Yaliyojiri katika kesi ya Mbowe 26 Jan 2022. Shahidi wa 12 Luteni Denis Urio kuendelea kutoa ushahidi wake

Yaliyojiri katika kesi ya Mbowe 26 Jan 2022. Shahidi wa 12 Luteni Denis Urio kuendelea kutoa ushahidi wake

Naiona Ludovick ndani ya kesi ya Lwakatare kwenye kesi ya Mbowe....nawona IGP Siro na Mwigulu Nchemba kwenye kesi ya Lwaka na Mbowe.
Kinachofurahisha sana ni pale ambapo watu wazima wanapotezea muda watu wenye nguvu ambao wangekua wazalishaji.
 
Kwani nawe mchaga

Shahidi: Kitu cha Kwanza tulisalimiana Salamu za Muda Mrefu, Lakini Baada ya Salamu hizo akaniambia komredi mwaka huu wa 2020 Kuna Uchaguzi Mkuu, Hivyo Chama Changu Kimepanga Kuchukua Dola Kwa namna na Kwa Gharama Yoyote ile. Akaniambia Wewe si Unaona Watu wa wanyonge wa hali ya Chini wanavyoishi Maisha ya Shida Akanielekeza, komredi Tumefahamiana Muda Mrefu, Tunatoka Mkoa Mmoja, pia wewe ni Mchaga Mwenzangu, Tukichukua Dola Unafikiri Wewe Utakosa Cheo Cha Juu Jeshini?

Akaniambia hivyo Jeshini Kuna Watu Waliostaafu au Kufukuzwa Kazi ya Jeshi.. Wale ambao wamefanya Mafunzo Maalum ya Komandoo. Homeboy naomba unitafutie Vijana hao wenye Mafunzo Maalum ya Komando, ambao nitaambatana nao kwenye Harakati za Kuchukua Dola. Najua Watakuwa na Uwezo wa Kunisaidia Kufanya Nchi isitawalike, Kuleta Taharuki na Kusiwe na Amani.. Tutafanya hayo Kwa Kuzua Taharuki Mheshimiwa Freeman Mbowe Alisema yalikuwa ni Kulipua Vituo Vya Mafuta, Kuchoma Moto Masoko na Mikusanyiko Mkubwa Ya watu.

Kukata Miti Mikubwa iliyoota pembezoni Mwa Barabara zote, Hasa Kwenye Mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, Arusha, Mwanza, Kilimanjaro hasa Mjinwa Moshi na Barabara Kuu ya Morogoro - Iringa, Kwa Kufanya Vitendo hivyo Vitatu Kutapelekea watu Kuwa na Taharuki na Kuandamana Nchi Nzima.

Mikoa Mingine Iliyobakia Itasapoti Mikoa hii niliyo highlight.. Point Nyingine ya Mwisho ni Kuwadhuru Viongozi Wengine Wa Serikali, Ni Viongozi ambao ni Vikwazo Kwa Vyama Vya Upinzani.. Hivyo Homeboy nisaidie Kuwapata hao watu Nina Haraka nao sana, MWISHO WA MAELEZO YAKE FREEMAN.
Mbowe nyumbu kweli, yaani analeta uchaga kwa wanajeshi?
Apeleke ukabila kwa wanasiasa ona Sasa anaenda kunyea debe moja na Sabaya kisa ukabila.
 
Mimi tangu kesi inaanza mwanzo kipindi mbowe anakamatwa.nilisema kosa alilofanya mbowe NI kushirikiana na hao wanajeshi wengi hawakunielewa.

Sasa wanajionea wenyewe.

Kama alikuwa anataka ulinzi alitakiwa atafute kampuni za ulinzi sio hao.

Hao Wana viapo vya UTII.

Ila watu walinibishia humu.

Kuhusu Mbowe kushirikiana na hao makomando, sikwamba ilikuwa ni wazo lake direct! Ina maana wapo watu waliokuwa wamechomekwa kumshauri kabla kuhusu kuwatumia ili hii kesi itengenezwe kwa namna inavyoonekana!
Btw maadam bado hatujasikia upande wake, akianza kunguruma, nyeupe haitaonekana nyeusi!
 
SA
Mkuu yaani Urio anahusikaje na Kingai- ila kwa mawakili wenu wanaharakati watamuuliza swali hilo na ngoja niwachongee jibu kabisa-
Kibatala: Kingai alikujaje kutoka Arusha ambacho ndicho kituo chake cha kazi?
shahidi: Sijui
Kibatala; Mh. Jaji naomba swali langu likijibiwe
Jaji: Nimesikia shahidi anakujibu hajui
Kibatala: samahani kwa usumbufu Mh.
Swali, kama hawa makamdoo walikuwa hawajapewa kazi, hawajakutana na mbowe, walijipangaje mpaka waende na bastora?
 
