Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Hivi Mwinyi na Mkapa wameshindwa kumshauri JK kwa kusoma upepo? Ni dhahiri chama kinaweza kumfia mikononi.
 
Hao wote wanakubaliwa na USA kwa maslahi ya Watu wa Marekani.... Hapa Gas na Mafuta ndo vimeangaliwa Zaidi kwa manufaa ya watu wa Magharibi ... si Zaidi ya hapo .... UKAWA now or never ....

 

....Kweli umepatiaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Sasa kazi Imeanza. Ccm itapasuka? Fedha zilizotumika zitarudije? Lowasa atahamia ACT kama ilivyozungumzwa? Ni mwisho wa ccm au bado kitaendelea kudunda?
 
Kwa yaliyojiri kwenye CC ni dhahiri JK anataka kuigeuza nchi hii kuwa ya kifalme.

Iwapo watanzania watabugi step na kumpigia kura 'bamdogo' basi tutarajie next President wa year 2025 atakuwa Riz-One.
Wanataka baada ya Membe afuate Makamba then Rizone.
 
Nkwingwa,

Ina maana hizo taarifa si rasmi....?
Zimetolewa kwenye akaunti inayodaiwa ni ya CCM...Ambayo sio verified...

Kwa zama hizi za mtandao lolote laweza kuibuka na kuonekana la kweli..

Kawaida taarifa rasmi hutolewa na Katibu wa NEC - Itikadi na uenezi Nape Nnauye....

Mpaka dakika hii Nape hajatoa taarifa rasmi Nkwingwa...
 
Kwa mpango huu ccm wana kazi ya ziada kupata ushindi.Asanteni kwa kuwapa urahisi wapinzani
 
Mchezo utakuwa hivi tatu ataingia Membe,Amina na Makamba mkutano mkuu Makamba ataambiwa ajitoe kwa kigezo kuwa anamuunga Membe mkono hivyo watabaki Membe na Amina kura zitapigwa Membe atashinda na kuipeperusha bendera ya ccm.
 
Kwa yaliyojiri kwenye CC ni dhahiri JK anataka kuigeuza nchi hii kuwa ya kifalme.

Iwapo watanzania watabugi step na kumpigia kura 'bamdogo' basi tutarajie next President wa year 2025 atakuwa Riz-One.

Hata mimi limenishangaza hili! Inakuwaje unamkuta Lowassa halafu unaacha jina la Membe? Kikwete na CC wamekosa busara. Tangu mbio hizi za watia nia wa CCM zianze hakuna makundi yaliyokuwa hasimu kama kundi la Lowassa na Membe. Haya makundi yalitishia kukigawa chama.

Busara ya kawaida ilikuwa kama unakata jina la Lowassa basi na jina la Membe unalikata ili kulinda UMOJA wa chama. Lakini kukata jina moja na kuacha jina jingine, ndio umekigawa kabisa chama katika makundi mawili and believe me CCM itaingia kwenye uchaguzi wakiwa sio wamoja kama Membe ndiye atapeperusha bendera ya CCM.

Mimi nafikiri mapenzi ya Kikwete kwa mke wake, yanakiua chama! Wote tunajua Membe ni changuo la WAMA na ndio wamekuwa behind his campaign all the way.
 
Huyo(Makamba) kawekwa kwa sababu kuu 4
1.Hana kundi kubwa la kuweza kumuathiri Membe kwenye NEC na Mkutano Mkuu kama walivyo hao wenzake 3 waliopitishwa nae.

2.Wanamuandalia mazingira ya 2025

3.Wanajaribu kuzuga kuwa hata vijana wana nafasi-amewakiisha kundi la vijana

4.Ni kulipa fadhila za mzee Makamba
 

Nimekuelewa vyema kabisa na hongera kwa umakini wako.
 
safi sana kaka kwa kutupa ukweli usiopingika, nimekuelewa kwa mawazo yako yakinifu, haya ndo mambo tulokuwa tunayasubiri, ccm oyeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Nhamala,
Hata mimi sielewi kwa nini hakuna msukumo mkubwa ili kupatikane tume huru ya uchaguzi.

CCM siyo wajinga eti waweke Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na timu yake ambao siyo makada wa CCM.

Kama unavyosema, tumeyaona kwa Jaji Ramadhan ambaye alikuwa ni kada wa CCM wakati akiwa Jaji nchini.

Mimi nadhani ushindi kwenye serikali za mitaa umewafanya viongozi wakuu wa upinzani kubweteka wakidhani Jaji Rubuva anaweza kumtangaza mpinzani kuwa Rais wa Tanzania au inawezekana wapinzani wameamua kuweka nguvu zote kwenye udiwani na ubunge pekee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…