Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Katika Mapokezi na Mkutano Mkubwa wa hadhara wa Tundu Lissu Mjini Bukoba

Mkuu Molemo , japo kwa sasa mimi ni kada wa Chama cha Mapinduzi, CCM, ni muumini wa ukweli, uwazi na kufanya siasa safi, za kupingana bila kutukanana, sio muumini wa siasa za majitaka.

Kama ni kweli TV zote zimekatazwa kurusha live mikutano ya Chadema, nawapa pole!, ila nakuomba kuwa mkweli, ni nani aliyezikataza TV zote zisirushe live mikutano ya Chadema?. Jee mnao ushahidi wowote wa hili?. Kama ni kweli na ushahidi mnao, what did you do, wakati, sheria zipo, taratibu za kufuatwa zipo na mnazijua, kanuni za TCRA za utangazaji uchaguzi mkuu ziko wazi, mmefanya nini?.

Hilo la kijana wenu kukamatwa, hapa Mkuu mwenzangu ni kuwa mkweli tuu, hakukamatwa kwasababu anarusha live mkutano wa Chadema kupitia Chadema Media You Tube Platform yenu, naomba soma vizuri charge sheet!. Kosa lake ni kurusha maudhui mtandaoni kupitia online TV bila kusajiliwa na TCRA!.

Kiukweli kabisa mkubali mkatae, katika moja ya maeneo ambayo Chadema mna matatizo ni eneo la mass mobilization na doing the right thing!.
Niliwashauri siku nyingi toka ile 2015!. Kurusha kwenye YouTube ni bure, TCRA imeweka sheria ya kujisajili na kulipia just TZS 1,000,000 kwa miaka 2, juzi juzi wamepunguza ada ya usajili hadi just TZS 500,000 tuu!. Hivi kweli Chadema ni watu wa kurusha online TV bila kusajiliwa na wakati sheria, taratibu na kanuni mbazijua!. You are not serious!.

Sasa vitu vidogo vidogo kama hivi, vinawafanya watu wenye integrity kujiuliza, maswali kama haya
Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible & mature enough opposition?

Kuwa mkweli Mkuu mwenzangu Molemo, kweli nyie Chadema are you really serious?, sasa kama vitu vidogo vidogo tuu hivi kama kujisajili TCRA kupata leseni ya kurusha maudhui mtandaoni mnashindwa!, Ikulu mtaiweza?.

Hili la media, nimewashauri sana tangu yule "jamaa yangu" alipojiunga kwenu
Elections 2015 - Mabadiliko Chanya ya Ujio wa Lowassa: CHADEMA Kuhama Ufipa!, Kuwa Makao Yake, Kituo cha TV na Redio!
Nilisema

Wakati tukijiandaa kwa uchaguzi huu, kuna kitu niliuliza humu,
Uchaguzi wa 2020, Kukumbuka shuka kumekucha, is it too little too late kwa CHADEMA or better late than never?

Better late than never, mlipieni kijana wenu ile standard fine ya TZS 5.M, sajilini TCRA mpige kazi.
P
 
Lissu anakamilisha ratiba huko kanda ya ziwa hana chake, mdomo wake umemponza. Anachukia meli,treni,daraja la busisi nk. kwa kifupi ngoja akatembee na uwepo wake unawaponza wagombea ubunge na udiwani kupitia chadema.
inshomile sio watu wazuri yaani wamemwambia JPM kuwa hawamtaki,masikini
 
Mayalla na wenzie watavuna wanachopanda
 
Yale mapokezi ya Sumbawanga na Kyerwa jana yalitisha sana.
 
Overnight success comes after 15 years.
Lissu aliutafuta UBUNGE wa Singida Mashariki kwa miaka 15.
Kama atakuwa mvumilivu kama alivyokuwa mvumilivu kwenye kuutafuta ubunge, haitachukua zaidi ya awamu mbili kuupata urais.
Hayati mwalimu Nyerere aliwahi kusema huko nyuma.
"Jakaya Kikwete anafaa kuwa Rais wa Tanzania, lakini asubiri".
Alisubiri kwa miaka 10 lakini baadaye akawa Rais.
Tundu Lissu anafaa kuwa Rais wa Inchi yetu na hata sasa, lakini asubiri lakini aendelee kuipa CCM changamoto na kuimarisha chama chake kabla ya kuingia Ikulu.
 
Lissu anakamilisha ratiba huko kanda ya ziwa hana chake, mdomo wake umemponza. Anachukia meli,treni,daraja la busisi nk. kwa kifupi ngoja akatembee na uwepo wake unawaponza wagombea ubunge na udiwani kupitia chadema.
Umeandika kwa unyonge sana. Pole sana mrembo kunywa supu ya limao siku yako itaenda vizuri
 
Mkuu Pascal Mayalla tokea ulivyotanganza nia pale kawe na wajumbe wakafanya yao...post zako nazisoma tu tahadhari, hapo nyuma nilikuwa nazingatia sasa ushauri wako ila kwa sasa nimepunguza sana umakini....Hivi ilikuwa lazima kabisa wewe kuwa kada au kuna mambo yalibanika ukaamua kuchomokea hapo.

Nilidhani Mwandishi wa Habari huru mwenye uwezo wa kuhoji, kushauri, kukemea, kushawishi ingetosha....maana taaluma hii ni jicho la jamii, ni kinywa cha jamii, ni kalamu katikati ya jamii...
 
Pamoja na maelezo yako mengi unajifanya hujui ni Nani amekataza Chadema kurushwa Live mikutano yetu.Na pia unataka Chadema ikashtaki kwa huyo anayezuia Chadema isitangazwe.

Pia unajifanya hujui hata gazeti la Tanzania Daima lilifutiwa Usajili ili kipindi hiki Cha kampeni Media zote zimtangaze mfalme wenu tu.

Na pia hushangai inakuwaje Televisheni ya Taifa TBC inazunguka na mgombea mmoja tu na Mgombea Mwenza wake ili kuwatangaza Live kwa kila mkutano kinyume kabisa na maadili ya Tume ya Uchaguzi.

Pamoja na unyama na ushenzi wote huo wananchi wameamua kuondoa utawala huu madarakani na habari wanazipata kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo Molemo Media.
 
Kila wakumbuka Azory Gwanda waandishi wa habari wanaufyata.
 
Wanabari wenyewe mmeficha mikia matakoni mnataka wananchi tufanyaje ?

Vyombo vya habari ambavyo haviwezi kupigania uhuru wake wenyewe haviwezi kuitwa vyombo vya habari ni magenge ya wapiga kelele tu.
 
Nashangaa kwa nini hajadekiwa barabara kama ilivyokuwa kwa Lowassa!

Uzuri wa siasa za upinzani Tanzania, wagombea Urais huingia kwenye uchaguzi kwa mbwebwe na baada ya uchaguzi huanza kupotea polepole!

Tanzania kuna vituko!
Kila kitabu kina zama zake.... Ndiyo maana mgombea wetu safari hii hapigi push ups jukwaani.
 
Kwanini huwa Mna wajibu watu wenye stress na hofu ya wasicho kijuwa?
Pasco ubongo wake umesha Dumaa baada ya kupata kura moja!
Wajumbe wali Mchanganya ana karibia kuwa hovyo zaidi ya Mwakembe
 
Lissu anakamilisha ratiba huko kanda ya ziwa hana chake, mdomo wake umemponza. Anachukia meli,treni,daraja la busisi nk. kwa kifupi ngoja akatembee na uwepo wake unawaponza wagombea ubunge na udiwani kupitia chadema.
Nyie we zetu napatawapi h8zi taarifa mm sijui nina shida ya kacho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…