Kesi ya mchongo wa kitoto kabisa sijapata kuona! Afiche ushahidi gani na wakati alimtumia pesa? Tena kuna wakati kwa kutumia namba yake kabisa?

Na hata kama ni mazungumzo ya kutafuta walinzi, bado Mbowe alihitaji kuwa “discreet”, kwasababu mawasiliano yao si kawaida kabisa kudukuliwa? Wanadukuliwa kina Makamba, Nape na Kinana ndo iwe Mbowe? Tumia akili.

Walichozungumza face to face wapi mkuu? Yani Mbowe aletewe watu ambao Urio anawaamini, halafu aendelee kuwatumia na kuwasiliana nao huku akimtenga Urio? Hivi wewe unamuamini huyo kiazi kabisa?
Unajuaje kwamba alikuwa anatafuta walinzi, kama si kutokana na ushahidi wa Lt. Urio? Ikiwa ndivyo, kwa nini usiyaamini maelezo kamili ya shahidi huyu--kwamba haikuwa biashara ya ulinzi binafsi, ila ilikuwa ZAIDI YA HAPO--misheni chafu?

FM kutopokea simu za Lt. Urio mara kwa mara kunaweza kuwa na maana kadhaa. Hakutaka Lt. Urio ajue mwelekeo wake specific kuanzia hapo.

Pili, alikuwa anafuta ushahidi wa kimawasiliano incase chochote kikija kutokea baadaye. Refer kauli ya FM kupitia Messenger, baada ya Lt. Urio kumkosa kwenye simu ya kawaida mara nyingi: ^Any news? Sikuweza kupokea simu zako kwa sababu ya (...) (...) (...). Nadhani unanielewa...^

Tatu, he had nothing to do with him anymore. Alimtumia, amewapata vijana aliokuwa akiwatafuta, then, that's it! As the famous saying goes, ^Use them, then dump them when their honey is exhausted!^

NB: Mazungumzo ya face-to-face almost 3 good hours Mikocheni!
 
Kazi ya halali kwenda kulipua vituo vya mafuta,kuchoma masoko,kukata miti?
Hivi mnasoma lakini hayo yaliyoandikwa hapo juu?au mnakurupuka tu kukoment?
Ebu Soma kwanza kilichoandikwa usikurupuke.
Mbowe kafanya mawasiliano kibao na kamanda urio na huyo huyo ndo kaenda kumchoma.
Wewe inaonekana unajua kusoma "tu". Humu si kusoma tu bali na kuchambua pia,

Hiyo kazi ya kulipua vituo hadi sasa haijapata ushahidi usiotia shaka, ameyaongea Urio kama wewe unavyoweza kutunga story yoyote ukawaeleza watu.

Watuhumiwa wenyewe walikana kufanya kazi hiyo katika ushahidi wakiekeza kuwa walikwenda kufanya VIP protection.

Urio mwenyewe kwenye maelezo ya ushahidi wake hakuna sehemu ambapo amewaambia hao watuhumiwa kwamba wanaenda kufanya kazi ya kulipua vituo bali anawatuma vijana wake kwenda kufanya kazi halali ya kumlinda Mbowe ila kwa tahadhari ya kiapo chao, nao wanakubali na hata kabla ya kuanza kazi wakawahiwa kubambikiwa kazi "fake" kwenye mashtaka.

Kama Urio yeye alikuwa anajua kuwa kuna kuchoma vituo halafu akawaficha hao vijana wake akina Adamoo ili kutengeneza mtego kama inavyoonekana hili haliwezi kuhalalisha wao kuwa na nia hiyo ovu ya kutenda ugaidi bali atabaki nalo Urio maana si kwa nia wala vitendo vijana hao ktka ushahidi wao wote hakuna mahali walipohusika.

Ama hii ya kutaka kuonesha kuwa Mbowe ndiye aliyekuwa anaratibu haitatbitishwa kwa maneno tu ya Urio bali kuna zaidi yake, labda tusubiri hao mashahidi wengineo wanaokuja ila wa sasa amesha hitimisha kuwa walinzi wa Mbowe hawakuwa na hatia ktka shitaka la ugaidi.

