baada ya Lt. Urio kumkosa kwenye simu ya kawaida mara nyingi: ^Any news? Sikuweza kupokea simu zako kwa sababu ya (...) (...) (...). Nadhani unanielewa...^

Tatu, he had nothing to do with him anymore. Alimtumia, amewapata vijana aliokuwa akiwatafuta, then, that's it! As the famous saying goes, ^Use them, then dump them when their honey is exhausted!^

NB: Mazungumzo ya face-to-face almost 3 good hours Mikocheni!
 
Wewe inaonekana unajua kusoma "tu". Humu si kusoma tu bali na kuchambua pia,

Hiyo kazi ya kulipua vituo hadi sasa haijapata ushahidi usiotia shaka, ameyaongea Urio kama wewe unavyoweza kutunga story yoyote ukawaeleza watu.

Watuhumiwa wenyewe walikana kufanya kazi hiyo katika ushahidi wakiekeza kuwa walikwenda kufanya VIP protection.

Urio mwenyewe kwenye maelezo ya ushahidi wake hakuna sehemu ambapo amewaambia hao watuhumiwa kwamba wanaenda kufanya kazi ya kulipua vituo bali anawatuma vijana wake kwenda kufanya kazi halali ya kumlinda Mbowe ila kwa tahadhari ya kiapo chao, nao wanakubali na hata kabla ya kuanza kazi wakawahiwa kubambikiwa kazi "fake" kwenye mashtaka.

Kama Urio yeye alikuwa anajua kuwa kuna kuchoma vituo halafu akawaficha hao vijana wake akina Adamoo ili kutengeneza mtego kama inavyoonekana hili haliwezi kuhalalisha wao kuwa na nia hiyo ovu ya kutenda ugaidi bali atabaki nalo Urio maana si kwa nia wala vitendo vijana hao ktka ushahidi wao wote hakuna mahali walipohusika.

Ama hii ya kutaka kuonesha kuwa Mbowe ndiye aliyekuwa anaratibu haitatbitishwa kwa maneno tu ya Urio bali kuna zaidi yake, labda tusubiri hao mashahidi wengineo wanaokuja ila wa sasa amesha hitimisha kuwa walinzi wa Mbowe hawakuwa na hatia ktka shitaka la ugaidi.

Hata mwelekeo wa mashahidi watakaokuja hawatakuwa na jipya maana mpishi wa stori ndo huyu.



Akija mwenye ushahidi wa maana useme.
 
Freeman Mbowe akanieleza yafuatayo Kwamba Mwaka huu Kuna Uchaguzi, Sisi tumedhamiria Kuchukua Dola Kwa namna yoyote ile.
Mimi si mwanasheria lakini twaweza kujiuliza, katika maneno hayo hapo juu Mbowe walidhamiria yeye na nani kuchukua dola kwa namna yoyote ile. Binafsi sijasikia mtu mwingine akitajwa kuhusika na njama hizo. Kwa nini Mbowe alitumia uwingi. Kwa nini wengine hawajakamatwa waunganishwe kwenye kesi hii. Hivi ni kweli hizi njama alipanga, kama ni kweli, Mbowe peke yake alete taharuki nchi nzima bila kuungwa mkono hata na chama chake, viongozi wenzie au wanachama wa chama chake? Jambo kubwa kama hili lingepangwa na mu mmoja kweli au bado wengine hawajakamtwa? Nkumbuka kesi za uhaini miaka ya nyuma zilihusisha watu wengi au ugaidi kwa lengo la kushika dola ni tofauti?
 
Alafu cha ajabu gaidi anabaki anazulula na wasio na hatia ya kosa hata moja wamefanya wanawekwa kwenye mateso na kuwatesa familia zao Sasa mbona haiingii akilini?
 
Hakuna ushahidi wa sms hata moja unataka hayo maneno ya kwamba walichat hivyo hizo ni story za urio
Hata aliyoyaongea na kina Mohamed baada ya kufika Moshi hayajathibitishwa na kitu chochote zaidi ya kauli zake
Hivyo vilipuzi viko wapi? Hayo mashoka yako wapi?? Unawaza kwa kutumia makalio
Fuatilia mwenendo wa kesi, utapata majibu yake soon! BTW: They were apprehended before their dirty mission went to effect!
 
Umeishia darasa la ngapi? Yaani uwaingize watu kwenye uhalifu halafu wewe uwe salama, sasa kwanini hawakuwekewa mtego wakamatwe wakiwa wanataka kutekeleza mauaji maana taarifa zilikuwepo.
 
Unajuaje? Ushahidi tafadhali.
 
Umeishia darasa la ngapi? Yaani uwaingize watu kwenye uhalifu halafu wewe uwe salama, sasa kwanini hawakuwekewa mtego wakamatwe wakiwa wanataka kutekeleza mauaji maana taarifa zilikuwepo.
Anayedhaniwa kuwaingiza kwenye uhalifu ndiye huyo mtuhumiwa namba moja. Hadi sasa yuko chini ya vyombo vya dola. Lastly, unataka kulipangia jeshi la polisi namna ya kutenda kazi yao?

Kanuni ya ^the sooner the better,^ unaijua?
 
Alimwamini kwa kigezo cha ^Homeboy^! Jiulize, kwa nini hata alidiriki kufanya naye mawasiliano yoyote? (And, they are not blood-related?) Sababu ni ileile ya HOMEBOY!

FM kukata mawasiliano? Mbowe mwenyewe kwenye Messenger alimwambia Lt. Urio (according to shahidi wa leo): ^Nimeshindwa kupokea simu zako kwa njia ya kawaida kwa sababu (...) (...) (...) Nadhani unajua!^
 
Hapa anaepona ni bwire,, wale watatu walishaenda hadi moshi kutekeleza mission, ndo wakakamatwa
Walikamatwa wakiwa wanafanya uhalifu au wapo wa dada zao? Kulikuwa na haraka gani ya kuwakamata wakati mipango yao ilikuwa inajulikana kwanini hawakuwekewa mtego? Kwanini serikali haikuwatumia watu wao ikaacha hawa vijana kutumika, ni ushahidi upi unaonesha kuwa walikuwa Moshi kufanya uhalifu?
 
Kwa jinsi kesi inavoendelea sisi watu wa nje tutakua tunatoa maoni yetu lakin ukwel wa mambo anajua mbowe na uyo urio na serikali sion haja ya sisi kufungamana na upande wowote. Ni ngum kujua Ukweli
Sisi tunaangalia Ile beyond reasonable doubt
 
Kesho ndo kesho...nasubiri jopo la utetezi - yaani ni kama mbuzi kujileta mwemyewe kwa mpika supu...

Urioooo, unashuhudia uwongo ndugu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…