Hata mwelekeo wa mashahidi watakaokuja hawatakuwa na jipya maana mpishi wa stori ndo huyu.



Akija mwenye ushahidi wa maana useme.
 
Freeman Mbowe akanieleza yafuatayo Kwamba Mwaka huu Kuna Uchaguzi, Sisi tumedhamiria Kuchukua Dola Kwa namna yoyote ile.
Mimi si mwanasheria lakini twaweza kujiuliza, katika maneno hayo hapo juu Mbowe walidhamiria yeye na nani kuchukua dola kwa namna yoyote ile. Binafsi sijasikia mtu mwingine akitajwa kuhusika na njama hizo. Kwa nini Mbowe alitumia uwingi. Kwa nini wengine hawajakamatwa waunganishwe kwenye kesi hii. Hivi ni kweli hizi njama alipanga, kama ni kweli, Mbowe peke yake alete taharuki nchi nzima bila kuungwa mkono hata na chama chake, viongozi wenzie au wanachama wa chama chake? Jambo kubwa kama hili lingepangwa na mu mmoja kweli au bado wengine hawajakamtwa? Nkumbuka kesi za uhaini miaka ya nyuma zilihusisha watu wengi au ugaidi kwa lengo la kushika dola ni tofauti?
 
Reallocation is equivalent to poor planning! Hivi viraka viraka katika hii case japo mi si mwanasheria, naona kabisa ina viashiria vingi vya uongo! Haikupangwa vizuri, na inaanika uonevu wa Serikali dhidi ya watu wake. Njia inayotumika ni ya kuzimu, kufanikisha ukweli usiyokuwa wa kweli.

Eee Mungu simama na waja wako. Haiwezekani hata mara moja Mwanajeshi akashirikiana na Askari Polisi kutafuta watu wa kufanikisha Ugaidi na kuifanya nchi isitawalike. Alafu akawaacha hao watu wa kufanya Ugaidi bila uangalizi wowote, na kumonitor kwa kutumia simu tu. Haiji akilini! Kwamba Serikali iliamua kutengeneza watu wa kufanya Ugaidi na Gaidi Mkuu kwa Maslahi ya nani Sasa!!!!


Sterling kauawa Kabla ya Pigo la Mwisho! Shida ni kwamba hata Trailer tu iliharibu mambo tangu kwa Mama wa Glocery na Mlima mbogamboga na wale wa PGO! Nia ya Serikali ingeishia hapo hapo, lkn kama ni kumtia mtu hatiani kwa kesi hiyo, itakuwa ni nguvu tu ya Serikali na siyo utekelezaji wa Sheria.

Mtunzi kafeli kuimalizia vizuri, japo naamini Moses Lijenje nae atakuja kutoa ushahidi namna alivyoamua kujiondoa kwenye mpango wa Ugaidi baada ya kugundua nia ovu ya Mbowe! Maana hisia zinaniambia kuwa mko nae anafundishwa Cha kuja kusema. Ni suala la muda tu, Mungu atasimama na mwenye haki.
Alafu cha ajabu gaidi anabaki anazulula na wasio na hatia ya kosa hata moja wamefanya wanawekwa kwenye mateso na kuwatesa familia zao Sasa mbona haiingii akilini?
 
Hakuna ushahidi wa sms hata moja unataka hayo maneno ya kwamba walichat hivyo hizo ni story za urio
Hata aliyoyaongea na kina Mohamed baada ya kufika Moshi hayajathibitishwa na kitu chochote zaidi ya kauli zake
Hivyo vilipuzi viko wapi? Hayo mashoka yako wapi?? Unawaza kwa kutumia makalio
Fuatilia mwenendo wa kesi, utapata majibu yake soon! BTW: They were apprehended before their dirty mission went to effect!
 
Imagine kwenda kuwa mlinzi wa mtu anayesemekana ana viashiria vya ugaidi! Better yet, Luteni Urio aliambiwa na ^walinzi^ hao kwamba kazi yao imebadilika kutoka kuwa ya ulinzi, na sasa ni ya kwenda kumla mtu kichwa huko Moshi.

Umeona?

Sasa tuchukulie kwamba walidanganywa. Kwa nini wasingemwambia Boss wao kwamba kazi waliyofanyiwa interview na kuitiwa siyo hiyo? Au, kwa sababu ya usalama wao wenyewe, wazuge tu kana kwamba wameridhia kwenda kuitekeleza mishe husika (tactical appreciation), kisha wakasepa zao? Na hapa tunawazungumzia MAKOMANDOO, si watoto fulani wa darasa la nne!

Ina maana involvement yao huioni? Huoni wakienda kutenda uhalifu kwa hiari yao wenyewe?

Leo hii, nikimwomba rafiki yangu twende matembezini (but at the back of my mind niko na malevolence or should I say ^femalevolence,^ halafu along the way nikamshirikisha tumkabe roba hasimu wangu (Mola aepushie mbali!), then rafiki yangu huyo hana haki kabisa mbele ya vyombo vya sheria kujitetea kwamba sikuwa nimemwambia tunaenda kumtoa mtu roho. Do you understand?
Umeishia darasa la ngapi? Yaani uwaingize watu kwenye uhalifu halafu wewe uwe salama, sasa kwanini hawakuwekewa mtego wakamatwe wakiwa wanataka kutekeleza mauaji maana taarifa zilikuwepo.
 
Kuhusu Mbowe kushirikiana na hao makomando, sikwamba ilikuwa ni wazo lake direct! Ina maana wapo watu waliokuwa wamechomekwa kumshauri kabla kuhusu kuwatumia ili hii kesi itengenezwe kwa namna inavyoonekana!
Btw maadam bado hatujasikia upande wake, akianza kunguruma, nyeupe haitaonekana nyeusi!
Unajuaje? Ushahidi tafadhali.
 
Umeishia darasa la ngapi? Yaani uwaingize watu kwenye uhalifu halafu wewe uwe salama, sasa kwanini hawakuwekewa mtego wakamatwe wakiwa wanataka kutekeleza mauaji maana taarifa zilikuwepo.
Anayedhaniwa kuwaingiza kwenye uhalifu ndiye huyo mtuhumiwa namba moja. Hadi sasa yuko chini ya vyombo vya dola. Lastly, unataka kulipangia jeshi la polisi namna ya kutenda kazi yao?

Kanuni ya ^the sooner the better,^ unaijua?
 
Unarudi kulekule,ndio hapo kwenye doubt!Urio alikuwa active soldier!Inawezekanaje Mbowe amwambie amtafutie watu wa kutenda uhalifu?Wewe Huoni Kuna dosari hapo?It's either Mbowe ni Mjinga au Urio anasema uongo na kwamba aliambiwa amtafutie walinzi!
Pili,yaani Mbowe baada ya kuwapata hao wahalifu(tuassume alitaka kutafutiwa watu wa kutenda uhalifu),iweje akate mawasiliano na Urio?Mimi nilitegemea Mbowe angemuhonga Urio Ili akae kimya eti badala yake anakata mawasiliano na mtu anayejua mipango yake ya kuchoma vituo vya mafuta?Inazingua akilini?

Nashawishika kuamini ushahidi huu wa Urio ni wa kuchongwa!Mbowe asingeweza kumwambia active soldier ambaye hamjui vizuri kuhusu mipango yake ya kuvuruga amani ya nchi!
Alimwamini kwa kigezo cha ^Homeboy^! Jiulize, kwa nini hata alidiriki kufanya naye mawasiliano yoyote? (And, they are not blood-related?) Sababu ni ileile ya HOMEBOY!

FM kukata mawasiliano? Mbowe mwenyewe kwenye Messenger alimwambia Lt. Urio (according to shahidi wa leo): ^Nimeshindwa kupokea simu zako kwa njia ya kawaida kwa sababu (...) (...) (...) Nadhani unajua!^
 
Hapa anaepona ni bwire,, wale watatu walishaenda hadi moshi kutekeleza mission, ndo wakakamatwa
Walikamatwa wakiwa wanafanya uhalifu au wapo wa dada zao? Kulikuwa na haraka gani ya kuwakamata wakati mipango yao ilikuwa inajulikana kwanini hawakuwekewa mtego? Kwanini serikali haikuwatumia watu wao ikaacha hawa vijana kutumika, ni ushahidi upi unaonesha kuwa walikuwa Moshi kufanya uhalifu?
 
Kwa jinsi kesi inavoendelea sisi watu wa nje tutakua tunatoa maoni yetu lakin ukwel wa mambo anajua mbowe na uyo urio na serikali sion haja ya sisi kufungamana na upande wowote. Ni ngum kujua Ukweli
Sisi tunaangalia Ile beyond reasonable doubt
 
Kesho ndo kesho...nasubiri jopo la utetezi - yaani ni kama mbuzi kujileta mwemyewe kwa mpika supu...

Urioooo, unashuhudia uwongo ndugu...
 
Back
Top Bottom